Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Bournemouth inamfukuzia Nwaneri Arsenal

Ethan Nwaneri

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Arsenal Ethan Nwaneri
Muda wa kusoma: Dakika 3

Bournemouth ina nia ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Arsenal Ethan Nwaneri, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza aliye na umri wa chini ya umri wa miaka 21, 18, anapendelea kusalia na The Gunners hadi mwisho wa msimu huu, ingawa anatatizika kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. (Independent)

Meneja wa Crystal Palace Oliver Glasner anasema "ataimarisha" mazungumzo kuhusu mkataba mpya na klabu hiyo "wiki zijazo" kabla ya kufanya "uamuzi wa mwisho". (Mirror)

Mlinzi wa Palace Marc Guehi anasakwa mwezi huu na Liverpool inaweza kuwa tayari kuwasilisha dau la pauni milioni 20 ili kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 25. (Mirror)

Mlinzi wa Liverpool Joe Gomez, 28, na mlinzi wa Nottingham Forest wa Brazil Murillo, 23, ni chaguo mbili ambazo AC Milan inapolenga kuimarisha safu yake ya nyuma. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Beki wa Manchester City John Stones yuko katika mwaka wa mwisho wa kandarasi yake katika klabu hiyo lakini meneja Pep Guardiola ana mashaka na mustakabali wa beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 31 katika klabu hiyo. (The Times)

Mshambulizi wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli yuko tayari kujiunga na klabu ya 14 katika maisha yake ya soka huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 akielekea kwenye klabu ya daraja la pili ya UAE Al Ittifaq. (Goal)

Kipa wa Ufaransa Mike Maignan, 30, amekuwa akihusishwa na Chelsea lakini anakaribia kusaini mkataba mpya AC Milan. (Sky Sports Italia, via Football Italia)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Bayern Munich na Ufaransa Dayot Upamecano, 27, wamekubaliana kwa kimsingi kusaini mkataba mpya, huku suala lililosalia likiwa ni kuhusu kipengele cha kutolewa katika mkataba huo. (Fabrizio Romano)

Liverpool wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Mason Greenwood. Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 24 amefanya vyema zaidi Marseille katika ligi hii. (Fichajes - kwa Kihispania)

Tottenham iko kwa mazungumzo ya kumsajili beki wa Brazil Souza kutoka Santos baada ya dau la awali la pauni milioni 8 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kukataliwa. (Standard)