AFCON 2025: Nguvu ya makocha wa Afrika yaonekana

V

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Nani kati ya makocha hawa wa Afrika, Pape Thiaw (Senegal), Hossam Hassan (Misri), Walid Regragui (Morocco) au Eric Chelle (Nigeria) atatwaa ushindi Kombe la Mataifa ya Afrika 2025?

Baada ya kumalizika kwa robo fainali, kulikuwa na jambo moja la hakika; kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) litabaki mikononi mwa kocha kutoka bara hili.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa AFCON mwaka 1957, timu nne zilizofika nusu fainali, Senegal, Misri, Nigeria na Morocco, zote zinaongozwa na makocha raia wa Afrika.

Mmoja kati ya Pape Thiaw, Éric Chelle, Hossam Hassan na Walid Regragui, atakuwa bingwa wa Afrika tarehe Januari 18, 2026.

Tangu 2019, Kombe la Mataifa ya Afrika limekuwa na mabadiliko kwa makocha Waafrika. Djamel Belmadi aliiongoza Algeria kushinda mwaka 2019, Aliou Cissé aliipa Senegal taji lake la kwanza mwaka 2021, na Emerse Faé aliiongoza Ivory Coast kushinda mwaka 2023.

Zaidi ya hayo, AFCON ya 2025 inaashiria mabadiliko makubwa katika soka na uthibitisho kuwa soka la Afrika linazidi kuwa huru, na makocha wake sasa wana uwezo wa kushindana, si tu barani bali pia duniani kote.

Katika hatua ya makundi: kati ya timu 24 zilizoshiriki, 15 zilisimamiwa na makocha wa Kiafrika. Raundi ya 16: Makocha 11 ni kutoka Afrika kati ya timu 16 zilizofuzu.

Robo fainali: Makocha 6 ni kutoka Afrika kati ya 8, ni Mbelgiji Tom Saintfiet (Mali) na Mswisi Vladimir Petkovic (Algeria) pekee ndio ambao hawakuwa wazawa.

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika, timu zote nne zilizofika nusu fainali katika mashindano hayo zinaongozwa na makocha wa Kiafrika.

Hossam Hassan, Misri

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya ushindi wa Hugo Broos kwa Cameroon mwaka 2017 (kocha wa mwisho ambaye si Mwafrika kushinda taji), Kombe la Mataifa ya Afrika liliingia katika enzi mpya.

Miongoni mwa timu nne zilizofika nusu fainali, kocha mmoja wapo ni: Hossam Hassan. Kocha wa sasa wa Misri ni mmoja wa wachezaji wa kipekee wa Afrika.

Hadi sasa, ni makocha wawili tu wameshinda AFCON wakiwa wachezaji na kisha kama makocha: Mahmoud El-Gohary wa Misri na Stephen Keshi wa Nigeria.

Hossam Hassan, ambaye tayari ameshinda kombe hilo mara tatu kama mchezaji (1986, 1998, 2006), anaweza kujiunga nao katika historia hiyo.

Kocha wa Mafarao ndiye mfungaji bora katika historia ya timu ya taifa ya Misri, akiwa na mabao 69 katika mechi 176, rekodi inayomfanya kuwa mmoja wa wachezaji mahiri barani Afrika.

Alishiriki katika matoleo saba ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Je, ataandika historia nyingine katika AFCON ya 2025?

Pape Thiaw, Senegal

ll

Chanzo cha picha, Getty Images

Miaka minne baada ya ushindi wa kihistoria wa Aliou Cissé huko Yaoundé, Senegal inajikuta tena ikiwa imebakisha mechi mbili chini ya uongozi wa kocha wa ndani.

Baada ya kujizolea umaarufu katika kiwango kizuri wakati wa CHAN 2022, na alishinda akiwa na Senegal kabla ya kujiunga na benchi la timu ya taifa, Thiaw alichukua nafasi ya kocha mkuu Desemba 2024 akiwa na dhamira ya kufanya vizuri kama mtangulizi wake katika nafasi hiyo.

Kama Aliou Cissé mwaka 2021, Pape Thiaw, mchezaji wa kizazi cha 2002, ana fursa ya kihistoria ya kuwaongoza Lions of Teranga kwenye taji jipya la bara, akithibitisha ukuu wa makocha wa ndani.

Makocha wa Kiafrika sasa wana ujuzi wa kanuni za kisasa za mchezo, huku pia wakiwa na faida ya ujuzi wa kina wa muktadha wa kitamaduni, kisaikolojia na kijamii wa timu zao za kitaifa.

Eric Chelle, Nigeria

pp

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Januari 2025, Nigeria ilimteua kocha wa zamani wa Mali, Eric Chelle, kuwa kocha mkuu mpya wa timu yake ya taifa ya wanaume.

Timu hiyo ya Afrika Magharibi ilifika robo fainali ya Afcon ya 2023 mwaka jana, ambapo ilitolewa na Ivory Coast walioshinda baada ya muda wa ziada.

Alizaliwa mwaka 1977, Eric Sekou Chelle anajivunia uraia wa Ufaransa, Ivory Coast, na Mali. Kazi yake ya ukocha ilianza katika mazingira ya ushindani ya soka la Ufaransa.

Chelle alianza katika klabu za Ufaransa za US Boulogne na FC Martigues kabla ya kupanda kimataifa. 2023, aliiongoza Mali wakati wa AFCON iliyofanyika Côte d'Ivoire, na kuwaongoza kumaliza robo fainali.

Uwezo wake wa kuinua timu ulimfanya atambulike haraka, na kwenda katika klabu ya Algeria ya MC Oran kabla ya jukumu la sasa Nigeria.

Michuano ya AFCON ya 2025 inaashiria kuonekana kwa Chelle kwa mara ya pili katika mashindano hayo kama kocha mkuu.

Akiwa kocha wa Mali aliweza kufuzu robo fainali mwaka 2023, akionyesha ustadi wake wa kukabiliana na ugumu wa mashindano makubwa ya soka ya Afrika.

Walid Regragui, Morocco

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Regragui ameiongoza Morocco tangu Agosti 2022 na aliiongoza timu hiyo hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia la mwaka huo huko Qatar katika mashindano yake ya kwanza makubwa akiwa na timu hiyo.

Chini ya uongozi wake, timu ya Morocco imepata rekodi ya ajabu, na kuwa timu ya kwanza ya Kiafrika katika historia kufikia nusu fainali ya Kombe la Dunia. Hatimaye Morocco ilimaliza katika nafasi ya nne.

Walid Regragui aliyezaliwa Ufaransa na anabeba uraia wa nchi hiyo na Morocco, anashikilia kile kinachoweza kuwa kiti cha ukocha chenye joto zaidi katika Kombe la Mataifa ya Afrika la Total Energies 2025.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49, atakuwa meneja wa Atlas Lions watakapocheza mbele ya umati wa watu Morocco.

Katika kipindi chote cha ukocha wake, Regragui ameongoza vilabu kadhaa vya Morocco, ikiwa ni pamoja na Fath Union Sport na Wydad Casablanca. Pia alifanya kazi nje ya nchi, akifundisha klabu ya Al-Duhail ya Qatar.