Air Force One: Siri tisa zinazoifanya ndege inayombeba rais wa Marekani kuogopwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Ifikiapo mwaka 2024, iwapo mambo yatafanyika kulingana na mipango iliowekwa na Marekani, Utawala wa rais Joe Biden utapokea ndege mpya aina ya Airforce One .
Ndege za sasa ni aina ya Boeing 747 na sawa na zile zitakazokuja, ijapokuwa zitakuwa aina mpya ambayo ni ndefu na pana zaidi ya mtangulizi wake
Lakini licha ya kuwa ndege ya abiria, tunauliza ni kwanini ndege hiyo inaogopwa sana duniani?
1.Inaweza kuhimili mlipuko wa nyuklia!
Ndege hiyo ilioundwa kwa lengo la kivita ina uwezo wa kuhimili mshindo wa mlipuko wa kinyuklia. Iwapo mlipuko wa bomu hilo ungetokea rais wa Marekani angeepuka .
Anaweza kutoa maagizo na mikakati kukabili vita akiwa ndani. Hii ni kwasababu mwili wa ndege hiyo umeundwa kwa lengo la kuepuka mlipuko wowote .
Katika madirisha ya ndege hiyo kuna waya zilizowekwa kuzuia mionzi, mbali na kuzungukwa na mabati yaliowekwa waya kuzuia mapigo ya umeme, joto, na moto.

2.Ndege hiyo inaweza kujazwa mafuta ikiwa angani
Teknolojia kushangaza ya ndege aina ya Airforce One ni uwezo wake wa kuweka mafuta ikiwa angani.
Ijapokuwa ndege mpya ya Airforce One inayotarajiwa kuzinduliwa 2024 huenda ikose teknolojia hiyo, ni muhimu sana.
Ili kuweza kujazwa mafuta ikiwa angani ni sharti kuwepo kwa ndege nyengine na tangi la mafuta katikati.
Operesheni hiyo kwa jina boom husimamia uhamishaji huu wa mafuta huku rubani akifuatilia kwa makini.
Operesheni ya boom hukata mara tu mafuta yanapojaa.
Iwapo ndege moja itasogea kidogo mafuta hayo pia hujikata mara moja. Kwa kujaza mafuta angani , ndege hiyo inaokoa muda wa kutua ardhini na kujaza mafuta
3. Ina ngazi zake na mashine ya kupandisha mizigo ndani ya ndege
Kwa kuwa ni ndege ya rais , hakuna sababu ya ukosefu wa raslimali zinazotumika kutengeneza ndege hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ndege hiyo ina ngazi inayoweza kuwekwa na kutolewa hivyobasi haitegemei ngazi ya uwanja wa ndege kwa watu kushuka ndani ya ndege hiyo au kupanda.
Hatua hiyo inahakikisha kuwa ngazi hiyo haina kasoro yoyote.
Kwasababu hizohizo ndge hiyo ina mashine ya kupandisha mizogo ndani ya ndege hiyo hivyobasi hakuna uwezekano wa mzigo isiojulikana kuingizwa ndani ya ndege hiyo.
4. Ina vifaa tofauti vya kiusalama - ikiwemo uwezo wa kutoa miali ya moto.
Kwa kuwa iliundwa kwa lengo la kivita na usalama wa Rais, kuna teknolojia ya usalama iliotengenezwa ndani yake.
Ndege hiyo ina vifaa vya kielektroniki vinavyoweza kuzikabili rada zozote za adui zitakazotambuliwa.
Ndege hiyo pia inaweza kujilinda dhidi ya makombora ya adui zake kwa kutoa miale ya moto dhidi yake inayoweza kuyakabili.

Chanzo cha picha, Ikulu ya Whitehouse
5. Kifaa kinachoweza kuficha na kutatiza mawasiliano
Mawasiliano ni mojawapo ya vitu vinavyolengwa kwa urahisi na hutumika sana wakati wa shambulio.
Ili kuhakikisha kuwa kuna viwango vya juu vya usalama wakati kunapokuwa na mawasilino ya juu ya ndege na ardhini , Airforce One ina uwezo wa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yako salama kupitia kuficha na vifaa vya kutataiza.
Ishara zilizosimbwa au kufichwa za GPS husaidia kuelewa chanzo cha habari inayowasilishwa.
6.Chumba cha mawasiliano
Ndege ya Airforce One ina kitengo kizima cha mawasiliano kinachotumiwa na Rais kinachomwezesha kuwasiliano licha ya kuwa angani .

Chanzo cha picha, Getty Images
Anaweza kupiga simu za kawaida simu za video, kufanya mikutano ya video, kuhutubia umma, na kadhalika .
Kwa kuwa ndege hiyo inaweza kujazwa Mafuta ikiwa angani , iwapo kutakuwa na mzozo mrefu Rais anaweza kufanya kazi zake akiwa ndani ya ndege.

Chanzo cha picha, Ikulu ya Whitehouse
7. Chumba cha matibabu
Huku ikiwa kuna mikakati mingi ambayo imewekwa kwa lengo la kuzuia tukio lolote, matokeo yake pia yametiliwa maanani.
Ndege hiyo ina kituo kizima cha afya kilicho na madaktari na vifaa vya kisasa tayari kukabiliana na tatizo lolote la kimatibabu.
Pia kuna daktari ndani ya ndege hiyo kusimamia matibabu ya rais na mawaziri wake.
Huku kukiwa na mpango wa kimatibabu ndege aina ya Airforce One ina uwezo mkubwa kwa kweli.
8. Ina Vifaa na teknolojia ambazo haziwezi kuonekana na jicho la kawaida.
''Nukuu maarufu inayoelezea ugumu wa ubongo wa binadamu vizuri''.
Kuna baadhi ya vifaa na teknolojia zinazotumika katika ndege ya Airforce One ambazvyo haviwezi kuonekana kwa jicho la kawaida.
Kuna mambo mengi kuhusu ndege hiyo ambayo mtu wa kawaida hawezi kuelewa.
Pia ni vigumu sana kwa wanajeshi kutambua teknolojia hiyo na hiyo ndio sababu inaitwa Airforce One - mojawapo ya- ndege isio ya kijeshi inayoogopwa zaidi duniani.
9. Ikulu ya Whitehouse ilio angani
Marekani huwavutia wengi wakati ndege hiyo inapopenyeza katika mawingu na kumsafirisha rais wake katika mataifa tofauti.

Chanzo cha picha, Ikulu ya Whitehouse
Wengi wanasema kwamba ndege hiyo ni ikulu ya whitehouse ilio angani, kwasababu ina ofisi ya Rais , ina chumba cha mikutano, pamoja na mawaziri ndani yake.












