Virusi vya Marburg ni nini?

Microscope image of Marburg virus

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko unaoshukiwa kuwa wa virusi vya ugonjwa wa Marburg umewaua watu wanane katika mkoa wa Kagera Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Taarifa ya shirika hilo iliyochapishwa mtandaoni inasema kuwa mnamo tarehe 10 Januari 2025 ''WHO ilipokea ripoti za kuaminika kutoka kwa vyanzo vya ndani kuhusu visa vinavyoshukiwa vya ugonjwa huo katika mkoa wa Kagera, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kikohozi, maumivu ya viungo, kuhara na kutapika, na mara nyingi hata upungufu wa damu katika mwili.

Ugonjwa wa Marburg ni nini?

Kulingana na Umoja wa Mataifa, virusi vya Marburg, ambavyo ni sawa na virusi hatari vya Ebola, viligunduliwa kwa mara ya kwanza baada ya watu 31 kuambukizwa, saba kati yao walikufa, mnamo 1967 huko Marburg na Frankfurt. Ujerumani na Belgrade huko Serbia.

 Virusi vya Marburg vilipatikana kwa mara ya kwanza kwa tumbili wa kijani kibichi wa Kiafrika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Virusi vya Marburg vilipatikana kwa mara ya kwanza kwa tumbili wa kijani kibichi wa Kiafrika

Mlipuko huo ulitokana na tumbili wa Kiafrika walioagizwa kutoka Uganda. Lakini virusi hivyo vimehusishwa na wanyama wengine tangu wakati huo.

Na miongoni mwa wanadamu, huenezwa zaidi na watu ambao wamekaa kwa muda mrefu katika mapango na migodi iliyo na popo.

Huu ni mlipuko wa kwanza nchini Ghana - lakini nchi kadhaa za Afrikazimewahi kuripoti mlipiko wa virusi ikiwa ni pamoja:

  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
  • Kenya
  • Afrika Kusini
  • Uganda
  • Zimbabwe

Mlipuko wa mwaka 2005 nchini Angola ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 300. Lakini barani Ulaya, ni mtu mmoja tu amefariki katika kipindi cha miaka 40 - na mmoja nchini Marekani,baada ya kurejea kutoka katika safari ya kuzuru mapango nchini Uganda.

Milipuko mikubwa:

  • 2017, Uganda: visa vitatu, watu watatu walifariki
  • 2012, Uganda: vis 15, watu wanne walifariki
  • 2005, Angola: visa 374, watu 329 walifariki
  • 1998-2000, DR Congo: visa 154 cases, watu 128 walifariki
  • 1967, Ujerumani: visa 29, watu saba walifariki

Chanzo: WHO

Inasababisha ugonjwa gani?

Unaanza ghafla na:

  • Homa
  • kuumwa vibaya na kichwa
  • kuumwa na misuli

Hii mara nyingi siku tatu hufuatwa na:

  • kuharisha
  • kuumwa na tumbo
  • kichefuchefu
  • kutapika

WHO inasema: "Mwonekano wa wagonjwa katika awamu hii umeelezewa kuwa unaonyesha sifa za 'kama mzimu', macho ya ndani, nyuso zisizo na hisia na uchovu mwingi."

Baadhi ya watu hutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili na kufa siku nane hadi tisa baada ya kuugua kwa sababu ya kupoteza damu nyingi na mshtuko.

Kwa wastani, virusi huua nusu ya walioambukizwa, WHO inasema, lakini aina hatari zaidi imeua hadi 88%.

Popo wa matunda wa rousette wa Misri ndiye mbebaji mkuu wa virusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Popo wa matunda wa rousette wa Misri ndiye mbebaji mkuu wa virusi

Je, inaeneaje?

Popo wa matunda aina ya rousette wa Misri mara nyingi huwa na virusi. Nyani wa kijani kibichi na nguruwe wanaweza pia kubeba.

Miongoni mwa wanadamu, huenea kupitia maji ya mwili na malazi yaliyochafuliwa nao.

Na hata watu wakipona, damu au shahawa zao, kwa mfano, zinaweza kuwaambukiza wengine kwa miezi mingi baadaye.

Je, inaweza kutibiwaje?

Hakuna chanjo maalum au matibabu ya virusi.

Lakini aina mbalimbali za bidhaa za damu, madawa ya kulevya na matibabu ya kinga yanatengenezwa, WHO inasema.

Na madaktari wanaweza kupunguza dalili kwa kuwapa wagonjwa waliofika hospitali maji mengi ili kuchukua nafasi ya damu iliyopotea.

Vinawezaje kudhibitiwa?

Watu barani Afrika wanapaswa kuepuka kula au kushika nyama ya porini, Gavi, shirika la kimataifa linalokuza upatikanaji wa chanjo, linasema.

Watu pia wanapaswa kuepuka kuwa karibu na nguruwe katika maeneo yenye mlipuko, WHO inasema.

Wanaume ambao wamekuwa na virusi wanapaswa kutumia kondomu kwa mwaka mmoja baada ya kupata alili au hadi shahawa zao zitakapothibitishwa mara mbili kuwa hazina virusi.

Na wale wanaozika watu ambao wamekufa kutokana na virusi wanapaswa kuepuka kugusa mwili.