Marekani imetumia droni za gharama nafuu dhidi ya Iran kwa mara ya kwanza

Chanzo cha picha, US CENTCOM
Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) imetangaza kwamba Marekani imetumia ndege mpya zisizo na rubani za masafa marefu dhidi ya Iran. Ndege hizi zisizo na rubani zinafanana kimuundo na ndege zisizo na rubani za Iran za "Shahed".
Kulingana na picha zilizochapishwa, kuna uwezekano kwamba ndege hizi zisizo na rubani zina vifaa vya mawasiliano vya setilaiti.
Ni droni za bei nafuu zinazojulikana kama "Lucas," kama na zile za Shahed-136 za Irana ambazo nazo pita ni za gharama nafuu." Marekani imethibitisha matumizi ya kwanza ya ndege hizi nchini Iran, lakini haijataja matumizi ya satelaiti katika muundo wake.
Kutumia ndege zisizo na rubani zilizo na vifaa vya mawasiliano vya setilaiti huruhusu kudhibitiwa wakati wote wa safari. Ikiwa ndege zisizo na rubani zimewekwa kamera, mwongozaji wa anaweza kuona picha mubashara.
Kuvuruga mawimbi ya setilaiti si rahisi. Muendeshaji anaweza kuirusha ndege isiyo na rubani kwenye mwinuko wa chini ili kuepuka rada au kuepuka kupita katika maeneo yanayojulikana kuwa na ulinzi wa anga. Hii inafanya iwe vigumu sana kuizuia ndege isiyo na rubani kama hiyo.
Uwezo huu unaweza kuongeza zaidi ufanisi wa droni hii na kuongeza usahihi na uhuru wake wa uendeshaji.
Jinsi zilivyotumiwa na Urusi

Chanzo cha picha, US CENTCOM
Mwezi Desemba, vikosi vya Urusi vilianza kutumia ndege zisizo na rubani zinazotumia vifaa ya Starlink katika vita vya Ukraine, vifaa hivyo vilinunuliwa nje ya nchi na kisha kuingizwa Urusi, na hivyo kukwepa vikwazo.
Serhiy Beskrestov, mshauri wa Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, alitangaza mwishoni mwa Januari kwamba mamia ya visa vilivyothibitishwa vya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani zenye vifaa vya Starlink vilirekodiwa kufikia wakati huo.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Kuna tishio kubwa. Hebu fikiria ndege isiyo na rubani ambayo mwendeshaji anaielekeza kutoka ardhi ya Urusi na anaona kila kitu kwa wakati huo. Sote tunajua kwamba Starlink inafanya kazi vizuri na hutoa picha za wazi. Kwa hivyo hiyo ni moja ya changamoto ambazo tunapaswa kukabiliana nazo na kuzishughulikia," alisema.
Mwanzoni mwa mwezi Februari, Wizara ya Ulinzi ya Ukraine ilifikia makubaliano na kampuni ya utengenezaji silaha kuzima vituo vya mawasiliano vya setilaiti ambavyo havikusajiliwa nchini Ukraine.
Kwa hivyo, jeshi la Urusi halikupoteza tu uwezo wa kutumia ndege zisizo na rubani zilizo na vifaa hivi, pia lilipoteza matumizi ya Intaneti katika maeneo mengi ya mstari wa mbele, kwani Starlink ilikuwa ikitoa mawasiliano ya kuaminika katika vitengo vingi vya Urusi.
Serikali ya Urusi haiwezi kuweka mfumo mwingine wa mawasiliano ya setilaiti kama ya Starlink kwa sababu haina mfumo wa anga za juu kama huo.
Kampuni binafsi ya Urusi inayoitwa Boro 1440 ina mkusanyiko wa satelaiti za mawasiliano sawa na ule unaotumiwa na Starlink. Kampuni hiyo ilipanga kuzindua kundi la kwanza la satelaiti mwaka 2025, lakini mpango huo umeshindwa
Droni za gharama nafuu
Hakuna taarifa katika vyanzo vya umma kuhusu ni nani aliyekuja na wazo la kwanza la kuweka vifaa vya Starlink kwenye droni.
Kwa mara ya kwanza Desemba 15, 2025, Sergey Beskrestov, mtaalamu wa Ukraine katika uwanja wa teknolojia za redio za kijeshi, alitangaza ugunduzi wa ndege isiyo na rubani ya Urusi iliyo na vifaa vya Starlink.
Wiki mbili mapema, Desemba 3, Kamandi Kuu ya Marekani ilichapisha picha za ndege zisizo na rubani za Lucas zilizokamilika zikiwa na vifaa vinavyofanana na vifaa vya Starlink.
Hata hivyo, wazo la matumizi makubwa ya ndege zisizo na rubani za kushambulia za bei nafuu lilianzia Iran na Urusi.
Urusi ilianza mashambulizi yake dhidi ya Ukraine mwaka 2022 kwa kutumia ndege zisizo na rubani za Iran "Shahed," ambazo ilizipa jina la "Geranium-2," na imeendelea kuongeza uzalishaji wa mifumo hii.
Mbali na kufanya uharibifu katika mashambulizi, ndege hizi zisizo na rubani pia hulazimisha mifumo ya ulinzi wa anga kutumia rasilimali kubwa ili kuziharibu. Katika baadhi ya matukio, gharama ya kuzidungua ni kubwa kuliko thamani ya ndege zenyewe.
Kulingana na Reuters, kila ndege isiyo na rubani inaweza kugharimu karibu dola $35,000. Ili kuzitumia ndege hizi zisizo na rubani, kitengo maalum kiliundwa nchini Marekani na kupelekwa Mashariki ya Kati, kikiitwa "Operesheni Scorpion Strike Group."














