Je, vita baina ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ni halali?

A woman holding a picture of two children is sitting on the ground being comforted by two other woman; the legs of many others standing around them are visible.

Chanzo cha picha, Amirhossein Khorgooei/ISNA/West Asia News Agency via Reuters

Maelezo ya picha, Mazishi yamefanyika baada ya kile ambacho mamlaka ya Iran ilisema ni shambulizi la Marekani na Israel dhidi ya shule moja kusini mwa Iran
Muda wa kusoma: Dakika 7

Mashambulizi yaliyoratibiwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran, na majibu ya Iran tayari yamesababisha vifo vya raia na kulaaniwa na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, akiwasihi pande zote mbili kuheshimu sheria za kimataifa.

Pande zote mbili zinadai kuwa zina haki, lakini ili kuthibitisha kama mashambulizi ya awali dhidi ya Iran yalikuwa halali, lazima turudi kwenye viwango vya sheria za kimataifa ambavyo nchi nyingi ziliunga mkono, baada ya vitisho vya vita vya pili vya dunia.

Muda mfupi baada ya Marekani na Israel kuanza kuishambulia Iran mnamo Februari 28, rais Donald Trump aliishutumu Tehran kwa kutengeneza silaha za nyuklia ambazo zinatishia washirika wa Marekani na zinaweza "kufikia nchi ya Marekani hivi karibuni".

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya nje Marco Rubio alisema mnamo Machi 2 kwamba Marekani ilibidi "iwafukuze mapema" kwani utawala ulijua kutakuwa na "hatua ya Israel" dhidi ya Iran.

An aerial photo of at least five rows of rectangular holes in the ground, some marked and yet to be dug out, with three mechanical diggers visible.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Serikali ya Iran imetoa picha za kile inachosema ni makaburi ya watu waliouawa katika shule moja katika mji wa kusini wa Minab.

Wakati huo huo, rais wa Israel Isaac Herzog aliambia kipindi cha BBC Radio 4 cha Today kwamba mipango inayodaiwa ya Iran "kutengeneza bomu" ilitosha kuhalalisha mashambulizi hayo.

Iran ilijibu kwa kuishambulia Israeli na nchi za Mashariki ya kati zinazohifadhi kambi za kijeshi za Marekani, ikidai kujilinda.

Idadi ya majeruhi inaendelea kuongezeka.

Zaidi ya watu 780, wakiwemo wasichana 165 na wafanyakazi waliouawa katika kile ambacho mamlaka ya Iran ilisema ni shambulio la Marekani na Israel kwenye shule, wameuawa nchini Iran, kwa mujibu wa shirika la misaada nchini Iran.

Nchini Lebanon, zaidi ya watu 50 walifariki wakati wa mashambulizi ya Israeli Jumatatu.

Kwa upande mwingine, makumi ya wengine, wakiwemo wanajeshi sita wa Marekani, walifariki nchini Israel na nchi nyingine za Ghuba.

Je, mashambulizi hayo yalikuwa halali?

Wataalamu wa sheria ambao BBC ilizungumza nao wanasema kwamba masharti ya kisheria ya shambulio la awali kati ya Marekani na Israel hayaonekani kutimizwa - lakini kulipiza kisasi kwa Iran kunaweza pia kuwa kulikiuka sheria za kimataifa.

Chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, hati ya mwanzilishi wa shirika hilo, kwa ujumla nchi zimepigwa marufuku kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya taifa lingine isipokuwa kama kuna ubaguzi maalum unaotumika.

Vifungu viwili ni muhimu:Kifungu cha 2(4): Kinakataza tishio au matumizi ya nguvu dhidi ya mataifa mengine.

Kifungu cha 51: Kinaruhusu kujibu shambulio la silaha.

Baadhi ya majimbo yanasema hii inajumuisha mashambulizi ambayo yanakaribia.

Several people stand outside a damaged building with its windows blown out.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Israel ilizindua mashambulizi ya anga dhidi ya Lebanon siku ya Jumatatu, ikijumuisha kitongoji cha mji mkuu wake Beirut

Kwa hivyo, swali muhimu la kisheria ni ikiwa Iran ilikuwa tishio.

Susan Breau, mtaalamu wa sheria wa kimataifa katika Taasisi ya kisheria nchini Uingereza, anasema kujilinda kisheria kutahitaji "ushahidi usiopingika wa uwezekano wa kushambuliwa", akiongeza kwamba hajaona ushahidi wowote kama huo.

Wakili maarufu wa haki za binadamu Sir Geoffrey Nice anaunga mkono.

Kuanzia 1998 hadi 2006, aliongoza mashtaka ya rais wa zamani wa Yugoslavia Slobodan Milošević katika Mahakama ya kimataifa ya Jinai.

"Hakuna ushahidi uliotolewa," anasema. "Kuna uwezekano mkubwa kwamba vita ilianzishwa kinyume cha sheria."

Nchini Marekani, Wabunge wa democrats wengi wanasema kwamba operesheni dhidi ya Iran ni kinyume cha sheria, wakidai kwamba bunge pekee ndilo lililopewa mamlaka ya kutangaza vita.

Hata hivyo, amiri jeshi mkuu, rais wa Marekani anaweza kufanya shughuli fulani za kijeshi bila tamko rasmi la vita.

Je, kulikuwa na tishio la karibu?

Flames engulf the top of a tower block at night while smoke billows into the night sky. A tall building next to it appears not to have been damaged

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Bahrain: Jengo lateketea Jumapili baada ya kushambuliwa na ndege isiyo na rubani ya Iran
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Rais Donald Trump alisema kuwa Marekani ilijaribu kufanya mazungumzo na Iran baada ya kushambulia vituo vitatu vya nyuklia mwezi Juni 2025, lakini Tehran "ilikataa kila fursa ya kuachana na mpango wake wa nyuklia."

Alisema Iran ilikuwa inajaribu kujenga upya mpango wake wa nyuklia na kuendeleza makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kutishia washirika wa Marekani na wanajeshi wake walioko nje ya nchi, na hatimaye kuweza kufikia ardhi ya Marekani.

Ezra Cohen, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha ujasusi na usalama wa rais Trump katika utawala wake wa kwanza, aliiambia BBC kuwa:

"Kuna taarifa za kutosha kwamba… Iran ilikuwa inajiandaa kutumia vikosi vyake vya makombora kushambulia kabla ya Marekani au Israel kufanya uamuzi wa kuendelea na mashambulizi."

Rafael Grossi, mkurugenzi wa International Atomic Energy Agency (IAEA), pia alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu kuwa Iran ina "mkakati mkubwa sana katika masuala ya nyuklia," lakini hawajaona ushahidi unaoonyesha kuwepo kwa "mpango maalum wa kutengeneza silaha za nyuklia."

Ripoti ya Mei 2025 ya Defense Intelligence Agency (DIA) pia ilihitimisha kuwa Iran bado iko miaka kadhaa mbali na kuzalisha makombora ya masafa marefu.

Wataalamu pia wanasema kuwa kauli ya awali ya Trump kwamba mpango wa nyuklia wa Iran "ulifutwa kabisa" wakati wa vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran mwaka jana inaonekana kupingana na wazo la kuwepo kwa tishio.

Three cars drive along a three-lane highway with smoke ahead of them. The sky is dark blue and the sides of the road are dusty with a few shrubs.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Moshi unafuka kutoka kiwanda cha kusafisha mafuta cha Ras Tanura cha Saudi Arabia siku ya Jumatatu baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani kutoka Iran

Mgogoro mkubwa katika sheria za kimataifa unahusu jinsi neno "hatari ya tishio inavyopaswa kufasiriwa kwa usahihi wake.

Ilivyozoeleka, "uwepo wa tishio" humaanisha "wakati wa mwisho kabisa ambapo unaweza kuzuia shambulio ambalo vinginevyo lingeangukia eneo lako bila kuepukika," anaeleza Marc Weller, msomi wa sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Cambridge.

Pia kumekuwa na mjadala wa muda mrefu kuhusu ni lini taifa linaweza kisheria kutumia nguvu katika kujilinda kwa kujihami mapema, anasema Breau: baadhi ya wataalamu hudai kuwa shambulio lazima liwe tayari limeanza; wengine wanasema hatua hiyo inaweza kuhalalishwa ikiwa kuna ushahidi wa kuaminika kwamba shambulio litatokea karibuni sana.

"Lakini si baada ya miaka 10," anasisitiza.

Aidha, kuna masharti mawili ya kujilinda kisheria, kulingana na Breau:

Lazima kuwepo na ulazima yaani "hakuna njia nyingine mbadala."

Uwiano wa matumizi ya nguvu lazima uwe sawia na tishio lililopo.

Wote wawili, Weller na Breau, wanaona shambulio la Israel dhidi ya Misri mwaka 1967 wakati wa Six-Day War kama mojawapo ya mifano inayotajwa sana ya kujilinda kwa kujihami mapema katika historia ya kisasa.

Wakati huo, wengi waliamini kuwa wanajeshi wa Misri waliokuwa wamekusanyika mpakani walikuwa tayari kuanzisha shambulio, anasema Breau.

Hata hivyo, anaeleza kuwa hata wakati huo, shambulio la Israel lilionekana kuwa "lenye utata."

A firefighter at night projects water from a hose at a burning car that is lit up in orange flames; other cars around it are severely damaged works.
Picture from Itai Ron / Reuters - no access to Israeli outlets

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Iran ilishambulia mji mkuu wa Israeli Tel Aviv kwa makombora na ndege zisizo na rubani mnamo tarehe 28 Februari

Je, jibu la Iran ni halali?

Wataalamu wengi wanaamini kwamba kulipiza kisasi kwa Iran kunaweza pia kuwa kulivunja sheria za kimataifa.

Weller anasema Iran imekiuka sheria za kimataifa kwa kufanya "mashambulizi ya kiholela" dhidi ya nchi za Ghuba.

Sir Nice anasisitiza kwamba ingawa Iran inaweza kujilinda, jibu lazima liwe "sawa". Uwiano, anasema, unahitaji kupima shambulizi la kijeshi dhidi ya uharibifu unaosababishwa.

"Kuhusu Iran, matumizi ya makombora ambayo hayajalengwa kwa usahihi na kwa umakini yanaweza kwa urahisi kusemwa kuwa hayakuwa ya uwiano na kwa hivyo ni kinyume cha sheria."

Breau anakubaliana na hilo na anataja hoteli maarufu duniani ya Fairmont Dubai iliyoko katikati ya jiji la Dubai, ambayo ilishambuliwa na vikosi vya Iran.

"Hilo halikulenga jeshi, bali raia," anasema.

Kielelezo hatari

People and rescue forces working in rubble following an Israel strike on a school in Minab, Iran, 28 February 2026 Image from Abbas Zakeri/Mehr News/WANA (West Asia News Agency) via REUTERS

Chanzo cha picha, West Asia News Agency via Reuters

Maelezo ya picha, Iran: Waokoaji wameendelea kuopoa miili kutoka kwenye vifusi baada ya shambulio la anga kati ya Marekani na Israel kwenye shule moja huko Minab

Wataalamu wanaonya kuwa kushindwa kutambua wazi matumizi ya nguvu yaliyo kinyume cha sheria kunaweza kudhoofisha mfumo wa sheria za kimataifa kwa kipindi kirefu.

Breau anaonya kuwa mataifa mengine yanaweza kutumia hoja kama hizo na kuamua kutumia nguvu, kama vile China, ambayo inaitazama Taiwan kama jimbo lililojitenga.

"Hakuna jambo hatari zaidi kwa mfumo wa kimataifa kuliko kukubaliana na matumizi ya nguvu yaliyo kinyume cha sheria," anasema.

Katika makala yake kwa Chatham House, Weller anaonya kuwa itakuwa vigumu kupinga "uchokozi zaidi wa Urusi au upanuzi unaoweza kufanywa na China" bila "kuzua malalamiko ya viwango viwili na unafiki," na kwamba Marekani pamoja na mataifa mengine huenda "yakajutia kupoteza mamlaka yao ya kisheria na kimaadili hali hii itakayosababisha."

Iwapo mataifa yenye nguvu yataendelea kukiuka sheria za kimataifa bila kuchukuliwa hatua, wengi wana hofu kwamba utaratibu wa dunia ulioundwa baada ya vita kuu utaanguka na nafasi yake kuchukuliwa na utawala wenye nguvu zaidi.