Moja kwa moja, Sitairuhusu Iran kuwa na silaha za nyuklia – Trump
Rais wa Marekani amesema: "Kwa miongo kadhaa, imekuwa sera ya Marekani kutoruhusu Iran kupata silaha za nyuklia.”
Moja kwa moja
Rashid Abdallah
Sitairuhusu Iran kuwa na silaha za nyuklia – Trump
Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa
Marekani Donald Trump ametoa hotuba yake ya kila mwaka katika majengo ya Bunge
la Marekani na kusisitiza kuwa hatoiruhusu Iran kuwa na silaha za nyuklia.
Rais wa
Marekani amesema: "Kwa miongo kadhaa, imekuwa sera ya Marekani kutoruhusu
Iran kupata silaha za nyuklia.”
“Wameonywa
wasijaribu kujenga upya mpango wao wa silaha, lakini wanaendelea kufuata
matarajio yao mabaya ya nyuklia. Napenda tutatue tatizo hili kupitia
diplomasia, lakini jambo moja ni hakika: Sitawaruhusu kupata silaha za
nyuklia."
Trump
ameweka rekodi ya hotuba ndefu zaidi, akitumia karibu saa 1 na dakika 50,
akiizidi rekodi ya Bill Clinton ya hotuba yake ya mwisho mnamo 2000.
'Iwapo Marekani itafanya makosa ya kutushambulia itapata hasara kubwa' - Mkuu wa Jeshi Iran
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mkuu wa Jeshi la Iran Jenerali Mousavi
Hapo awali tuliripoti kwamba Waziri wa Ulinzi wa Armenia Soren Papikyan alisafiri hadi Tehran na kukutana na Waziri wa Ulinzi wa Irani Aziz Nasirzadeh.
Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, Mkuu wa Jeshi la Iran pia alikutana naye.
Bwana Mousavi alisema katika mkutano huo: "Sisi hatukuwa waanzilishi wa vita vyovyote, na mbinu yetu huko nyuma ilikuwa kuzuia kupanuka kwa wigo wa vita na kupunguza majeruha. Lakini hatua za Marekani zilitufanya kubadili mtazamo wetu, na wakati huu, ikiwa itafanya makosa, tutaisababishia hasara kubwa."
Msemaji wa Ikulu ya White House Carolyn Leavitt amesema leo kuwa chaguo la kwanza la Donald Trump siku zote ni diplomasia, lakini yuko tayari kutumia nguvu ikibidi.
Nigeria yakana ripoti kwamba ililipa fidia ili wanafunzi waliotekwa nyara waachiliwe huru
Chanzo cha picha, EPA/Shutterstock
Maelezo ya picha, Zaidi ya wanafunzi 200 na wafanyakazi walichukuliwa na watu wenye silaha kutoka Shule ya St Mary's mwezi Novemba - wote waliachiliwa huru kufikia Krismasi
Serikali ya
Nigeria imekataa ripoti ya vyombo vya habari inayodai kwamba ililipa fidia kwa wanamgambo
wa Kiislamu wa Boko Haram ili kuachiliwa huru kwa zaidi ya wanafunzi 200 na
wafanyakazi waliotekwa nyara katika shule ya bweni ya Kikatoliki mwezi Novemba.
Waziri wa
Habari Mohammed Idris amesema madai hayo, yaliyotolewa na shirika la habari la
AFP akinukuu vyanzo vya kijasusi, kuwa "ya uwongo na yasiyo na msingi."
Pia amekanusha
kwamba makamanda wawili wa Boko Haram waliachiliwa huru kama sehemu ya
makubaliano hayo.
Nigeria inakabiliwa
na tatizo la utekaji nyara - huku wahalifu wakiwa ni pamoja na wanamgambo wa
Kiislamu, wanachama wa magenge yanayojulikana kama "majambazi" na
watu wanaotaka kujitenga.
Baadhi ya
wachambuzi walionukuliwa na AFP wanaamini utekaji nyara katika Shule ya St Mary
huko Papiri katika jimbo la magharibi mwa Niger uliongozwa na kamanda maarufu
wa wanamgambo wa Boko Haram anayejulikana kama "Sadiku."
Ingawa Boko
Haram inasalia kuwa na shughuli nyingi zaidi katika jimbo la Borno
kaskazini-mashariki, ambapo kundi hilo lilianza uasi wake mwaka 2009, mitandao
mingine ya uhalifu ina shughuli katika sehemu kubwa za maeneo ya
kaskazini-magharibi na kaskazini-kati mwa Nigeria.
Chanzo
kimoja kilichonukuliwa na AFP kilidai fidia hiyo ilifikia takriban naira
milioni 40 (karibu dola 30,000, pauni 22,000) kwa kila mateka, huku chanzo
kingine kikidokeza kwamba jumla ya naira bilioni 2 (karibu dola milioni 1.5)
zililipwa.
Ripoti hiyo
pia ilidai pesa hizo zilisafirishwa kwa ndege hadi kwenye eneo la Gwoza la Boko
Haram katika jimbo la Borno na kukabidhiwa kwa kamanda wa eneo hilo.
"Madai
kwamba fidia ilitolewa kwa helikopta kwa waasi, pamoja na uthibitisho wa risiti
kuvuka mpaka, ni hadithi ya kubuni," Idris alisema katika taarifa hiyo.
Boko Haram
walipata umaarufu mwaka wa 2014 kwa kuwateka nyara zaidi ya wasichana 200 wa
shule kutoka kijiji cha Chibok.
Tangu wakati
huo nchi imekabiliwa na ongezeko la utekaji nyara kwa wingi, huku wachambuzi
wakisema kwamba malipo ya fidia - kutoka kwa familia, wapatanishi au, katika
baadhi ya matukio, mamlaka za serikali - yamesaidia kuchochea kile ambacho
baadhi hukielezea kama "sekta ya utekaji nyara kwa faida".
Mexico yawasaka wafungwa 23 waliotoroka gerezani wakati wa vurugu
Chanzo cha picha, EPA
Polisi
nchini Mexico inawasaka wafungwa kadhaa waliotoka gerezani huko Puerto Vallarta
wakati wa wimbi la machafuko yaliyoanzishwa na genge la dawa za kulevya la Jalisco New Generation
Cartel (CJNG) siku ya Jumapili.
CJGN ilifanya
vurugu kulipiza kisasi kwa mauaji ya kiongozi wao, Nemesio Oseguera Cervantes,
anayejulikana kama "El Mencho" na vikosi vya usalama.
Wakati wa
machafuko hayo, watu wenye silaha waligonga milango ya gereza kwa gari, na kuwafungulia
njia wafungwa 23 kutoroka, amesema afisa mmoja.
Zaidi ya
watu 70 - wakiwemo wanajeshi 25 - waliuawa katika operesheni ya kukamata El
Mencho na vurugu zilizofuata.