Ligi Kuu England: Chelsea yatumia £230m kununua wachezaji 11 - kunani?

Ju

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Enzo Maresca aliteuliwa kuwa meneja wa Chelsea mwezi Juni
    • Author, Nizaar Kinsella
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Chelsea inatawala dirisha jingine la usajili. Hili litakuwa ni dirisha la tatu la uhamisho wa majira ya kiangazi tangu klabu hiyo kuwa chini ya wamiliki Behdad Eghbali na Todd Boehly kuanzia 2022.

Chelsea imesajili wachezaji wengi zaidi kuliko wapinzani wake na inaonekana kuwaondoa wale wa zamani.

Chelsea ilimsajili mshambuliaji wa Wolves, Neto kwa pauni milioni 54 siku ya Jumapili, na hivyo kufikia usajili wa wachezaji 11 waliosajiliwa majira ya joto na wastani wao wa umri ni chini ya miaka 21. Kikosi chao kwa sasa kina zaidi ya wachezaji 50.

Ingawa dili la pauni milioni 35 la kumuongeza Samu Omorodion wa Atletico Madrid limeshindikana, wanatarajiwa kuleta mchezaji mwingine wa ziada, ambaye anatajwa huenda akawa ni Joao Felix atakayekwenda Stamford Bridge.

Baadhi ya wale ambao wamejiunga na timu hiyo watakwenda moja kwa moja kwa mkopo katika timu nyigine na wengine watauzwa kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili wa Agosti 30.

Tangu Clearlake Capital na Boehly kuchukua umiliki wa Chelsea wametumia zaidi ya pauni bilioni 1.5 kwa usajili, wengi wao wakiwa wachezaji vijana ambao wanaweza kuuzwa kwa thamani kubwa siku zijazo.

Lakini mashabiki wanajiuliza ikiwa hii ni moja ya timu kubwa zaidi za Ligi Kuu Uingereza kuwahi kukusanywa. Wachezaji hao ni akina nani?

Pia unaweza kusoma

Nani yupo kwenye kikosi cha Chelsea?

Makipa 8: Filip Jorgensen, 22, alisajiliwa kwa pauni milioni 21, Robert Sanchez, 26, kwa pauni milioni 25, Djordje Petrovic, 24, pauni milioni 14 (anapatikana kwa mkopo), Kepa Arrizabalaga, 29, pauni milioni 72 (anauzwa), Marcus Bettinelli, 32, yuko huru, Mike Penders, 19, pauni milioni 17 (anapatikana kwa mkopo) bado hajathibitishwa, Gabriel Slonina, 20, pauni milioni 9 (anapatikana kwa mkopo), Lucas Bergstrom, 21, haijajuulikana ikiwa anauzwa au wa mkopo.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Walinzi wa nyuma 7: Reece James, mlinzi wa kulia, 24, kutoka chuo cha michezo, Marc Cucurella, mlinzi wa kushoto, 26, amesajiliwa kwa pauni milioni 62, Ben Chilwell, mlinzi wa kushoto, 27, kwa pauni milioni 45, Renato Veiga, mlinzi wa kushoto, 21, kwa pauni milioni 12, Malo Gusto, 21, mlinzi wa kulia, kwa pauni milioni 30, Josh Acheampong, kulia, 18, kutoka chuo cha michezo, Caleb Wiley, kushoto, 19, kwa pauni 9 (anapatikana kwa mkopo).

Walinzi wa kati 9: Axel Disasi, 26, amesajiliwa kwa pauni milioni 39, Wesley Fofana, 23, kwa pauni milioni 75, Levi Colwill, 21, kutoka chuo cha michezo, Tosin Adarabioyo, 26, yuko huru, Benoit Badiashile, 23, kwa pauni milioni 33, Trevoh Chalobah, 25, kutoka chuo cha michezo (anauzwa), Aaron Anselmino, 19, kwa pauni milioni 16 (yupo tayari kwa mkopo), Alfie Gilchrist, 20, kutoka chuo cha michezo (kuondoka kwa mkopo), Bashir Humphreys, 21, kutoka chuo cha michezo, anauzwa au kwa mkopo.

Wachezaji wa kati 15: Enzo Fernandez, 23, amesajiliwa kwa pauni milioni 107, Moises Caicedo, 22, kwa pauni milioni 115, Christopher Nkunku, 26, kwa pauni milioni 52, Omari Kellyman, 19, kwa pauni milioni 19, Cesare Casadei, 21, kwa pauni milioni 17, Lesley Ugochukwu, 20, kwa pauni milioni 23, Kiernan Dewsbury-Hall, 25, kwa pauni milioni 30, Romeo Lavia, 20, kwa pauni milioni 53, Carney Chukwuemeka, 20, kwa pauni milioni 20, Tino Anjorin, 22, kutoka chuo cha michezo na anapatikana kwa mauzo/mkopo), Andrey Santos, 20, puani milioni 18 (anapatikana kwa mkopo), Kendry Paez, 17, kwa pauni milioni 17 (anapatikana kwa mkopo), Alex Matos, 19, yupo huru, Jimi Tauriainen, 20, anapatikana kwa mkopo, Leo Castledine, 18, kutoka chuo cha michezo na anapatikana kwa mkopo.

Wachezaji wa pembeni 9: Mykhailo Mudryk, kushoto, 23, amesajiliwa kwa pauni milioni 89, Raheem Sterling, kushoto, 29, pauni milioni 48, Pedro Neto, kushoto, 24, pauni milioni 54, Cole Palmer, kulia, 22, pauni milioni 43, Noni Madueke, kulia, 22, pauni milioni 29, Estaevo Willian, kulia, 17, pauni milioni 51 (anapatikana kwa mkopo), Angelo Gabriel, kulia, 19, pauni milioni 13 (anaptikana kwa mkopo), Harvey Vale, 20, kutoka chuo cha michezo (anauzwa/mkopo) na Diego Moreira, 20, anapatikana bure.

Washambuliaji 7: Romelu Lukaku, 31, amesajiliwa kwa pauni milioni 100, Nicolas Jackson, 23, milioni 32, David Datro Fofana, 21, pauni milioni 11 (anauzwa), Deivid Washington, 19, pauni 17, Marc Guiu, 18, pauni milioni 5, Mason Burstow, 21, pauni milioni 1.5, (anauzwa/mkopo), Armando Broja, 22, kutoka chuo cha michezo (anauzwa).

Utabiri juu ya kikosi chake cha kwanza

Kikosi cha kwanza cha wachezaji 11: Sanchez; James, Tosin, Colwill, Cucurella; Caicedo, Lavia, Fernandez; Palmer, Nkunku, Neto.

Kikosi cha pili cha wacheza 11: Jorgensen; Gusto, W Fofana, Badiashile, Veiga; Ugochukwu, Dewsbury-Hall, Chukwuemeka; Madueke, Jackson, Sterling.

Wengine wa ziada ni: Mudryk, Kellyman, Disasi, Chalobah na Chilwell.

Je, kuna ukomo wa ukubwa wa kikosi?

Chelsea italazimika kuwasilisha kikosi cha wachezaji 25 baada ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi ambacho ni lazima kiwe na angalau wachezaji wanane 'wa nyumbani' - wale wa taifa lolote ambao wamekaa miaka mitatu katika chuo cha michezo cha klabu yoyote ya Uingereza kabla ya kufikisha umri wa miaka 21.

Lakini pia klabu inaweza kusajili wachezaji wa chini ya miaka 21 kama inavyopenda juu ya kikosi hicho cha wachezaji 25.

Chelsea ilikuwa na kikosi kilichojaa wachezaji zaidi ya 40 chini ya Graham Potter, ripoti ziliibuka kuwa wachezaji walikaa sakafuni wakati wa mikutano ya timu na walibadilisha nguo za mazoezi kwenye korido.

Msimu huu wa joto watafanya uhamisho mdogo. Takribani wachezaji 14 wataondoka kwenye kundi la Chelsea la wachezaji 55 walioorodheshwa hapo juu. Lakini swali litakaloulizwa, kwanini Chelsea inasajili wachezaji wengi vijana? Klabu hiyo inasema, haina umri wa chini au mshahara wakati wa kutafuta wachezaji na huamua ununuzi kwa msingi wa kutazama mchezaji mmoja mmoja.

Wanaamini wanaweza kuwepo katika nafasi ya timu nne bora katika ligi wakiwa na kikosi cha sasa na kuanza kuwinda mataji makubwa katika misimu ijayo.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla