Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Man United kumrudisha kiungo wa Scotland Scott McTominay kwa £70m

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United wanafikiria kumsajili tena kiungo wa Scotland Scott McTominay kwa euro 80m (£70m) msimu ujao, huku Napoli ikiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 miaka miwili tu baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Old Trafford. (Fichajes - In Spanish)

Real Madrid wanafuatilia kwa karibu hali ya beki wa kati wa Tottenham Micky van de Ven mwenye umri wa miaka 24, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi akiwa hajakubaliana na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza. (TeamTalks)

Brighton wanatarajia kupata dili la winga wa Cologne Mjerumani mwenye umri wa miaka 19 Said El Mala kwa kumsajili pia kaka yake mkubwa, mshambuliaji Malek mwenye umri wa miaka 20. (Time - Subscription Required)

Manchester United wamefurahishwa na kiungo wa kati wa Nottingham Forest na Ivory Coast Ibrahim Sangare, 28, katika kutafuta mbadala wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil Casemiro, 34. (GiveMeSport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sangare

Casemiro atakuwa na chaguo la kuhamia Marekani mkataba wake Manchester United utakapomalizika, huku kiungo huyo akiwa tayari kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka. (Telegraph - Subscription Required)

Liverpool wanaweza kufikiria mpango wa kubadilishana na Real Madrid ambao utamleta winga wa Brazil Rodrygo, 25, Anfield na kuruhusu kiungo wa kati wa Hungary Dominik Szoboszlai, 25, kujiunga na wababe hao wa Uhispania. (Fichajes - In Spanish).

Meneja wa Chelsea Liam Rosenior anasitasita kumruhusu mshambuliaji wa Uingereza Liam Delap mwenye umri wa miaka 23 kuondoka msimu huu wa joto, huku klabu nyingine ya Ligi ya Premia Everton ikimtaka. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Liam Rosenior

Crystal Palace itamruhusu meneja wa Austria Oliver Glasner kuendelea kuinoa timu hiyo hadi mwisho wa msimu. (Football Insider)

Aston Villa, Crystal Palace na Wolves ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa kushoto wa Scotland Andy Robertson, iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ataondoka Liverpool msimu huu. (Caught Offside)

Nottingham Forest inaweza kuwa tayari kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Brazil Igor Jesus, 24, mwishoni mwa msimu huu. (Football Insider)