Kwaresima: Kwa nini kipindi hiki 'takatifu' ni cha kipekee kwa Wakristo duniani?

.

Chanzo cha picha, YASSER AL-ZAYYAT / AFP via Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Imeandikwa kuwa: "Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu,"(Mathayo 4:4)

Maneno haya yalisemwa na Yesu Kristo baada ya kufunga kwa siku arubaini usiku na mchana akiwa jangwani.

Wakati alipojaribiwa akiwa mlimani, kulingana na injili ya mtakatifu Mathayo, inaashiria umuhimu wa binadamu kuachana na "tamaa ya kumiliki vitu" na kuingia katika "ulimwengu wa kiroho" na kusisitiza kuhusu misingi ya imani ya kikristo, maisha ya mtu na kanuni za dini ikiwemo Kwaresima.

Kwaresima, au "mfungo mtakatifu" ni mojawapo wa kipindi muhimu na mrefu wa mfungo takatifu wa waumini wa Kikristo.

Inaashiria safari ya kiroho ambayo huanza na mfungo wa siku 40, ambayo ilitokana na yesu Kristo kufunga jangwani kwa siku arubaini, na kufuatiwa na ''wiki takatifu'' kisha sherehe ya ''ufufuo'' ambayo ni ukumbusho wa kufufuka kwa yesu Kristo kulingana na imani ya wakristo.

Katika kipindi cha Kwarisema, idadi kubwa ya waumini huudhuria misa, kuomba, kuimba na kusoma biblia, wakijikita katika kuomba msamaha na ''kurejesha maisha yao kwa Mungu.''

Mchoro wa Yesu

Chanzo cha picha, VCG Wilson/Corbis via Getty Images

Kwaresima inatokana ni "njia ya mabadiliko na kuleta mwamko mpya kwa roho ya mtu" ambayo hailengi tu kujizuia kula kwa kipindi fulani bali pia inahusisha kufunga kwa hisia, akili na moyo, pamoja na kujitahidi kufanya matendo ya huruma na kuonyesha upendo kwa wengine.

Katika kipindi hiki, muumini hujiandaa kushiriki katika "wiki takatifu" kwa unyenyekevu hadi kufikia siku ya "furaha ya ufufuo."

Kwaresima Magharibi na Mashariki

.

Chanzo cha picha, Joe Raedle/Getty Images

Kwarisema hutofautiana katika makanisa yaliyoko katika mataifa ya mashariki na Magharibi, haswa wakati wa kuanza mfungo, ingawa lengo lao huwa moja kuomba msamaha na kujiandaa kwa paska.

Kanisa la katoliki wao huanza mfungo wao siku ya Jumatano maarufu kama 'Ash Wenesday' ambapo alama ya msalaba huchorwa usoni mwa waumini kwa kutumia majivu ya matawi ambayo yalikuwa yamehifadhiwa kutoka jumapili ya matawi ya mwaka uliopita kama ishara ya kuomba msamaha.

Katika kanisa la mashariki la Orthodox, mfungo wao huanza siku ya Jumatatu. Tofauti kati ya kanisa hizi ni mfumo wa kukokotoa muda wa kufunga.

.

Chanzo cha picha, Steve Gonzales/Houston Chronicle via Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Makanisa ya magharibi hufunga kwa siku 40 kabla ya wiki takatifu, huku makanisa ya magharibi yakigawa wiki za kufunga na mada tofauti na kuzipa jina tofauti. Kanisa la Coptic huwa na "wiki ya kujiandaa" na kufanya siku za kufunga kuwa 55 (wiki ya kujiandaa, siku 40 za kufunga, na wiki takatifu'

Kanisa Katoliki halihesabu Jumapili kama siku ya kufunga. Katika sheria za kufunga, waumini hawafai kula nyama katika siku mbili muhimu, Jumatano na Ijumaa, na chakula hicho kinafaa kuliwa kwa kiwango cha wastani.

Kufunga kwa wakatoliki hujikita sana kwa maisha ya kiroho na huruma ya mtu, kwa hivyo wakati wa kufunga si kubadilisha tu lishe,bali tabia na mienendo ya mtu.

Waumini wa kanisa la Orthodox huanza kufunga siku ya Jumatatu ambayo inaitwa "Jumatatu safi" na hudumu kwa siku arubaini na kisha kufuatwa na wiki takatifu, muda huu ukichuliwa kama muda wa kutubu. Kipindi cha mfungo waumini huacha kula nyama au maziwa.

Madhehebu mengine ambayo ni ya "protestant" yanatoafutiana na kanuni za kufunga, ikilinganishwa na makanisa ya kiasili. Yao huwa mfungo wa hiari ambapo waumini huchagua kuacha vitu na tabia ambazo wamezizoea ili kuonesha kujitolea kwao.

"Kumshuhudia Yesu"

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wajibu wa Kwaresma ni "safari ya msamaha na kuunda makubaliano mapya na mungu" wengine husema ni muda wa kujitakasa, kujidhibiti na kushinda majaribio ya tabia ambazo si nzuri ili awe kama "mfano wa Kristo" pamoja na kuomba mara kwa mara na kusoma biblia ili kujiandaa kwa wiki takatifu na kushuhudia 'furaha ya ufufuo'

Kwa makanisa tofauti siku ya jumamosi na Jumapili hakuna kufunga, kwani ni wakati wa kufurahi na kusherehekea kufufuka kwa yesu Kristo.

Jumamosi ambayo watu hufunga ni "Jumamosi kuu" kabla ya pasaka. Muda wa kufunga hutaofautaina kulingana na afya ya mtu na umri.

"Jumapili ya Kwaresima kuu"

Kila jumapili ya Kwaresma huwa na maudhui yake ya kiroho ambayo humsaidia muumini katika safari yake ya kupata uokovu na msamaha.

Ifuatayo ni maudhui na mada ambazo hujadiliwa jumapili za Kwaresema hasa kupitia kanisa la Coptic

Kujiwekea hazina

Jumapili ya kwanza ya kwaresema, huhubiri amri za yesu Kristo kuhusu "hazina ya kweli" kama ilivyoandikwa katika kitabu cha mtakatifu Mathayo (6:19-20) ambayo inasema, "Msijiwekee hazina hapa duniani ambako nondo na kutu huharibu, na wezi huingia na kuiba.

Jiwekeeni hazina mbinguni ambako nondo na kutu hawawezi kuiharibu, wala wezi hawaingii wakaiba." Maudhui ya Jumapili hii ni kutoa, huruma na kuwasaidia wasio jiweza.

Majaribio

Katika kitabu cha mtakatifu Mathayo, kinasema kuwa yesu Kristo alifunga kwa siku arubaini, alijaribiwa mara tatu na shetani na alikuwa akismshinda shetani kila mara na kusema baada ya kila jaribio kuwa"imeandikwa binadamu hatoishi kwa mkate pekee" na kuongezea kuwa pia "imeandikwa usimjaribu bwana Mungu wako"

Kanisa hapa huhubiri kuwa kushinda majaribu haitokani na nguvu ya mwanadamu ila kwa nguvu za Mungu kupitia kufunga.

Mwana mpotevu

Jumapili hii hujikita kwa msamaha, kutumia hadithi ya "mwana mpotevu" ambaye alirejea kwa babake baada ya kuwa mbali kwa muda mrefu, kisha babake alimkaribisha kwa furaha. Hii ni kuashiria kuwa mbingu hufurahia iwapo mtu mwenye dhambi atatubu na kumuelekea Mwenyezi Mungu.

.

Chanzo cha picha, Sepia Times/Universal Images Group via Getty Images

Mwanamke msamaria

Katikati ya Kwaresema, kanisa la Coptic hutumia hadithi ya "mwanamke msamaria" na mazungumzo yake na yesu Kristo, kupitia kitabu cha mtakatifu Yohana 4,ambacho kinaelezea kuwa uokovu ni wa kila mtu, na kila mtu yuko na nafasi ya kuomba msamaha na kurejea kwa mungu anaye itwa "maji yaliyo hai".

Yesu amponya mtu Bethesda

Jumapili hii, kanisa la Coptic huangazia uponaji wa mwanaume mmoja eneo la Bethesda ambaye alikuwa amepooza kwa miaka 38.

Yesu alipompita kulingana na kitabu cha mtakatifu Yohana 5:6 yesu alimuuliza "Je, wataka kuponywa?" na kisha kumwambia amka chukua mkeka wako na utembee, alipoamka mara moja alikuwa ameponywa.

Kanisa hapa huzingatia nguvu za maneno ya yesu Kristo ambayo yanaweza kumtoa mtu kutoka kwenye udhaifu wake.

.

Chanzo cha picha, Fine Art Images/Heritage Images/Getty Images

Kuponywa kwa kipofu

Jumapili hii huhusishwa na miujuza ya "kupona kwa mwanaume aliyezaliwa kipofu" kisa ambacho kinapatikana katika kitabu cha mtakatifu yohana 9 ambapo yesu alimfanya kipofu kuona, huu ukiwa muujiza unaotumika kuhubiri kuhusu "kupata mwanga wa kiroho na imani"

Jumapili ya matawi

Ni Jumapili ya mwisho ya kwaresima kabla ya Jumapili ya pasaka. Kanisa la Coptic huangazia wakati yesu aliingia mjini Jerusalem kama mfalme, na kutimiza utabiri ambao umetajwa katika kitabu cha Zechariah 9:9.

"Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda."

Sherehe hii huwa ya furaha, na waumini hubeba majani ya matawi kama vile watu walivyofanya mjini Jersalem wakati yesu aliingia katika mji huo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Jumapili ya ufufuo

Hapa ndipo mwisho wa kwaresema ambapo kanisa huita "furaha ya ufufo" na "maisha mpya." Kulingana na injili ya kikristo, yesu aliwakujia wafuasi wake baada ya kufufuka na kudhibitisha kuwa kuna "maisha baada ya kifo"

Kwarisema pamoja na kanuni za kiroho, inasalia kuwa zaidi ya hafla ya kidini ya kutokula na majaribio mengine ya maisha. Ila ni wakati takatifu kwa waumini wa kikiristo, ambao wanajikita kwa roho ya kusamehe.

Kila mtu anafuata nyayo za yesu kristo za kufunga kwa siku 40 jangwani .

Hii imechangia makanisa ya mashariki na magharibi kuja na kanuni tofauti za kufuata katika safari hii ya kiroho.

Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula