Uchaguzi Kenya 2022: Kwa nini uchaguzi wa Kenya mwaka huu ni muhimu?

Chanzo cha picha, AFP
- Author, Yusuf Jumah
- Nafasi, BBC Swahili
Kenya inajitayarisha kwa uchaguzi wake mkuu wa Agosi tarehe 9 mwaka huu huku hamu ya wengi ikiangazia matokeo ya kinachoonekana kama kitakachokuwa kinyang'anyiro kikali kati ya ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na naibu wa rais William Ruto.
Kikubwa hata hivyo ambacho kinaufanya uchaguzi huu kuwa wa kipekee Kenya ni kuvunjika kwa uhusiano wa kisiasa kati ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto
.Kilichoanza kama 'ndoa' thabiti iliyojaa matumaini na mpango ulioonekana wa kudumu wa kupokezana madaraka baada ya miaka kumi ya hatamu ya rais Kenyatta -sasa kimegeuka kuwa talaka yenye vishindo,lalama,madai ya usaliti na uhasama wa kiasa ambao kwa mujibu wa kauli zinaztolewa na viongozi wa marengo hiyo miwili ,imeleta mgawanyiko nchini humo.
Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma
UNAYOFAA KUJUA:Uchaguzi Kenya 2022: Je Naibu wa rais wa Kenya William Ruto anakabiliwa na changamoto gani katika kumteua naibu wake wa rais?
Rais Kenyatta alianza ushirikiano wake na Bw Odinga kupitia mchakato wa handshake-maridhiano kati yao ambayo yalifaa kuleta utulivu nchini na baadaye yakazaa mapendekezo ya BBI yaliyokuwa na dhamira ya kubadilisha katiba.
Hilo lilifichua mpasuko mkubwa kati ya rais na naibu wake ingawaje palikuwepo na minong'ono kwamba uhusiano kati yao tayari ulikuwa umeanza kushuhudia changamoto .
Rais na washirika wake pia kupitia chama cha Jubilee ambacho waliunda na Ruto wameonyesha ishara kwamba watakuwa nyuma Bw.Odinga katika uchaguzi huu ambao huenda ni wake wa mwisho kuwania -ambao utakuwa wa tano sasa.
Wameunda muungano -Azimio la Umoja ili kumenyana na Ruto ambaye alikihama chama tawala na kuunda chama United Democratic Alliance ambacho sasa kipo katika mrengo wa Kenya Kwanza baada ya kuungana na chama cha ANC cha Musalia Mudavadi na Ford-Kenya cha Moses Wetangula
Kipute kikali cha uchaguzi ambao rais aliye madarakani hayupo mbioni lakini ameonyesha wazi kwamba anataka kuwa na jukumu kubwa la kuamua mrithi wake dhidi ya mshirika wake wa zamani kisiasa na ambaye ameweza kumega idadi kubw aya wabunge na viongozi kutoka ngome yar ais,ni jambo moja zito ambalo linaufanya uchaguzi wa Kenya kuwa wa kipekee mwaka huu.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya wana mengi ya kusema kuhusu kitakachofanyika na maswali yapo.
Je, rais atafaulu kutumia ushawishi wake kama kiongozi aliye madarakani kumpa ushindi mgombeaji ambaye anataka awe mrithi wake? Je,kutakuwa na athari gani au matokeo yake iwapo rais aliye madarakani Kenya atabwagwa na mrengo wa naibu wake?
Uzito na umuhimu wa uchaguzi wa mwaka huu Kenya unachochewa na masuala mengi lakini haya ,yanajitokeza bayana kuupa uchaguzi huu umuhimu wa kipekee kuliko chaguzi za hapo awali nchini Kenya tangu siasa za mfumo wa vyama vingi .
Rais hatetei kiti chake lakini ameshafanya chaguo lake
Rais Uhuru Kenyatta sio mgeni wa siasa za Kenya na kinachojirudia mwaka huu ni kile ambacho amewahi kukipitia ingawaje wakati huo mwaka wa 2002,yeye alikuwa mgombeaji aliyeonekana kama mradi wa serikali ya wkati huo ya rais wa zamani hayati Daniel Moi.
Kama uchaguzi wa mwaka huo,uchaguzi wa mwakaa huu utawahusisha wagombeaji ambao hawashikilii nafasi ya urais.Kenyatta hakitetei kiti chake na kwa hivyo ni kura ya kumpokeza madara kiongozi mwingine .

Chanzo cha picha, Reuters
Hilo pekee kwamba utawala wan chi utabadilika,ni jambo zito kwa Kenya kwani imefanyika tu mara mbili-baada ya uchaguzi wa 2002 ambapo rais Moi alimkabidhi madaraka mshindi wa uchaguzi huo rais mstaafu Mwai Kibaki aliyemshinda Uhuru Kenyatta na baada ya uchaguzi wa 2013 wakati Kibaki alipompokeza madaraka rais Kenyatta .
Makabidhiano mengine ambayo yalitokea ingawaje kwa hali tofauti ni mwaka wa 1978 wakatoi Moi alipoapishwa kuchukua usukani baada ya kifo cha rais wa kwanza wa Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta .
Rais Kenyatta anajua fika umuhimu na mchango wake katika siku za baada ya uongozi wake.ameeleza wazi kupitia kauli zake za hivi punde kwamba lengo lake ni kuliunganisha taifa na anaamini ataafikia hilo kwa kumuunga mkono Bw.Odinga .
Matumaini ni kwamba ataweza kutumia ushawishi wake kisiasa kuzileta kura za ngome yake yae neo la kati mwa Kenya(Mlima Kenya) katika kapu la Odinga .
Lakini wadadisi wanasema hatua hiyo ina hatari.Tayari mrengo wa naibu war ais umedai kwamba Odinga ni mradi wa serikali na ameshawekwa kapuni na matajiri ambao wanataka ayalinde maslahi yao.
Ruto na kundi lake wametumia hilo kama kigezo cha kutawaka wapiga kura kumtompa nafasi ya urais Bw.odinga wao wakijinadi kama 'watetezi wwa wanyonge'.Wakiahidi kuboresha uchumi wa kuanzia chini ,mashinani hadi juu kupitia wanachokiuza kama 'Bottom-up'.
Ni muda ndio utakaoamua uamuzi huo war ais utazaa matunda yapi kwani tayari kuna mpango kwa kiongozi huyo wan chi kwenda mstari wa mbele kumfanyia kampeni Bw.Odinga .
Rais Kenyatta mwenyewe anafahamu vyema jinsi alivyotajwa kama mradi wa serikali wakati rais Moi alipomuunga mkono kuwania urais kwa mara ya kwanza mwaka wa 2002.
Kinaya ni kwamba wakati huo Odinga alikuwa miongoni mwa waliompinga rais Kenyatta na Bw.Ruto alikuwa upande wa rais Kenyatta.Siasa kwa kweli hazina uadui wala urafiki wa kudumu .
Kupima mipaka ya kinachowezekana na kisichowezekana katika siasa
Uchaguzi wa Kenya mwaka huu pia huenda ukaandikisha historia kwa mengi mengi katika demokrasia ya ndani.Kando na kwamba naibu wa rais William Ruto anataka kudhihirisha uwezo wake wa kumshinda bosi wake bila usaidizi wake, hatua yake hiyo pia imewafanya wengi kutaka kushuhudia mambo ambayo yanaweza kufanyika na yasioweza kufanyika katika siasa.
Marais wamewahi kushindwa katika chaguzi Afrika ,lakini wengi huwa hawaamini kwamba matamanio yao yanaweza kushindwa pia kupitia kura .
Ni wachache wanaoweza kuelewa kinachofanyika kwa sababu pia marais wengi wamefaulu kushinda ama kuwapa ushindi wagombeaji ambao wanawapendelea kuwa warithi wao.Uchaguzi huu wa Kenya utazaa moja ya hilo.
Yaani huenda mgombeaji anayeungwa mkono na rais akashinda uchaguzi kuwa mrithi wake ama akashindwa kama ilivyofanyika mwaka wa 2002 kenya wakati Kenyatta mwenyewe alipokuwa akiungwa mkono na Moi na kushindwa .
Historia pia itaandikishwa katika maeneo yan chi na jinsi wapiga kura watakavyofanya maamuzi yao .
Kura nchini Kenya kwa kiasi kikubwa hupigwa kwa misingi ya kikabila .
Hesabu hizo na historia ya zamani pia zitawekwa kwenye mizani mwaka huu.Itawezekana kwa rais Uhuru kwa mfano kulishawishi eneo la Mlima Kenya kumpa kura nyingi Bw.Odinga?
Iwapo hilo halitafanyika na Ruto afaulu kuzipata kura nyingi,litakuwa jambo zito.Litakuwa na ujumbe mkubwa kuhusu ushawishi wa rais Kenyatta kwa ngome yake .
Mapambano ya uongozi katika maeneo ya mashinani,ugatuzi na raslimali
Kando na kura ya kumchagua rais ,uchaguzi wa mwaka huu huenda utakuwa wenye wagombeaji wengi zaidi kuwahi kujitokeza kuwania viti mbali mbali.
Tangu kupitishwa kwa katiba mpya inayoruhusu mgombeaji kuwania kiti chochote kama mgombea huru bila haswa kufadhiliwa na chama cha siasa ,idadi ya wagombeaji wa nyadhifa za kisiasa imekuwa ikiongezeka na hilo litadhihirika pia katika kura yam waka huu .

Chanzo cha picha, AFP
Tayari serikali na utumishi wa umma imekuwa mwathiriwa wa hilo kwa idadi ya wajuu ya watumishi wa umma kuanzia ngazi na uwazi ambao wameacha kazi ili kujiingiza katika siasa .
Hilo limechochewa na ugunduzi mkubwa kwamba ugatuzi umesababisha raslimali kupelekwa mashindano karibu na wananchi .
Nyadhifa kama ugavana ambazo awali wengi hawakujua nguvu na ushawishi wake zimewavutia wagombeaji wengi kuliko ilivyowahi kutokea katika chaguzi zilizopita .
Nafasi za uakilishi wadi,ubunge,useneta na mwakilishi wa akina mama zimewavutia wagombeaji wengi katika uchaguzi wa mwaka huu hatua inayoashiria ushindani mkali unaotarajiwa katika kura za mwaka huu .
Hilo pia linakupa taswira ya kiasi cha fedha na raslimali zitakazotumiwa na wagombeaji kuwashawishi wapiga kura kuwapa dhamana ya uongozi .
Wanaoshikilia madaraka katika ngazi hizo za chini wana mchango mkiubwa wa maendeleo ya sehemu hizo nan chi kwa jumla .
Uwanja wa siasa hizo za mashinani umefungua fursa kwa wagombeaji wengi na kuzidisha uzito ambao kura yam waka huu itebeba .
Wapiga kura nao wamegundua umuhimu wa kuwa na usemi kuhusu watendakazi wa kisiasa wanaowaakilisha kitaifa na hivyo wanalipa uzito mkubwa sana zoezi la kuamua ni viongozi wa aina gani wanapewa dhamana kuchukua uongozi .
Usalama wa Kanda na Biashara
Kenya ni taifa lenye umuhimu wa kipekee katika kandaaya Afrika mashariki na kati na upembe wa Afrika.Kinachofanyika nchini Kenya huwa na athari kwa nchi Jirani na uchaguzi wa mwaka huu nchini humo umezua maskio kwa nchi hizo kufahamu kinacheoendelea kisiasa .
Wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007/08 Nchi kama Uganda,Rwanda na DRC ziliathirika sana kibiashara wakati usafiri ulipokatizwa na mpaka kufungwa Kenya ilipokuwa katika msukosuko huo wa kisiasa.
Umuhimu wake pia umedhihirika wakati inapotokea kwa rais wa taifa Jirani la Uganda kujitokeza na kusema kwamba haungi mkono mgonbeaji yeyote katika uchaguzi wa Kenya .
Museveni aliaminika kuwa mshirika wa karibu wa naibu wa rais William Ruto ambaye Pamoja na ujumbe wake wamekuwa wakifanya ziara za kibinafisi kwenda Uganda na hata Ruto aliwahi kumfanyia kampeni rais Museveni katika eneo la Sebei ambalo lina watu wenye uhusiano wa karibu na jamii ya Wakalenjin nchini Kenya.
Uhusiano huo ulisababisha pawepo na uvumi kwamba huenda Museveni alikuwa akiegemea upande wa Ruto lakini rais huyo alilazimika kutoa tamko kwamba Uganda iko tayari kufanya kazi na mgombeaji yeyote atakayeshinda uchaguzi wa Kenya .
Kenya pia ina wanajeshi wake katika kundi la Amisom nchini somali linalolinda amani na uchaguzi wa mwaka huu unaangaliwa kwa makini na wadau wanaofanikisha mipango kama hiyo ili pasiwe na athari kwa misheni kama hiyo ya nchini Somalia .
Umuhimu wa uchaguzi wa Kenya mwaka huu pia umedhihirika wakati mabalozi wa nchi za ulaya na Marekani walipotaka hakikisho kutoka kwa serikali kwamba uchaguzi utafanywa kwa njia ya amani na utakuwa wa haki na uwazi .
Mawaziri wakiongozi na waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiang'i walilazimika kuwahakikishia mabalozi hao na wajumbe kutoka UN kwamba usalama utadumishwa kuhakikisha uchaguzi unafanywa kwa njia shwari na demokrasia inatekelezwa.
Mabalozi hao pia walitaka hakikisho la kulindwa kwa maslahi yan chi zao kama vile uwekezaji na miradi inayoendeshwa Pamoja na serikali zao.
Ahadi za kampeni zinazotolewa na wagombeaji .
Kila kipindi cha uchaguzi huambatana na vifurushi vya ahadi kutoka kwa wagombeaji wakuu wa siasa na mwaka huu sio tofauti .uzito wa baadhi ya ahadi hizo kwa taifa na kwa Maisha ya wananchi zinaufanya uchaguzi wa mwaka huu kuwa wa umuhimu mkubwa .
Ingawaje miungano mikubwa miwili haijatoa rasmi manifesto kwa wapiga kura ,matamshi ya ahadi zinazotolewa yanatoa taswira ya kila wanachosimamia na wanacholenga kutekeleza ingawaje nutekelezaji wa ahadi za kisiasa ni kitu tofauti sana Kenya .
Kando na ahadi inayokumbukwa na wqengi sana katika uchaguzi wa 2002 ya rais mstaafu Mwai Kibaki kuanzisha masomo ya bila malipo klatika shule za umma .
Ahadi nyingi za wanasiasa husalia kuwa maneno.Chama cha Jubilee kiliahidi viwanja kadhaa vikubwa vya michezo na kompyuta bebe kwa Watoto wa shule za msingi wakati wa kampeni kabla ya kuingia madarakani-lakini ahadi hizo hazijawahi kutekelezwa.
Raila ameahidi mabilioni ya pesa kwa tabaka la chini kabisa la jamii huku akitaka kumgeuzia macho Ruto ambaye kwa muda mrefu amekuwa akijionyesha kuwa mwokozi wa masikini nchini.
Huku Ruto pia akiahidi kutenga Shilingi 100 milioni kwa kila eneo bunge kati ya 290 kusaidia biashara ndogo na za kati ili kuchochea ukuaji na kubuni nafasi za kazi, Raila anataka kutoa pesa taslimu kwa familia zilizo fukara .
Raila pia amewaahidi vijana angalau nafasi nne za baraza la mawaziri kama sehemu ya ahadi zake za 2022.
Kiongozi huyo wa ODM anasema atatoa Shilingi 6,000 kwa familia maskini, ikiwa atachaguliwa kuwa rais mwaka huu , akisema mara tu atakapoziba mianya yote ya ufisadi ambayo hupora Shilingi 2 bilioni kila siku, kutakuwa na rasilimali za kutosha kufadhili mpango huo.
Kwa mara ya kwanza, kipute cha kuwania urais nchini Kenya kinaonekana kufika hadi kwenye mijadala ya mustakabali wa uchumi, huku Raila na Ruto wakijitokeza kunadi mikakati yao kukwamua uchumi .
Ruto amejitangaza kama mfuasi wa Kibaki kiuchumi na kwamba anafahamu vyema matatizo yanayosumbua kila eneo.
Ili kueneza mtindo wake wa uchumi wa chini kwenda juu(Bottom-Up) Ruto amekuwa akifanya mijadala ya kiuchumi kuwaruhusu Wakenya wa kawaida kutaja vipaumbele vyao ambavyo vitatoa mwongozo wa sera zake .
Kwa kuzingatia idadi kubwa ya wapiga kura ni vijana, ameanzisha mpango unaolenga wajasiriamali wadogo na kuwapa michango ili kuboresha maisha yao na kuwalinda dhidi ya athari za janga la Covid-19.
Miongoni mwa ahadi alizotoa Ruto kwa wapiga kura ni kutenga Shilingi bilioni 100 ili kuunda ajira kwa vijana ikiwa atachaguliwa kuwa Rais.
Viongozi hao wawili pia wameonekana kuzitumia ahadi hizo kuyalenga maalum maalum ya wapiga kura huku vijana na wanawake wakionekana kama walengwa wakuu .
Vijana walio na idadi kubwa ya kura na yaonekana katika uchaguzi huu wengi wamejitosa mbioni kuwania viti mbali mbali .
Kampeni zinapoendelea itabainika wazi kila mrengo una yapi kwa makundi hayo na hasa wanawake ambao bado uakilishi wao ni adimu sana licha ya kuwepo sheria inayotaka pawepo usawa wa kijinsia katika uakilishi wa nafasi za uongozi .














