Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Je ni sababu gani zinazoweza kumfanya Rais Uhuru Kenyatta kuhudumu zaidi ya muhula wake?

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
    • Author, Abdalla Seif Dzungu
    • Nafasi, BBC Swahili

Uchaguzi wa Kenya siku zote huwa na ushindani mkali lakini kura iliyopigwa tarehe 9 Agosti mwaka huu imekuwa ya ushindani mkali zaidi katika historia ya taifa hili hususan wakati ambapo rais aliyepo madarakani anaondoka.

Baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo na kura kuhesabiwa, naibu ya rais William Ruto alitangazwa mshindi huku Mpinzani wake Raila Odinga akienda mahakani kupinga matokeo hayo yaliotangazwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati

Kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi huo ,Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anahudumu muhula wake wa pili na wa mwisho, amekuwa akizozana na Naibu wake William Ruto, ambaye alichangia pakubwa ushindi wake katika chaguzi mbili zilizopita 2017

Badala ya kumuunga mkono Ruto kama alivyokuwa ameahidi hapo awali, Kenyatta aliweka uzito wake nyuma ya kinara mkongwe wa upinzani Raila Odinga, ambaye akiwa na umri wa miaka 77 alikuwa anashiriki kwa mara ya tano na huenda ikawa mara yake ya mwisho kupigania wadhfa huo.

Vile vile mbali na Ruto na Raila kuna wagombea wengine wawili waliojitosa katika kinyang'anyiro hicho nao ni George Wajackoya na Waihiga Mwaure

Ijapokuwa wagombea hao wote wanaweza kuingia madarakani mapema Septemba, iwapo Wakenya watamuingiza mmoja wao Ikulu, kuna matukio ambayo yanaweza kusababisha nchi kusubiri hadi mwaka ujao kwa Rais wa 5 kuapishwa, hatua ambayo itaongeza muda wa rais aliyepo madarakani kuhudumu hadi rais mpya atakapopatikana.

Kwa mujibu wa Ibara ya 142(1) ya Katiba, "Rais atachukua madaraka kwa muhula unaoanzia tarehe ambayo Rais aliapishwa, na kumalizika rais mpya atakapoapishwa 136 (2) (a). ) ''.

Tayari rais Kenyatta amewaondoa hofu Wakenya kuhusu iwapo ataongeza muhula wake zaidi ya miaka 10, na kuwahakikishia kwamba uchaguzi wa kumchagua mrithi wake utafanyika tarehe 9 Agosti 2022 kama ilivyo.

Hatua hii inajiri huku kukiwa na madai kutoka kwa wakosoaji wake kwamba kiongozi huyo alikuwa anapanga kuhudumu zaidi ya muhula wake aliopatiwa na katiba

Lakini Je ni matukio gani yanayoweza kumuongezea muda rais Uhuru Kenyatta kuhudumu kikatiba?

Iwapo kesi ya kupinga matokeo itawasilishwa mahakamani

Majaji mahakama ya kilele nchini kenya

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Majaji mahakama ya kilele nchini kenya

Kifungu cha 136 kinaeleza uchaguzi wa urais utafanyika Jumanne ya pili ya Agosti, katika kila mwaka wa tano. Kifungu cha 140 cha Katiba hata hivyo kinatoa nafasi kwa maswali kuhusu uhalali wa uchaguzi wa urais katika Mahakama ya Juu Zaidi.

Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?

Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya

Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake

Raila Amollo Odinga

Muungano wa Azimio la Umoja

  • Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 77 ni mhandisi aliyesomea Chuo Kikuu cha Ufundi cha Magdeburg (sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Otto-von-Guericke Magdeburg) nchini Ujerumani.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
  • Hili litakuwa jaribio lake la tano baada ya kugombea katika: 1997, 2007, 2013 na 2017.
  • Bw Odinga alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Alikamatwa, akafungwa na wakati fulani akaenda uhamishoni kwa sababu ya kupigania haki hiyo
  • Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kuanzia 2008-2013.
  • Odinga alihusika kufanikisha miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya Kibaki, kama vile miradi ya umeme vijijini na barabara.
  • Kuafikia ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia uwekezaji katika biashara ndogo ndogo na sekta ya viwanda.
  • Utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.
  • Utoaji wa vifaa vya michezo na burudani kwa ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii, kimaadili na maendeleo ya watu.
  • Kufuatia jaribio la mapinduzi ya Agosti 1, 1982, Raila Odinga alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo ya uhaini ambayo alizuiliwa bila kufunguliwa mashtaka. Tume ya Ukweli ya Haki na Maridhiano iliambiwa mwaka 2011 kwamba Odinga alikuwa na mawasiliano na mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo. Odinga amekana kuhusika kila mara. - Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

William Samoei Ruto

Muungano wa Kenya Kwanza

  • Mgombea huyu mwenye umri wa miaka 55 ana Shahada ya Uzamifu/PhD katika Ikolojia ya Mimea na BSc katika Botany na Zoology kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance ( chenye mafungamano na Kenya Kwanza).
  • Aliongoza Vuguvugu la vijana la Youth for Kanu '92 (YK'(92).
  • Wizara yake iliorodheshwa kama inayofanya bora zaidi serikalini alipokuwa Waziri wa Kilimo.
  • Alihudumu kama Naibu Rais wa kwanza wa Kenya chini ya katiba mpya ya 2010.
  • Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Eldoret Kaskazini kuanzia 1997-2007.
  • Kutenga $424 milioni kila mwaka kwa biashara ndogo ndogo za kati.
  • Kuanzisha mfuko wa elimu wa kitaifa ili kukidhi gharama zisizo za masomo.
  • Tekeleza kikamilifu sheria ya usawa wa kijinsia ya thuluthi mbili katika uteuzi wa kisiasa na kutenga nusu ya baraza lake la mawaziri kwa wanawake.
  • Mnamo 2008, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru Naibu Rais William Ruto kusalimisha shamba la ekari 100 na kulipa $ 62,500 kwa Adrian Muteshi, mkulima ambaye alimshtaki kwa kuchukua mali hiyo baada ya uchaguzi wa 2007. - Kenya Law
  • Mnamo 2011, Bw Ruto alikabiliwa na kesi kwa makosa matatu dhidi ya binadamu: Mauaji, uhamisho wa watu kwa lazima na mateso ya watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Miaka mitano baadaye mahakama ilisitisha kesi hiyo kwa msingi kwamba - ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa dhaifu. -ICC

George Wajackoyah

Chama cha Roots

  • Profesa huyo mwenye umri wa miaka 61 ana shahada ya uzamili katika sheria kuhusu maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick na shahada ya uzamili , sheria (sheria za Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Baltimore.
  • Bw Wajackoyah anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots Party.
  • Alihudumu kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
  • Yeye ni mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
  • Alifunnza somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
  • Kuhalalisha matumizi ya kiviwanda ya bangi
  • Badilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi.
  • Huduma ya afya ya bure na msaada kwa wazee, walio hatarini na wajawazito

David Mwaure Waihiga

Chama cha Agano

  • David Mwaure anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Agano.
  • Ni kiongozi wa Chama cha Agano.
  • Alihitimu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya uongozi.
  • Yeye ni wakili mkuu na amehudumu kama mwanasheria kwa zaidi ya miongo mitatu.
  • Ana kampuni ya uwakili na amewania viti mbalimbali vya kisiasa.
  • Ilianzishwa chama cha Agano mwaka 2006.
  • Kupambana na ufisadi uliokithiri.
  • kuunda nafasi za ajira.
  • Kurejesha mali ya Kenya iliyofichwa nje ya nchi.

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa

Ombi la kupinga matokeo hayo linaweza kuwasilishwa katika Mahakama ya Juu ndani ya siku saba baada ya kutangazwa kwa matokeo na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka. Ikiwa matokeo ya mwisho yatatangazwa na Tume ya Uchaguzi (IEBC) ndani ya siku 7 zilizowekwa na Katiba kwa uchaguzi wa wiki ijayo, basi malalamiko yanaweza kuwasilishwa hadi Agosti 23.

Kwa hali ya kawaida iwapo hakuna ombi lililowasilishwa kufikia Agosti 23, basi rais mpya ataapishwa Agosti 30, ambayo ni siku 14 baada ya siku ya mwisho ambayo IEBC inaweza kutangaza matokeo ya urais na kwa mujibu wa Kifungu 141(2)(a) cha Katiba ya 2010.

Mahakama ya Juu, kwa mujibu wa katiba, nayo itakuwa na siku 14 kubainisha maombi ya kupinga uhalali wa uchaguzi wa urais. Hii itachukua muda wa kuapishwa kwa rais mpya hadi Septemba 13, ikiwa maombi yaliyowasilishwa mwezi Agosti yatatupiliwa mbali na Mahakama ya Juu kama ilivyofanyika mwaka wa 2013.

Iwapo uchaguzi utabatilishwa katika Mahakama ya Juu kama ilivyokuwa mwaka wa 2017, uchaguzi mpya utafanywa kuanzia Novemba 6 - siku 60 baada ya kutolewa kwa uamuzi kulingana na Kifungu cha 140(3) - huku matokeo yakitarajiwa kutangazwa ndani ya siku 7. Ikiwa uchaguzi mpya utatangazwa mnamo Novemba 13, rais mpya ataapishwa ifikapo Novemba 27 ikiwa hakutakuwa na ombi lililowasilishwa ifikapo Novemba 20.

Ikiwa matokeo mapya yatapingwa, basi Mahakama ya Juu itapitia mchakato wa awali na rais mpya ataapishwa kufikia Desemba 11 ikiwa uamuzi utafanywa kuwa matokeo ya uchaguzi ni halali.

Iwapo Mahakama ya Juu itabatilisha matokeo mapya ya uchaguzi, Wakenya watalazimika kurejea kwenye upigaji kura Februari 4, 2023, matokeo yakitarajiwa kutolewa haraka zaidi Februari 11, 2023. Ikiwa hakuna ombi lililowasilishwa kufikia Februari 18, basi matokeo mapya yanatarajiwa. Rais ataapishwa ifikapo Februari 25.

Iwapo ombi litawasilishwa kufikia Februari 18, 2023, na kutupiliwa mbali na Mahakama ya Juu kufikia Machi 4, 2023, rais mpya ataapishwa kufikia Machi 11, 2023.

Hakuna kikomo katika Katiba kuhusu muda gani mzunguko huu unaweza kuendelea, na wakati wote huo rais aliyepo madarakani ataendelea kuhudumu hadi pale rais mpya atakapopatikana.

Awamu ya pili ya Uchaguzi

Katika uchaguzi wa urais wa Kenya, mgombea hutangazwa kuwa rais ikiwa amepokea zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi (asilimia 50 pamoja na moja); na angalau asilimia ishirini na tano ya kura zilizopigwa katika kila zaidi ya nusu ya kaunti.

Naibu wa rais William Ruto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Naibu wa rais William Ruto

Iwapo hakuna mgombea anayetimiza kizingiti hiki , uchaguzi wa marudio utafanyika ndani ya siku thelathini baada ya uchaguzi uliopita. Kwa usahihi zaidi, matokeo yatarudiwa katika mojawapo ya hali zifuatazo: ambapo mgombea anayeongoza atapokea 50% pamoja na kura moja iliyopigwa lakini hajapata 25% ya kura zilizopigwa kwa zaidi ya nusu ya kaunti zote, iwapo mgombeaji atapata 25% ya kura zilizopigwa katika zaidi ya nusu ya kaunti lakini hajapata 50% pamoja na kura moja iliyopigwa; au iwapo hakuna mgombea anayepokea 50% pamoja na moja kati ya jumla ya kura zilizopigwa wala 25% ya kura zilizopigwa katika zaidi ya nusu ya kaunti nchini.

katika tukio hili duru ya pili itafanyika kati ya mgombea au wagombea waliopata idadi kubwa zaidi ya kura. Muda ambao mchakato huu wote unahitajika kufanyika ni ndani ya siku 30. Katika kipindi chote cha marudio ya uchaguzi , rais aliyepo madarakani ataendelea kuhudumu hadi rais mpya atakapotangazwa na kuapishwa.

Iwapo mgombea mmoja wa urais atafariki kabla ya uchaguzi

Wagombea wanne wa Urais nchini Kenya
Maelezo ya picha, Wagombea wanne wa Urais nchini Kenya

Wakati kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha urais kinapopamba moto, kifo cha mmoja kati ya wagombea wanne wa urais - hali ambayo hakuna mtu angetamani itokee - kinaweza kutokea.

Katiba ya 2010, kwa kutambua uwezekano huo, imeorodhesha katika Ibara ya 38(8)(b) kifo cha mgombea wa kuchaguliwa kuwa Rais au Naibu Rais kabla ya tarehe ya uchaguzi iliyopangwa kuwa mojawapo ya sababu zitakazopelekea kufutwa kwa uchaguzi wa urais. Punde tu uchaguzi utakapofutwa , Uchaguzi mpya utalazimika kufanyika katika kipindi cha siku 60 baada ya tarehe ya uchaguzi wa awali kulingana na katiba.

Hali kadhalika uchaguzi unaweza kuahirishwa iwapo kuna janga lililotokea kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo. Wakati huu wote rais aliyepo madarakani ataendelea kuhudumu hadi uchaguzi mpya utakapofanyika na rais mpya kutangazwa na kuapishwa.

th

Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma

.