Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Chelsea iko tayari kumuuza Fernandez

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea imeiambia Real Madrid kuwa iko tayari kumtoa kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez mwenye umri wa miaka 25 mwaka huu. (Team talk)
Manchester United iko tayari kuchuana na Napoli na Atletico Madrid kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Wolves na Ureno Joao Gomes, 24. (Caught offside)
Viungo wawili wa England - Elliot Anderson wa Nottingham Forest, 23, na Adam Wharton wa Crystal Palace, 21 - pia wako kwenye orodha ya wachezaji wanaolengwa na Manchester United msimu wa joto. (Football Insider)
Tottenham na Manchester United zimewasiliana na meneja wa zamani wa Barcelona Xavi Hernandez. (Fichajes - kwa Kihispania)
Nottingham Forest inajadiliana na klabu ya Napoli kuhusu mkataba wa mkopo wa Januari kwa mshambuliaji wa Italia Lorenzo Lucca, 25, ambaye anaweza kujiunga kwa mkataba wa kudumu msimu wa joto. (Fabrizio Romano)
Crystal Palace wamekataa ombi la awali la Juventus kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 28. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Barcelona wanamtazama mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta na mkufunzi wa Paris St-Germain Luis Enrique kama wagombea wanaoweza kuinoa klabu hiyo siku za usoni, lakini wanataka meneja wa sasa Hansi Flick abakie kwa muda mrefu iwezekanavyo. (Diario Sport - kwa Kihispania)
Klabu za Bournemouth na West Ham zinavutiwa na winga wa Real Betis Mhispania Pablo Garcia, 19, na ziko tayari kulipa ada ya pauni milioni 26 ya kifungu chake cha kununuliwa. (Fichajes - kwa Kihispania)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton na Fulham zinaongoza mbio za kumsajili winga wa Wolfsburg wa Austria Patrick Wimmer, 24. (Rudy Galetti)
Leeds inafanya mazungumzo na Werder Bremen kuhusu mkataba wa £13m kumsajili kiungo wa kati wa Austria mwenye umri wa miaka 25 Romano Schmid. (Fabrizio Romano)
Chelsea na Manchester City zina nia ya kumsajili winga wa Leicester City mwenye umri wa miaka 16 Jeremy Monga. (Fichajes - kwa Kihispania)
Mshambuliaji wa Feyenoord Anis Hadj Moussa, 23, anafuatiliwa na Chelsea lakini Marseille na Benfica pia zinamnyatia mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria. (Florian Plettenberg)















