El Chapo Guzmán: "Katika miaka 6 sijaona jua"

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, El Chapo Guzman

Joaquín "El Chapo" Guzmán, ambaye alikuwa mmoja wa walanguzi wa dawa za kulevya waliokuwa wakisakwa zaidi duniani, amewasilisha ombi lakutaka usaidizi kwa kwa rais wa Mexico.

Mmoja wa mawakili wa "El Chapo", José Refugio Rodríguez, alieleza kuwa mteja wake alimweleza kuhusu hali anayoishi katika gereza la usalama wa juu la ADX Florence katika jimbo la Colorado, magharibi mwa Marekani

Na amemuagiza kukutana na rais wa Mexico ili uwezekano wa kurejea katika gereza la Mexico uangaliwe upya.

"Hali yake ni ya mateso ya kisaikolojia, kwa sababu ametengwa katika seli yake," Rodríguez alielezea kituo cha redio cha Mexico Radio Fórmula.

"Na anaumia kwa kosa hili, ukiukaji huu wa haki zake za kibinadamu (...) Ananiuliza nipiganie kurejea kwake Mexico."

Kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico, Marcelo Ebrard, hakuna uwezekano kwamba Guzmán atarejeshwa nyumbani akiwa anatumikia kifungo nchini Marekani.

Lakini López Obrador alisema kwamba ombi hilo lazima lichambuliwe: "Inapokuja kuhusa haki za binadamu, kuna njia na kuna matukio ya kimataifa. Kwa hivyo, haipaswi kutengwa. Kwa sababu haki kuu ya binadamu ni haki ya kuishi, basi kwa mtu yeyote wanapaswa kuhakikishiwa haki hiyo," rais wa Mexico alisema Jumatano.

"Hakuna kitu zaidi cha kuona ikiwa inaendelea au la."

.

Chanzo cha picha, Serikali ya Mexico

Maelezo ya picha, Rais Lopez Obrador

Guzmán alihukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Marekani kwa makosa ya dawa za kulevya.

"El Chapo" alikuwa kiongozi wa Sinaloa Cartel, moja ya mashirika yenye vurugu zaidi nchini Mexico ambayo makumi ya maelfu ya mauaji yanahusishwa nalo nchini humo katika miongo miwili iliyopita.

"Katika miaka 6 sijaona jua"

Wakili Rodríguez, mwakilishi wa Guzmán nchini Mexico na ambaye si sehemu ya watetezi wa dawa za kulevya nchini Marekani, alieleza kuwa alipokea ushuhuda wa mteja wake mwishoni mwa mwaka jana.

"Ananiambia kuwa katika miaka 6 aliyokaa Marekani hajaona jua," alieleza katika mahojiano na Radio Formula.

"Kuanzia Aprili hadi sasa [Novemba 2022] wamenipeleka kwenye uwanja wa kuchezea ambao una upana wa mita 2 na urefu wa 2.5m, mara moja kwa wiki. Kiwango cha juu ni mara tatu kwa wiki kwa saa mbili. Lakini jua halipigi" Guzmán alimwambia .

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gereza la Adamax Florence

Rodríguez pia alisema kuwa mteja wake alimhakikishia kuwa "alikuwa mgonjwa wa meno na badala ya kuyaponya, yaliondolewa ili asisumbue."

Wamemruhusu tu kupiga simu sita, kuwasiliana na wakili wake, binti zake, dada yake na mama yake. Na wamemruhusu wageni watatu tu.

Pia analalamika kwamba "chakula ni cha ubora wa kutisha" na kwamba haruhusiwi kuwasiliana na wafungwa wengine au kuzungumza kwa Kihispania, lugha pekee anayoijua.

"Ana televisheni, lakini kwa vile hazungumzi Kiingereza, anasema ana ufikiaji wa chaneli mbili tu kwa Kihispania," anaelezea Rodríguez.

Ombi la Kurudi Mexico

Maagizo ambayo Guzmán alimpa wakili wake ni kutafuta mahojiano na Rais López Obrador ili kumwomba apitie masharti ambayo alirejeshwa Marekani na uwezekano wa kutumikia kifungo chake nchini Mexico.

Rodríguez anasema kwamba alituma barua pepe kwa Ubalozi wa Mexico mjini Washington ili "serikali ya Mexico ijue hisia zake, ijue kwamba wamemtelekeza."

"Mimi naona ni SOS, ya mtu anayetembea baharini na kuona kipande cha mbao cha kushikilia. Kwa sababu ya kukata tamaa anayohisi huko Marekani na kwa sababu anaumia kutokana na kesi ambayo haikufanyika. ... Ingawa amehukumiwa, anaendelea kuwa na utu na haki za binadamu," Rodríguez alisema.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, El Chapo Guzman alitoroka jela za Mexico mara mbili
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ubalozi huo uliripoti Jumanne kwamba ulipokea barua pepe hiyo Januari 10: "Hakuna barua iliyopokelewa kutoka kwa Bw. Loera. Barua pepe hiyo ilitumwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje, kwa kuwa ni suala lililo ndani ya uwezo wake."

Alipoulizwa na waandishi wa habari, Waziri wa Mambo ya Nje Ebrard alisema kuwa ni vigumu sana kwa Guzmán kukubaliwa ombi la kurejeshwa nyumbani, kwa kuwa lazima atumike kifungo chake nchini Marekani. Rais López Obrador alisema kwamba jibu lazima lijadiliwe.

Kwa wakili Rodríguez, serikali ya Rais Enrique Peña Nieto (2012-2018) ilikiuka haki za utetezi za mteja wake kwa kumrejesha Marekani kwa njia ya haraka, akifanya "ukiukaji wa haki zake za kibinadamu."

"Kisheria, mkataba [wa kurejeshwa kati ya Mexico na Marekani] unaturuhusu kurejea, kwa sababu huko Mexico ana kesi za jinai zinazosubiri," anasema Rodríguez.

Hatari ya uwepo wa "El Chapo" katika magereza ya Mexico ilidhihirika baada ya kufanikiwa kutoroka mara mbili (2001 na 2014) kutoka kwa magereza yenye ulinzi mkali.