Coronavirus: Jinsi wanyama wanavyohusishwa katika mlipuko wa magonjwa mapya

Urban monkeys in Varanasi, India

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati ulimwengu ukikabiliana na virusi vipya vya corona ambavyo vimesambaa kutokea nchini China mpaka mataifa mengine yapatayo 15.

Mlipuko wa virusi hivi vipya vya ugonjwa wa corona havijawahi kutokea kabla.

Lakini virusi hivyo vipya vinasadikiwa kuwa vimesababishwa na wanyama pori na kufanya hatari ya magonjwa ambayo yanatokana na wanyama.

Jambo ambalo linaonekana kuwa tatizo kubwa kwa siku za baadae wakati ambao mabadiliko ya tabia nchi na utandawazi wa namna wanyama na binadamu wanavyohusiana.

Wanyama wanawezaje kuwafanya watu waumwe?

Kwa miaka zaidi ya 50, maambukizi ya magonjwa yamekuwa yakitoka kwa wanyama mpaka kwa binadamu.

Mwaka 1980, janga la virusi vya Ukimwi vilidaiwa kuwa vilitokea kwa sokwe, mwaka 2004 mpaka 2007 mafua makali ya ndege na nguruwe pia walidaiwa kusababisha mafua makali ya Swine mwaka 2009.

Vilevile ilibainika kuwa maambukizi ya Sars yalitokana na popo huku Ebola pia ikidaiwa kusababishwa na popo.

Chickens in cages, China

Chanzo cha picha, Getty Images

Binadamu wamekuwa wakipata magonjwa kutoka kwa wanyama, haswa maambukizi ya magonjwa ya hivi karibuni yanaelezwa kuwa yametokea kwa wanyama pori.

Lakini mabadiliko ya mazingira yanaongeza kasi ya maambukizi ya aina hiyo kutokea, huku ongezeko la watu wanaoishi mjini na kusafiri mataifa mbalimbali wakati ugonjwa huo umeanza unafanya maambukizi yasambae kwa kasi zaidi.

Ni namna gani virusi hivi vinahama kutoka kwa wanyama mpaka kwa binadamu?

Wanyama wengi huwa wana bakteria hatari na virusi ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa.

abiria wa treni Hong Kong

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Abiria wa treni mjini Hong Kong

Mzunguko wa virusi huwa unategemea nani ambaye yuko navyo kwa wakati fulani na vimewezaje kufika upande mwingine.

Maambukizi mapya ya virusi yameonyesha kuwa

Kwa mfano ,asilimia kumi ya watu waliokufa kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa Sars mwaka 2003, ukilinganisha na mafua makali ambayo yalikuwa chini ya 0.1%

Nyani wakiwa kwenye takataka

Chanzo cha picha, Getty Images

Mazingira na mabadiliko ya tabia nchi yanabadilisha tabia ya wanyama ya namna wanavyoishi ,maeneo wanayoishi na huwa wanakula nini.

Jinsi maisha ya binadamu yalivyobadilika pia, asilimia 55 ya idadi ya watu duniani kote wanajishi mjini na kuanzia 35% miaka 50 iliyopita.

Na miji hii mikubwa ina makazi mapya ya wanyama pori kama panya, vicheche, fisi, nguchiro, ndege,nyani na wanyama wengine ambao wanaweza kuepo kwenye maeneo ya kijani, sehemu za kupumzikia na bustani , na kuacha taka ambazo zinaweza kuwafikia binadamu.

Mara nyingi wanyama pori huwa wanaonekana katika miji zaidi ya porini kwa sababu kuna upatikanaji wa chakula kingi maeneo ya mjini na kufanya mzunguko wa upatikanaji wa magonjwa uwe rahisi.

Nani yuko hatarini?

Magonjwa mapya yanayojitokeza mara nyingi ni hatari zaidi ndio maana magonjwa mapya huwa yanapewa uangalizi wa karibu zaidi.

Baadhi ya makundi ya watu wako kwenye hatari ya kupata magonjwa zaidi ya wengine.

A Bangladesh livestock market during an avian flu outbreak

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mjini Bangladesh wakati wa mlipuko wa mafua ya avian yaliyosababishwa na kuku

Miji maskini inapaswa kufanyiwa kazi ya usafi kwa ujumla, kwa sababu kama mazingira si safi basi inakuwa rahisi kwa magonjwa kuenea.

Watu ambao wana mifumo dhaifu kwa kutokuwa na afya nzuri wako kwenye hatari ya magonjwa zaidi, mfano mtu ambaye hana virutubisho vya mlo kamili, anaishi katika maeneo ambayo kuna hewa chafu na mazingira machafu.

Na wale ambao wakiugua huwa ni vigumu kupata huduma za kiafya na inawawia vigumu.

Maambukizi mapya yanaweza kusambaa katika miji mikubwa ambayo ina mkusanyiko mkubwa wa watu, ambao wanavuta hewa kwa pamoja na wako kwatika mazingira yanayofanana.

Baadhi ya tamaduni, watu huwa wanakula chakula ambacho wanahusiana na wanyama pori.

Presentational grey line

Tunapaswa kufanya nini?

Jamii na serikali zinajaribu kukabiliana na maambukizi mapya ya magonjwa kuwa janga la kivyake vyake bila kuhusisha dalili zake kwa kuangalia mabadiliko yanayotokea katika ulimwengu.

Kadri mazingira yetu yanavyobadilika , ndio magonjwa mapya pia yanaibuka.

Asilimia 10 tu ndio imeandikwa kuwa magonjwa mapya mengi yanahusishwa na wanyama.

Kuna umuhimu wa kuangalia jinsi magonjwa haya mapya yanaanzia wapi mpaka kufikia kuuwa watu katika maeneo ya mjini.

Kuweka mazingira kuwa safi ni jambo moja muhimu ambalo linaweza kusaidia kupunguza mlipuko wa magonjwa na kusambaa kwake.

Lakini pia kubadili namna watu wanahusiana na wanyama katika mazingira yao ni jambo muhimu pia kuzingatiwa.

line