Jinsi majasusi na makomando wa Marekani walivyomnasa Maduro

/

Chanzo cha picha, Donald Trump / Truth Social

    • Author, Gareth Evans
    • Akiripoti kutoka, Washington
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Kwa miezi kadhaa, majasusi wa Marekani walikuwa wakifuatilia kila hatua na nyendo za Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.

Kilikuwa ni kikundi kidogo cha majasusi, kilichofanya kazi pamoja na chanzo kimoja cha ndani ya serikali ya Venezuela. Walimfuatilia Maduro mwenye miaka 63 kwa kila hatua, walijua wapi analala, anakula nini, anavaa nguo gani na kwamujibu maafisa wa juu wa jeshi, waliwajua hadi "wanyama wake pendwa aliowafuga" nyumbani.

Sasa baada ya kukusanya taarifa zote hizo za kijasusi, kilichofuata kikawa ni kukamilisha mpango wa kumkamata. Hilo lilitekelezwa mwanzoni mwa mwezi Disemba 2025, operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la "Absolute Resolve" ilisukwa kwa umakini mkubwa.

Hatua hiyo ilikuwa ni matokeo ya miezi ya kujipanga na mazoezi ya kijeshi ya kina, ambayo hyalijumuisha wanajeshi wa vikosi maalumu.

Wanajeshi hao walitengeneza mpaka nyumba iliyofanana kabisa na nyumba yenye ulinzi mkali ambayo Maduro alikuwa akiishi Caracas ili kufanya mazoezi ya namna watakavyiovamia, kumkamata na kuondoka naye.

Oparesheni hiyo – ambayo ni kubwa zaidi Marekani kuitekeleza Amerika ya Kusini ambao tangu enzi za Vita Baridi – ilisukwa kwa usiri mkubwa. Bunge la Congress la Marekani halikufahamishwa au kuombwa ushauri.

Toka Disemba mwanzoni, wakuu wa jeshi la Marekani pamoja na majasusi wao walisubiri wakati na mazingira muafaka wa kutekeleza shambulio hilo. Trump aliwapa ruhusa ya kushambulia siku nne kabla lakini walisubiri hali ya hewa itulie pamoja na mawingu mazito kuondoka.

'Bahati nzuri na neema ya Mungu'

Usiku wa Ijumaa ulipofika amri ya mwisho ya uvamizi ikatoka, kilichofuata ilikuwa ni oparesheni iliyochukua saa mbili na dakika ishirini na kutekelezwa kutokea angani, ardhini na baharini.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, zaidi ya ndege 150 za kijeshi – zenye uwezo wa kipelelezi, kuangusha makombora makubwa na ndege vita zilitanda angani wakati wote wa operesheni.

Wakaazi wa Caracas waliamshwa na milio mikubwa ya milipuko kutoka angani saa nane za usiku, sawa na saa tatu asubuhi kwa Afrika Mashariki.

Wakati makombora ya Marekani yakiendelea kulenga maeneo mbalimbali ya kijeshi ya Venezuela ili kuzuia jeshi kuzima mashambulizi ya Marekani, makomando wa kikosi maalumu cha Delta Force walivamia makazi ya Maduro na kumteka na kuondoka naye baada ya kukabiliana na walinzi wake.

Trump akawa wa kwanza kuthibitisha shambulio hilo na kukamatwa kwa Maduro na mkewe ambao waliondolewa Venezuela kwa helikopta, kisha kusafirishwa kwa meli ya kivita na hatimaye ndege mpaka New York ambapo wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka.

Trump hakufuatilia did not follow the mission from the White House situation room. Trump alishuhudia uvamizi huo mubashara katika kasri lake la Mar-a-Lago alisema: ''lilikuwa jambo la kuvutia kuliona, na kuwa ilikuwa kama anatazama filamu.

Wengine waliyekuwa pamoja naye kufuatilia tukio ni Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio.


Picha inaonyesha Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, Rais Donald Trump na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio

Chanzo cha picha, Donald Trump / TruthSocial

Maelezo ya picha, Trump alishuhudia uvamizi huo mubashara katika kasri lake la Mar-a-Lago
Kutoka kushoto: Waziri wa ulinzi Pete Hegseth, CMkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, Rubio na Trump

Chanzo cha picha, Donald Trump / TruthSocial

Maelezo ya picha, Kutoka kushoto: Waziri wa ulinzi Pete Hegseth, CMkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, Rubio na Trump
A photograph posted by U.S. President Donald Trump on his Truth Social account shows U.S. Secretary of Defense Pete Hegseth sitting next to Chairman of the Joint Chiefs of Staff Dan Caine as CIA Director John Ratcliffe stands next to a screen showing posts on the X.com website

Chanzo cha picha, Donald Trump / TruthSocial

Maelezo ya picha, Gen Caine (kushoto) pia alikuwepo kwenye chumba hicho
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika miezi ya hivi karibuni, maelfu ya wanajeshi wa Marekani walipelekwa katika eneo hilo, kujiunga na meli za kubeba na ndege na makumi ya meli za kivita katika operesheni kubwa zaidi kijeshi katika miongo kadhaa huku Trump akimshutumu Maduro kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na ugaidi, na kulipua makumi ya boti ndogo zinazotuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya katika eneo hilo.

Lakini dalili za kwanza za Operesheni zilikuwa angani. Zaidi ya ndege 150 - ikiwa ni pamoja na ndege za kudondosha makombora, ndege za kivita na ndege za upelelezi - hatimaye zilitumwa usiku kucha, kulingana na maafisa wa Marekani.

"Ilikuwa shughuli pevu, ngumu sana, maarifa kama yote, kutua, idadi ya ndege," Trump aliambia Fox News. "Tulikuwa na ndege za kivita tayari kukabiliana na hali yoyote."

Milipuko mikubwa ilisikika mjini Caracas mwendo wa saa nane usiku saa za ndani (06:00 GMT), na moshi mwingi ulionekana ukufuka juu ya jiji. "Nilisikia sauti kubwa, kishindo kikubwa," ripota Ana Vanessa Herrero aliambia BBC. "Ilifunga madirisha yote. Mara baada ya kuona wingu kubwa la moshi ambalo karibu limzuie kuona kinachoendelea."

Aliongeza: "Ndege na helikopta zilikuwa zikipaa juu ya anga lote la katika jiji la Caracas."

Maelezo ya video, Tazama: Moshi, milipuko na helikopta ikipaa juu ya Caracas

Muda mfupi baadaye, video zinazoonyesha ndege kadhaa angani - na zingine athari ya milipuko hiyo- ilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii. Moja ilionyesha msafara wa ndege aina ya helikopta zikipaa chini kwenye angaa za mji wa Caracas huku moshi ukifuka kutoka eneo lililoshambuliwa.

"Tuliamshwa mwendo wa saa nane kasoro robo (01:55) na milipuko mikubwa na sauti za ndege zikipaa juu ya Caracas," mmoja wa mashuhuda, Daniela, aliiambia BBC. "Kila kitu kilitumbukia gizani, isipokuwa mwanga uliotokana na mabomu yaliyokuwa yakilipuka."

Aliongeza: "Majirani walikuwa wakituma ujumbe kwenye WhatsApp kuulizia kwa uwoga kilichokuwa kikiendelea kwa kuhofia kudhurika."

BBC Verify imekagua idadi ya video zinazoonyesha milipuko, moto na moshi katika maeneo karibu na Caracas ili kubaini ni maeneo yapi haswa yaliyolengwa.

Kufikia sasa, imethibitisha maeneo matano ikiwa ni pamoja na Generalissimo Francisco de Miranda Air Base, uwanja wa ndege unaojulikana kama La Carlota na Port La Guaira, njia kuu ya Caracas kuelekea Bahari ya Caribbean.

Map showing locations of US air strikes in and around Caracas, Venezuela. Highlighted sites include Port La Guaira to the north, Fuerte Tiuna and La Carlota in Caracas, and Higuerote Airport to the east.

Baadhi ya mashambulizi ya Marekani yalilenga mifumo ya ulinzi wa anga na malengo mengine ya kijeshi, maafisa walisema. Trump pia aliashiria kuwa Marekani ilikata nguvu za umeme mjini Caracas kabla ya operesheni kuanza, lakini hakufafanua jinsi walivyofanikiwa kufanya hivyo.

"Umeme mjini Caracas ulizimwa kwa kiasi kikubwa kutokana na utaalamu tulionao," alisema. "Kulikuwa giza balaa."

'Walijua tunakuja'

Milipuko ilipokuwa ikitikisa jiji la Caracas, vikosi vya Marekani vilikuwa vikiingia nchini humo. Vilikuwa ni kikosi maalum cha Delta Force, kiengo kunachotekeleza operesheni ya hali ya juu, vyanzo viliiambia mshishika wa habari wa BBC nchini Marekani CBS. Walikuwa wamejihami vikali - walikuwa wamebeba kifaa cha kusaidia kuvunja mlango wa chuma wakilazimikia kufikia mahali salama alipo Maduro.

Wanajeshi walifika mahali alipokuwa Maduro muda mfupi baada ya mashambulizi kuanza saa nane usiku, kulingana na Jenerali Caine. Trump alielezea nyumba hiyo salama kama "ngome" ya kijeshi katika mji wa Caracas, akisema: "Walikuwa tayari wanatusubiri. Walijua tunakuja."

Wanajeshi wetu walikabiliwa walipofika, na helikopta moja ilishambuliwa lakini iliweza kuruka. "Vikosi vilivyokuwa na jukumu la kumkamata Maduro vilifika katika makaazi yake kwa haraka na uweledi wa hali ya juu," Alisema Caine.

"Waliingia hadi mahali ambapo sio rahisi kufikia, unajua tena, milango ya chuma ambayo imewekwa bila maana yoyote," Trump alisema.

Wakati operesheni ya kumkamata Maduro na mke wake Cilia Flores, ilipokuwa ikiendelea - ndipo Rubio alianza kuwafahamisha wabunge kuhusiana na hatua hiyo, uamuzi ambao umewadhabisha baadhi ya Wabunge.

"Kusema ukweli: Nicolas Maduro nikiongozi wa kiimla aliye madarakani kinyume cha sheria. Lakini kutekeleza operesheni ya kijeshi bila idhini ya Bunge na mpango wa kile kitakachofuata ni makosa makubwa," alisema Chuck Schumer,nkiongozi wa ngazi ya juu wa chama cha Democratic katika bunge la Seneti.

Kulifahamisha bunge kuhusu operesheni hiyo kabla haijafanyika kungehatarisha ufanisi wake, Rubio aliwafahamisha waandishi wa habari siku ya Jumamosi. "Bunge lina tabia ya kuvuja taarifa," Trump aliongeza.'' haingelikuwa wazo zuri."

Fire at Fuerte Tiuna, Venezuela's largest military complex, is seen from a distance after a series of explosions in Caracas

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani ilishambulia maeneo kadhaa mjini Caracas, ikiwa ni pamoja na Fuerte Tiuna, jengo kubwa la kijeshi nchini Venezuela

Katika makaazi ya Maduro, wakati vikosi vya Marekani vilipoingia, Trump anasema Rais wa Venezuela - ambaye alikuwa ameripotiwa kutegemea walinzi waCuba kuimarisha ulinzi wake kkatika miezi ya hivi karibuni - alijaribu kukimbilia kwenye chumba salama.

"Alikuwa akijaribu kukimbilia mahali salama, ambapo hapakuwa salama kwa sababu mlango ungelivunjwa ndani ya sekunde 47," Trump alisema.

"Aliufikia mlango. Hakufanikiwa kuufunga. Alikimbizwa haraka sana hivi kwamba hakuingia kwenye [chumba] kile."

Alipoulizwa kama Marekani ingelimuua Maduro, kiongozi wa kimabavu ambaye alichukua kiti cha urais mwaka 2013, angeliangekataa kukamatwa, Trump alisema: "hilo lingelifanyika."

Kwa upande wa Marekani, "wanajeshi kadhaa walipigwa risasi", alisema, lakini hakuna hata mmoja wao aliyeuawa.

Katika taarifa siku ya Jumapili, Waziri wa Ulinzi wa Venezuela Vladimir Padrino alisema "sehemu kubwa" ya walinzi wa Maduro na "askari na raia wasio na hatia" waliuawa katika operesheni ya Marekani.

Hapo awali Marekani ilikuwa imetoa zawadi ya $50m (£37m) kwa yeyote ambaye angelitoa habari zitakazowezesha kukamatwa kwa Maduro. Lakini kufikia saa kumi na dakika ishirini Jioni (04:20) kwa saa za huko siku ya Jumamosi, helikopta zilikuwa zikiondoka Venezuela ikiwa na Maduro na mkewe wakiwa, chini ya ulinzi wa Idara ya Haki ya Marekani na kuelekea New York, ambako wanatarajiwa kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu.

Takriban saa moja baadaye Trump alitangaza habari za kutekwa kwake. "Maduro na mkewe hivi karibuni watakabiliwa vikali na mkono wa sheria wa Marekani," alisema.

Ripoti ya ziada na Cristobal Vasquez