Kwa nini kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kunakuwa rahisi zaidi na hatari zaidi

Sogeza ili kuendelea

Kuenea kwa magonjwa ya wanyama kwenda kwa wanadamu

Katika miaka mitatu iliyopita, Afrika imeona kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa milipuko ya zoonoses –magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na kuambukizwa kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu. Wataalamu wa afya wanaonya kwamba ueneaji wa magonjwa hayo, mifumo dhaifu ya afya na changamoto za kiuchumi na kijamii vinafanya bara hilo kuwa hatarini sana kwa janga jingine la kiafya.

Kuenea kwa magonjwa ya wanyama kwenda kwa wanadamu

Mlipuko ulioenea zaidi umekuwa mpox, ambao umeathiri takriban nchi 32 za Afrika, na kuwahusisha karibu watu 55,000 tangu Januari 2022 hadi Septemba 2025, kulingana na Shirika la Afya duniani (WHO). Takriban maisha 2,000 yamepotea, data inaonyesha kutoka Africa Centres for Disease Control and Prevention (Africa CDC)

Kuenea kwa magonjwa ya wanyama kwenda kwa wanadamu

Kutokana na kuongezeka kwa visa katika nchi nyingi za Afrika, WHO ilitangaza mpox kuwa dharura ya afya ya umma ya umuhimu wa kimataifa mwezi Agosti 2024. Hii ilikuwa mara ya pili tangazo kama hilo kuhusu mpox ndani ya miaka miwili.

Kuenea kwa magonjwa ya wanyama kwenda kwa wanadamu

Ingawa WHO mwezi Mei ilitangaza kwamba mlipuko wa mpox Afrika hauna tena hadhi ya dharura baada ya visa vyake kupungua , zaidi ya nchi kumi na mbili barani humo bado zinafanya kazi ya kukabiliana na ugonjwa huo, huku visa vikiwa vinaongezeka nchini Ghana, Liberia na Uganda.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliweza kukabiliana na mlipuko wake wa 16 wa ugonjwa wa Ebola katika miongo mitano iliyopita kuanzia Septemba hadi Novemba mwaka huu, huku Uganda ikiendelea kuwa makini kufuatia mlipuko wa Ebola wa miezi mitatu uliomalizika Aprili, mlipuko wake wa nane ndani ya miaka 25.

Katika Afrika Magharibi, Senegal inakabiliwa na mlipuko wa Ugonjwa wa Rift Valley Fever (RVF) pamoja na kuongezeka kwa visa vya mpox, ambapo vifo 11 vimeorodheshwa katika wiki mbili baada ya kugunduliwa kwa kesi hizo

Wakati huo huo, Rwanda na Tanzania zilitangaza kumalizika kwa milipuko ya ugonjwa wa Marburg baada ya juhudi kubwa za kukabiliana na ugonjwa huo mwaka 2024, huku Ethiopia ikithibitisha mlipuko wake wa kwanza wa ugonjwa huu mwaka huu.

Milipuko hii ya mara kwa mara inathibitisha onyo la wataalamu wa afya kwamba magonjwa ya zoonotic yanaongezeka kwa ukubwa, mara kwa mara kutoka katika maeneo ambayo kwa kawaida hutokea magonjwa ya mlipuko hadi maeneo mapya. Kwa mujibu wa Programu ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, hali hii imeongezeka kwa kasi tangu 1940

Kwa sasa magonjwa ya wanyama kwa binadamu yaambukiza takribani

1000000000

ya watu na magonjwa haya yanaua kila mwaka ,kwa mujibu wa WHO

1,000,000,000

Afrika imeathirika zaidi, ikiwa na ongezeko la asilimia 63 katika milipuko ya magonjwa yanayotokana na wanyama katika muongo uliopita, kama inavyoonyesha uchambuzi wa Shirika la Afya duniani(WHO).

Magonjwa ya zoonotic pia yanachangia takriban moja ya tatu ya kila milipuko wa magonjwa ya kuambukiza yaliyorekodiwa kwenye bara hili katika karne hii.

Tishio linaloongezeka limesukuma Africa CDC kuzindua mpango wa miaka minne mwezi Julai wa kuzuia na kudhibiti uenezaji wa magonjwa ya zoonotic kwenye bara.

Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC, Dk Jean Kaseya, anaonya kwamba Afrika iko karibu kukaribiana na janga lingine la kiafya kulingana na ushahidi.

Dk Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDCDk Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDCGetty Images


Barani Afrika, kile nilichokiona kutoka 2022 hadi 2024, hata sasa mwaka 2025, ni ongezeko kubwa la milipuko, aina mbalimbali za milipuko – Ebola, Marburg, mpox na mingine.”

Dk Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Africa CDC

Anasema kulikuwa na ongezeko la asilimia 41 ya milipuko ya magonjwa ya zoonotic katika miaka miwili iliyopita.

alt=""

Jinsi magonjwa makuu matano yanayotokana na wanyama yanavyoenea duniani

maambukizi

0

<100

<200

<300

<500

<999

1000 +

ChanzoWHO, US CDC, Africa CDC na wizara za afya katika mataifa mbalimbali

Magonjwa ya zoonotic huenea vipi kwa watu?

Maambukizi yanaweza kusambaa kwa binadamu kupitia mgongano wa moja kwa moja na vimelea au kupitia chakula, maji, hewa au mazingira yaliyochafuliwa.

Mfumo wa milipuko ya magonjwa yanayoenezwa na wanyama ni tofauti sana.

"Mpox, kwa mfano, ilisababisha maambukizi yasiyo ya kawaida kwa miongo kabla ya kuongezeka na kuwa mlipuko wa kimataifa. Kwa upande mwingine, COVID-19 ilitokea ghafla na kuenea kwa haraka kote duniani.

"Magonjwa mengine kama vile rabies, ugonjwa wa Chagas, homa ya Lassa, na salmonellosis huambukiza na kuua maelfu kila mwaka katika maeneo yenye milipuko ya kawaida.

"HIV ilianza kama magonjwa ya wanyama kwa binadamu lakini baadaye ikabadilika kuwa maambukizi yanayowaathiri watu tu

Homa ya Rift Valley ilienea kutoka kwa wanyama kwenda kwa watu, lakini haijaenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, wakati milipuko ya Marburg mara nyingi huanzia kutoka kwa wanyama kwenda kwa watu.

Kwa mfano, Waziri wa Afya wa Rwanda, Dk. Sabin Nsanzimana, alisema kwamba mgonjwa wa kwanza katika mlipuko wa Marburg nchini humo mwaka 2024 alipata virusi kutoka kwenye pango lililokuwa na popo."

Kwanini magonjwa haya yamekuwa mengi?

"Homa ya Rift Valley ilienea kutoka kwa wanyama kwenda kwa watu, lakini haijaenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, wakati milipuko ya Marburg mara nyingi huanza kutokana na kuenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa watu."

Kuingia kwa binadamu katika mfumo wa ikolojia wa wanyamapori na biashara ya wanyamapori huongeza uwezekano wa binadamu kuathirika na viini vya magonjwa yanayotokana na wanyama, wanasema Dkt. Krutika Kuppalli, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Texas Southwestern Medical Center, na Dkt. Peninah Munyua, mkuu wa idara ya epidemiology na ufuatiliaji katika Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Kenya.

Dkt. Krutika Kuppalli, Kituo cha Tiba cha UT SouthwesternDkt. Krutika Kuppalli, Kituo cha Tiba cha UT SouthwesternUT Southwestern Medical Center


Virusi vingi vinaweza kuambukizwa kupitia matone ya pumzi, kugusana na vimiminika vya mwili au wadudu wanaobeba magonjwa, jambo linalorahisisha uambukizi wa haraka.

Dkt. Krutika Kuppalli, Kituo cha Tiba cha UT Southwestern

Wataalamu wanasema kuwa mifumo iliyoboreshwa ya ufuatiliaji wa kiafya imewezesha utambuzi bora na kuripoti kwa wakati wa mlipuko wa magonjwa.

Maeneo hatarishi ya tishio la magonjwa yatokanayo na wanyama ni yapi?

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo kwa sasa inapambana na mlipuko wa Ebola na imerekodi idadi kubwa zaidi ya vifo katika mlipuko unaoendelea wa mpox,na Brazil, zimeathirika kwa kiwango kikubwa na magonjwa yatokanayo na wanyama.

DRC ina mzigo mkubwa wa magonjwa mengine mengi ya zoonotic yanayoendelea kuwepo nchini humo, yakiwemo kichaa cha mbwa (rabies) na trypanosomiasis ya binadamu barani Afrika, inayojulikana zaidi kama ugonjwa wa usingizi.

Vivyo hivyo, Brazil inaathiriwa na magonjwa ya zoonotic yanayoendelea kuwepo kama vile homa ya manjano, chikungunya, homa ya dengue na virusi vya Zika.

Nchi hizo mbili pamoja na nyingine zilizopo katika Bonde la Kongo, Amerika ya Kusini na Asia ya Kusini-Mashariki ni maeneo hatarishi makubwa ya magonjwa yatokanayo na wanyama

alt=""

Idadi ya walioambukizwa na vifo vya magonjwa makuu matano yanayotokana na wanyama kwa muda

maambukizi

0

<100

<200

<300

<500

<999

1000 +

ChanzoWHO, US CDC, Africa CDC na wizara za afya katika mataifa mbalimbali

Ulaji wa nyama pori huongeza hatari ya maambukizi ya magonjwa yatokanayo na wanyama katika maeneo hatarishi, anasema Dkt. Munyua.

Afrika ya Kati pekee,
kilo bilioni moja
za nyama ya pori huliwa kila mwaka.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Brazil pia zinakumbwa na magonjwa zaidi yanayotokana na wanyama kutokana na misitu yao mikubwa, Misitu ya mvua ya Kongo na Amazon.

Misitu ni makazi ya wanyama wadogo wanaobeba na kusambaza maambukizi, anasema Dkt. Kuppalli.

Anasema pia kwamba madhara ya magonjwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yanazidiwa na changamoto za kijamii na kiuchumi kama umasikini, upungufu wa huduma za afya, na migogoro, ambayo huruhusu magonjwa kuenea haraka katika idadi kubwa ya watu walioko kwenye makazi ya msongamano.

Kwa nini virusi husababisha milipuko mikubwa zaidi ya magonjwa yanayotokana na wanyama?

Virusi huwa na mwenendo wa kusababisha milipuko mikubwa kutokana na njia zao za uenezi zinazofaa, zinazowawezesha kuenea haraka na kuzidi uwezo wa mifumo ya afya mara tu wanapovuka kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Dkt. Kuppalli anasema kuwa virusi hubadilika kwa haraka, jambo linalowawezesha kuzoea wenyeji wapya na kuepuka mfumo wa kinga wa mwili. Virusi waliobadilika, kama vile aina ya mpox ya Clade 1b, huwa na uwezo mkubwa wa kuambukiza na kuwa hatari zaidi.

Milipuko ya virusi yanayotokana na wanyama ni vigumu kutabirika kwanini mara nyingi hubebwa na wanyamapori ambao kwa kawaida hawana dalili za ugonjwa.

Ni wenyeji na waenezi gani wa magonjwa yanayotokana na wanyama ambao ni wa kawaida zaidi?

Aina mbili za wanyama zinahusishwa katika kuenea kwa magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

"Wanyama wanaosababisha wanaojulikana pia kwa kubeba vimelea vya magonjwa. Huvisambaza kwa binadamu na wanyama wengine."

Dkt. Munyua anasema wanyama wanaosababisha kama popo, ngamia,panya na ndege wanatuletea changamoto.

Dkt. Peninah Munyua, tawi la CDC ya Marekani nchini KenyaDkt. Peninah Munyua, tawi la CDC ya Marekani nchini KenyaChanzo cha picha: BBC/Peter Njoroge


Popo wapo kila mahali na hubeba aina nyingi za virusi vilivyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni, ikiwemo virusi vya Ebola na Marburg.

Dkt. Peninah Munyua, tawi la CDC ya Marekani nchini Kenya

Anamuongeza ngamia, kuwa msambazaji mkuu wa virusi vya corona na kuleta wasiwasi barani Afrika kwani takribani sehemu mbili ya tatu ya idadi ya ngamia duniani wanatoka barani humo.

Panya na ndege, ambao wote wanasababisha na wasambazaji, wapo katika mazingira mbalimbali na ni vigumu kufuatilia magonjwa yanayowahusu.

Katika Afrika Magharibi, panya ni wenyeji na waenezaji wa homa ya Lassa, ambayo husababisha takriban mtu mmoja kati ya sita kulazwa hospitalini kila mwaka nchini Sierra Leone na Liberia.

Ni magonjwa gani yanayotokana na wanyama wanaosababisha na wanaoeneza, ndio wanaofiwa zaidi na wanasayansi?

Ripoti ya WHO ya mwaka 2024 ilibainisha takriban vimelea 30 vyenye uwezekano wa kusababisha milipuko mikubwa na majanga ya magonjwa duniani, vingi vikiwa ni magonjwa yatokanayo na wanyama (zoonotic).

Yanajumuisha mpox, virusi vya dengue, virusi vya influenza A, virusi vya mpox na virusi vya corona vinavyojulikana kama Sarbecovirus, ambavyo vinajumuisha SARS-CoV-2, virusi vilivyosababisha janga la kimataifa la COVID-19.

Nini chanzo cha kupunguza kuenea kwa magonjwa yatokanayo na wanyama (zoonotic)?

Dkt. Munyua na Dkt. Kuppalli wanasema kuwa kuratibu juhudi za kukabiliana na milipuko ya magonjwa na kuboresha mifumo ya utambuzi wa mapema ni mambo muhimu katika kudhibiti milipuko ya baadaye, wakitaja namna Rwanda ilivyoshughulikia mlipuko wa ugonjwa wa Marburg kama mfano bora.

“Nchi ilitekeleza kwa haraka ufuatiliaji na upimaji, na kuanza majaribio ya kitabibu ya (randomised control trial) kwa ajili ya tiba,” anasema Dkt. Kuppalli.

Wataalamu wanasema kuwa kuendelea kuendeleza vifaa vya uchunguzi wa magonjwa, chanjo na tiba barani Afrika pia ni hatua muhimu katika kudhibiti magonjwa yatokanayo na wanyama (zoonotic)