Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Arsenal yajiunga na mbio za kumsajili Guehi

Beki wa Crystal Palace na England Marc Guehi

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Arsenal imejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa England na Crystal Palace Marc Guehi, 25. (Mirror)

Hata hivyo, Manchester City ina imani itamsajili Guehi mbele ya wapinzani wao Liverpool. (Sta)

Tottenham wamefikia makubaliano ya kibinafsi na kinda wa Brazil mwenye umri wa miaka 19 na beki wa wa Santos Souza kabla hajahamia Ligi ya Premia Premia. (Fabrizio Romano)

Mshambuliaji wa Misri Omar Marmoush, 26, hana mpango wa kuondoka Manchester City Januari na bali anakusudia kusalia katika klabu hiyo na kupigania nafasi yake. (Florian Plettenberg)

Real Madrid inaongeza mbio za kumsaka beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani Nico Schlotterbeck, 26, huku mlinzi wa Ufaransa Dayot Upamecano, 27, akitarajiwa kusaini mkataba mpya Bayern Munich. (Bild - usajili unahitajika)

Manchester City ina nia ya kumsajili beki wa Brentford mwenye umri wa miaka 21 na Italia chini ya umri wa miaka 21 Michael Kayode. (Caughtoffside)

Omar Marmoush

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Omar Marmoush

Real Madrid wako tayari kumuuza Antonio Rudiger mwezi Januari hii kwa euro 10m (£9m), huku klabu za zamani za Chelsea na Paris St-Germain zikiwania kumsajili beki huyo wa Ujerumani, 32, ambaye kandarasi yake uwanjani Bernabeu inakamilika msimu wa joto. (Fichajes - kwa Kihispania)

Beki wa Union Berlin Mholanzi Danilho Doekhi, 27, ana hamu sana kuhamia Leeds United kujiunga na meneja Daniel Farke. (Team talk)

Aston Villa wafikia mkataba wa £10m kumsajili mshambuliaji wa Luxembourg, 16, Metz Brian Madjo. (Fabrizio Romano)