Mambo 7 unayopaswa kujua kabla ya kununua gari

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Kumiliki gari ni ndoto kwa wengi, lakini katika nchi nyingi kufanikisha ndoto hiyo huja kwa gharama kubwa.

Katika hali kama hiyo, swala la kununua gari mpya kabisa au kununua gari lililotumika linawagusa wengi.

Kupata gari linalofaa na la ubora wa juu sokoni wakati mwingine kunaweza kuwa changamoto.

Huu ni mwongozo rahisi unaokuelezea wewe, msomaji, jinsi ya kuchagua gari sahihi.

Kwa hili, BBC Sinhala ilishiriki katika mazungumzo na Mhandisi wa Teknolojia ya Magari Jagath Jayasinghe, mshauri wa nje wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uanafunzi na Mafunzo ya Kiufundi, ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 35 katika tasnia ya magari.

Pia unaweza kusoma

1. Kuchagua gari linaloendana na mahitaji yako

Kabla ya kununua gari, unapaswa kuwa mwangalifu zaidi kuhusu mahitaji yako. Itakufanya ustarehe zaidi bali pia kupunguza upotevu wa pesa.

Je, una familia ndogo? Familia kubwa? Je, unatafuta kununua gari kwa matumizi ya kibinafsi? Kwa madhumuni ya biashara? Kwa hivyo, ni gari gani linalokufaa? Je, una mpango wa kuitumia kwa muda mfupi kisha kununua gari lingine? Au una mpango wa kulitumia kwa muda mrefu? Je unahitaji gari kweli? Unapaswa kufikiria juu ya mambo haya yote ipasavyo.

Mhandisi wa teknolojia ya magari Jagath Jayasinghe, akizungumza na BBC Sinhala, alisema kuwa haiwezekani kwa watu wengi kumiliki magari kadhaa ili kukidhi mahitaji yao binafsi.

Kwa hiyo, alisema, ni sahihi zaidi kuchagua gari ambalo linaweza kukidhi angalau baadhi ya mahitaji yako.

"Kwa mfano, baadhi ya watu hununua gari lenye injini kubw na kulitumia kusafiri hadi ofisini na kwenye vitongoji. Haifai. Kwasababu injini hiyo inapokimbia inamaliza mafuta kwa urahisi."

"Halafu mtu ambaye hajawahi kwenda nje ya mji ananunua gari la nje ya mji - 4 wheel drive kuzunguka mji. Huo pia ni upotevu kamili wa pesa. Lakini ikiwa ni mtu ambaye huenda vitongojini mara kwa mara, kumaanisha kwamba anatoka nje ya mji, basi aina hiyo ya gari ni sawa kwake."

"Ikiwa mtu anasafiri umbali mrefu mara kwa mara na ana pesa, na anaendesha gari dogo kama hatchback, haitatoshi."

2. Pesa

Kabla ya kununua gari, unapaswa kuzingatia kwa makini ni kiasi gani unaweza kumudu kutumia.

Kulingana na hali ya kisheria nchini Sri Lanka, kuna taasisi mbalimbali kama vile benki ambazo hutoa vifaa vya kifedha kwa kusudi hili.

Unapaswa kuhakikisha kuwa unachukua tu mkopo unaofaa kwa mapato yako. Vyanzo vyako vya mapato ni vipi? Je, una chanzo thabiti cha mapato? Unapaswa kuzingatia kwa uangalifu ikiwa unanunua gari kwa pesa taslimu.

Lakini kuna jambo lingine muhimu ambalo unahitaji kulipa kipaumbele.

"Mtu akinunua gari - tuseme ambalo halijasajiliwa, jipya kabisa au lolote. Ikiwa halijasajiliwa,hatahitaji kulipia ukarabati kwa muda. Tunachopaswa kufanya ni kupata gari hilo na kulijaza mafuta tu," kulingana na mhandisi wa teknolojia ya magari Jagath Jayasinghe.

3. Kulikagua

Mhandisi wa teknolojia ya magari anasema kwamba ingawa sio muhimu kununua gari jipya, hali ya gari iliyotumiwa inapaswa kuangaliwa katika nyanja mbili kabla ya kuinunua.

Anasema kwanza ni hali ya kisheria.

"Jambo muhimu zaidi ni suala la kisheria. Hebu tuseme kuna baadhi ya masuala ya kisheria, au paa ambalo limeharibika, au kufanya kitu kinyume cha sheria, unaweza kuchukua nakala ya kitabu cha gari yani Logbook na kukichunguza kwa muda mfupi. Si lazima kwenda na gari lenyewe. Unapaswa kujua ni wamiliki wangapi wamesajiliwa? Unaweza kuangalia vitu hivi."

Pili, anasema kuwa hali ya kiufundi ya gari inapaswa kuangaliwa.

"Wakati wa ukaguzi wa mitambo, mhandisi mwenye uzoefu, fundi, au mthamini wa gari anaweza kuchunguza hali kimwili ya gari."

Hii hukuruhusu kuangalia vizuri ikiwa gari limekuwa katika ajali hapo awali na ikiwa limerekebishwa vizuri, na vile vile hali ya injini ya gari na ikiwa kuna kasoro zingine zozote.

4. Petroli? Dizeli? EV?

Magari ya umeme sasa yamekuwa mwenendo wa kimataifa. Lakini ni mahali gani pazuri pa kuchagua aina ya mafuta ya gari? Tuliangazie hilo pia.

"Watu wengi wanafikiri kwamba magari ya mwako wa ndani IC yanayotumia petroli/dizeli, hatimaye yataacha kutengenezwa. Lakini hilo halitafanyika, tunaweza kutumia injini za IC kwa muda mrefu," mhandisi wa teknolojia ya magari Jagath Jayasinghe aliambia BBC Sinhala.

"Lakini inabidi tutengeze magari ya umeme mahali ambapo hatuwezi kufikia viwango vya utoaji wa hewa chafu. Magari yanayotengenezwa duniani, na kutolewa kwa mujibu wa viwango vya utoaji wa hewa, kanuni hizo zinapokuwa kali, zitafikia hatua ya kuondoa injini za IC."

"Lakini katika nchi kama yetu, ukinunua gari, unanunua gari la familia. Ni gari moja ambalo hufanya kila kitu. Katika nchi zingine, kuna gari tofauti za familia, gari tofauti za biashara, gari tofauti za ofisi. Hatuna uwezo huo"

5. Manual au automatic?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Watu wengi pia huzingatia utendakazi wa gari wakati wa kulinunua. Wengine wanabishana juu ya ufanisi wa mafuta, wakati wengine wanabishana juu ya urahisi wa usafiri.

Pia tulimuuliza Mhandisi wa Teknolojia ya Magari wa BBC Sinhala Jagath Jayasinghe kuhusu hili.

Alisema kuwa kuchagua gari la manual au automatik kunaweza kufanywa kulingana na matakwa ya mnunuzi.

BBC Sinhala pia ilimuuliza ikiwa kuna tofauti katika ufanisi wa mafuta kati ya mifumo ya manual au automatic.

"Ilikuwa hivyo. Lakini hii leo, vifaa vingi vya ki-elektroniki vimeongezwa kwenye magari," mhandisi huyo wa teknolojia ya magari alielezea.

Alibainisha kuwa ufanisi wa mafuta ya gari la manual hutofautiana kulingana na nani anayeendesha.

"Katika kisanduku cha gia ya garri la automatic, hatuwezi kubadilisha gia tunavyotaka. kwasababu ndiyo inayokokotoa kasi ya gari, mzigo na kiasi cha kanyagio cha kuongeza kasi kinachotumika na kubadilisha gia."

"Kutokana na maendeleo hayo, magari ya manual yanatumia mafuta mengi kuliko yale ya automatic," alisema.

6. Usalama

Uchunguzi uliofanywa na BBC Sinhala umebaini kuwa wakati wa kuangalia ajali za barabarani zilizotokea katika kipindi cha miaka 5 iliyopita kuanzia 2020 hadi 2024, maisha hupotea kutokana na ajali mbaya za barabarani .

Mhandisi wa Teknolojia ya Magari Jagath Jayasinghe anasema kuwa wakati wa kununua gari, tahadhari pia inapaswa kuchukuliwa kwa usalama wake.

Hata hivyo, anasema kwamba kwa kuzingatia hali ya kiuchumi katika nchi, inaweza kuwa vigumu kwa mtu kununua gari lenye vipengele vya usalama vya hali ya juu.

"Usalama ukipotea inapotokea ajali, hatari ya maisha yetu kuwa hatarini ni kubwa. Lakini kwa kuzingatia uchumi wa nchi kama yetu hatuwezi kusema kwamba hii ni kawaida, ni tatizo ndani ya nchi na katika uchumi."

"Lakini maoni yangu binafsi ni kwamba ukichagua gari lenye angalau ABS (Anti-lock braking system) na Air Bags, unaweza kuzuia kifo kwenye ajali. Lakini magari ya bei nafuu hayana vitu hivyo," alifafanua.

7. Kutunza na kuliuza

Hatimaye, unapaswa kuwa na wazo fulani la gharama ya kutunza gari unalonunua.

Hali ni tofauti linapokuja suala la matengenezo ya magari ya umeme.

"Umeme ni gari ambalo hatuwezi kuzungumza juu ya gharama ya kudumisha. Kwa sababu hatuna huduma nyingi za kufanya juu yake. Hiyo ni hadithi tofauti," alisema mhandisi wa teknolojia ya magari Jagath Jayasinghe.

Hata hivyo, alidokeza kuwa inapokuja suala la magari ya petroli au dizeli, matengenezo ni ya kawaida.

"Nchini Sri Lanka, mafuta hubadilishwa kila kilomita 5,000. Lakini hakuna mahali popote duniani ambapo mafuta hubadilishwa namna hiyo. Unaweza kukimbia kwa angalau kilomita 7,000 na mafuta yoyote yanayopatikana Sri Lanka."

Alitaja gari linapaswa "kuhudumiwa" kila baada ya miezi 6 au 8.