Moja kwa moja, 'Ole wenu mnaocheza michezo ya paka na panya' na mikataba ya kibiashara – Trump

Trump, katika mfululizo wa machapisho ya mitandao ya kijamii, alisema pia anaweza kutoza ada za leseni kwa washirika wa kibiashara.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Sesko na Lammens waruhusu Man Utd kuwa na ndoto ya kuingia Ligi ya Mabingwa

    Manchester United match winner Benjamin Sesko and goalkeeper Senne Lammens after the 1-0 win at Everton

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Sesko na Lammens waruhusu Man Utd kuota Ligi ya Mabingwa

    Benjamin Sesko alikuwa mchezaji wa akiba wa Manchester United kwa mechi ya pili mfululizo huku Mslovenia huyo akifunga bao pekee dhidi ya Everton na kuwaweka vijana wa Michael Carrick katika nafasi ya nne.

    Siku kumi na tatu baada ya mshambuliaji huyo wa pauni milioni 73.7 kufunga bao katika dakika za majeruhi na kuokoa pointi moja dhidi ya West.

    Sesko aliendelea kutamba baada ya kumpa pasi Matheus Cunha. Kufikia wakati Cunha alipompa pasi ndefu Bryan Mbeumo, Sesko mwenye hamu kubwa alikuwa amewazidi nguvu walinzi wa Everton na alikuwa tayari kufunga bao lake la nane msimu huu.

    Cha kushangaza, mabao mawili tu kati ya hayo yalifungwa na kocha wa zamani Ruben Amorim, huku matatu yakifungwa na Darren Fletcher katika michezo miwili akiwa kama kocha wa muda na matatu chini ya Carrick, ambaye sasa ameshinda michezo mitano kati ya sita aliyocheza akiwa kama meneja.

    Ilikuwa wakati wa kusisimua baada ya muda mrefu katika mechi ambayo ilikuwa na ubora wa chini katika Uwanja wa Hill Dickinson.

    Pande zote mbili zilipambana dhidi ya ulinzi mkali, baada ya kukaa kwa karibu wiki mbili bila mchezo baada ya kucheza mapema katika raundi ya mwisho ya mechi, mechi hii ikiwa mwishoni, na bila mechi yoyote katika Kombe la FA baada ya kutolewa mapema.

    Katika mchezo wenye fursa finyu, mlinzi James Tarkowski alifanikiwa kuzuia mpira kuvuka mstari wa lango katika kipindi cha kwanza baada ya juhudi za Amad kuokolewa kiasi na Jordan Pickford.

    Kipa Senne Lammens alimnyima kinda Harrison Armstrong, ambaye alikuwa na mchezo mzuri upande wa Everton kabla ya Michael Keane kuachia mpira kwa nguvu dakika nane kabla ya mpira kuisha.

    Mpira ulikuwa unaelekea kwenye kona ya juu kushoto lakini Lammens alikuwa macho tena, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji akiokoa mpira kwa njia ya kipekee.

    Matokeo haya yanamaanisha kuwa sasa ni michezo saba ya nyumbani bila ushindi katika mashindano yote kwa Everton, ambao wako katika nafasi ya tisa.

    Soma zaidi:

  2. Trump akanusha ripoti kwamba kamanda mkuu wa jeshi la Marekani anapinga shambulio dhidi ya Iran

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump, Jumatatu jioni - Februari 23 - alikanusha ripoti kwamba Jenerali Daniel Kane, anayejulikana kama "Razen", anapinga hatua za kijeshi dhidi ya Iran.

    Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii Jumatatu jioni, Bw. Trump aliandika kwamba alizingatia ripoti hizo kuwa za "uongo kabisa" na kufafanua kuwa hakuna chanzo maalum kilichotajwa kuhusu madai haya.

    Amesisitiza kuwa: Jenerali Kane, sawa na maafisa wengine, hana mwelekeo wa vita, lakini iwapo uamuzi utatolewa wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran, anaamini kwamba atashinda kwa urahisi mzozo huo.

    Bw. Trump aliongeza kuwa Jenerali Kane anaifahamu vyema Iran kwa sababu aliamuru Operesheni ya Midnight Hammer, mashambulizi ya anga dhidi ya vituo vya Irani majira ya joto yaliyopita.

    Kufuatia shambulio hilo, alisema, mpango wa nyuklia wa Iran "hautaendelea tena" kwani "umeharibiwa kabisa" kufuatia mashambulizi ya ndege za Marekani za B-2.

    Rais wa Marekani alimtaja Jenerali Kane kama "shujaa mkubwa" na kusema anawakilisha "jeshi lenye nguvu zaidi duniani."

    Bw.Trump aliongeza kuwa kamanda huyo wa kijeshi wa Marekani hajawahi kusema kuchukua hatua dhidi ya Iran au hata mashambulizi machache - aliyoyaita "ya uwongo" - na analenga tu "ushindi" na ataelekeza operesheni hiyo ikiwa shambulio litaamriwa.

    Pia alisema kwamba nyenzo zote zilizochapishwa kuhusu uwezekano wa vita na Iran hazikuwa sahihi na ni za makusudi.

    Alisisitiza kwamba uamuzi wa mwisho ni juu yake na kwamba angependelea kufikia makubaliano na Iran, lakini kwamba ikiwa hakuna makubaliano yatafikiwa, "siku hiyo itakuwa mbaya sana kwa nchi hiyo" na, alisema, "kwa bahati mbaya kwa watu wake," ambao aliwataja kuwa "wakubwa na wanaostahili."

    Vyombo kadhaa vya habari vya Marekani, kama vile Wall Street Journal, Washington Post, na New York Times, vimechapisha ripoti katika siku chache zilizopita, vikinukuu "vyanzo vya habari" visivyojulikana, vinavyoelezea chaguzi, sifa, na majadiliano ndani ya White House kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran.

    Soma zaidi:

  3. Habari za hivi punde, Iran yaonya: Hatuna kitu kama mashambulizi ya mipaka; shambulio lolote halitahusu vita kati ya nchi hizo mbili pekee

    Iran imeonya kwamba uwezekano wa mashambulizi ya Marekani dhidi ya nchi hiyo hautafanyika kwa nchi mbili pekee.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran anasema hakuna kitu kinachoitwa shambulio lenye mipaka na operesheni yoyote dhidi ya Iran itakabiliwa na jibu kali.

    Hapo awali, baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kwamba Donald Trump alikuwa akizingatia shambulio dogo dhidi ya Iran ili kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu kukubali mistari myekundu ya Marekani kwa kufikia makubaliano.

    Israel pia imeonya kuwa shambulio la kisasi la Iran dhidi ya nchi hiyo litakuwa kosa kubwa zaidi katika historia ya Jamhuri ya Kiislamu.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Watu 15 wafariki baada ya helikopta kuanguka wakati wa uokoaji wa mafuriko Peru

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Watu kumi na tano wamefariki baada ya helikopta ya kijeshi inayotoa huduma za uokoaji wakati wa mafuriko makubwa kusini mwa Peru kuanguka siku ya Jumapili.

    Jeshi la Anga la Peru lilisema helikopta ya Mi-17 ilipoteza mawasiliano wakati ikifanya kazi katika eneo la Arequipa, ambalo limekumbwa na mvua kubwa na mafuriko.

    Maafisa walisema timu za uokoaji zilipata mabaki ya helikopta hiyo katika wilaya ya Chala Jumatatu. Watoto saba walikuwa miongoni mwa abiria 11 na wafanyakazi wanne waliofariki.

    Helikopta hiyo ilikuwa imetumwa kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji katika eneo hilo huku maporomoko ya matope na mito iliyofurika ikisababisha uharibifu mkubwa.

    Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba baadhi ya wanajeshi waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa na jamaa walioandamana nao. Mmoja wa waathiriwa alikuwa na umri wa miaka mitatu.

    Jeshi la Anga la Peru lilisema: "Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia, marafiki, na familia nzima ya FAP kwa msiba huu wa wafanyakazi wetu na abiria."

    Uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo, maafisa walisema.

    Mvua kubwa imesababisha mafuriko makubwa katika eneo la Arequipa nchini Peru na kusababisha maporomoko ya matope, mitaa iliyofurika maji, nyumba na miti kuanguka.

    Pia unaweza kusoma:

  5. 'Ole wenu mnaocheza michezo ya paka na panya' na mikataba ya kibiashara – Trump

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump ameonya nchi dhidi ya kujiondoa katika mikataba ya kibiashara iliyojadiliwa hivi karibuni na Marekani baada ya Mahakama ya Juu Zaidi nchini humo kutoa uamuzi kuwa ushuru wake wa dharura siyo halali, akisema kwamba ikiwa watafanya hivyo, atawatoza ushuru mkubwa zaidi chini ya sheria tofauti za kibiashara.

    Trump, katika mfululizo wa machapisho ya mitandao ya kijamii, alisema pia anaweza kutoza ada za leseni kwa washirika wa kibiashara huku kutokuwa na uhakika kuhusu hatua zake zijazo za ushuru kukiathiri uchumi wa dunia.

    "Nchi yoyote inayotaka 'kucheza mchezo wa paka na panya' na uamuzi wa kipuuzi wa mahakama ya juu zaidi, hasa zile ambazo 'zimeiibia' Marekani kwa miaka mingi, na hata miongo kadhaa, zitakabiliwa na ushuru wa juu na mbaya zaidi, kuliko ule ambao wameukubali hivi karibuni. MNUNUZI TAHADHARI!!!" Trump aliandika kwenye mtandao wa Truth Social.

    Trump alisema kwamba licha ya uamuzi wa mahakama wa kubatilisha ushuru wake chini ya Sheria ya Dharura ya Kiuchumi Kimataifa, uamuzi wake umethibitisha uwezo wake wa kutumia ushuru chini ya mamlaka zingine za kisheria "kwa njia yenye nguvu zaidi na ya kuchukiza, kwa uhakika wa kisheria, kuliko ushuru kama ulivyotumika awali."

    Alipendekeza kwamba Marekani inaweza kutoza ada mpya za leseni kwa washirika wa kibiashara, lakini hakutoa maelezo yoyote.

    Msemaji wa ofisi ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni zaidi kuhusu mipango ya Trump.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Hujambo msomaji wetu. Karibu katika matangazo yetu mubashara, tarehe ni 24/02/2026.