Yafahamu mataifa yanayosherehekea Krismasi leo Januari 7

Leo ni krismasi kwa mataifa kadhaa duniani, yakiadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Mamilioni ya Wakristo wa dhehebu la Orthodox husheherekea Krismasi Januari 7, badala ya Disemba 25, iliyozoeleka na wengi. Unaweza kuiita Krismasi ya Orthodox.
Ni sikukuu inayopewa heshima kubwa kwa baadhi ya mataifa hasa ya magharibi.
Sababu kuu ya tofauti ya tarehe ya Krismasi iko kwenye matumizi ya kalenda tofauti.
Wakristo wa dhehebu la Orthodox hufuata kalenda tofauti na kalenda ya Gregorian ambayo kawaida hutumika katika nchi za Magharibi.
Wanasherehekea Krismasi tarehe 7 Januari, na sherehe zikianza rasmi usiku wa manane katika mkesha wao wa Krismasi.
Julius Caesar alianzisha kalenda katika 46BC kulingana na ushauri wa mwana-astronomia wa Misri Sosigene, ambaye alikuwa amehesabu mwaka wa mwezi.
Lakini vipimo vyake havikuwa sahihi kwa takriban dakika 11, na kwa karne nyingi tarehe za sikukuu kuu za Kikristo zilikuwa zimebadilika sana na ikawa hoja ya mjadala.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ili kurekebisha hili, kalenda ya Gregorian ilianzishwa na Papa Gregory mwaka wa 1582, na hii ndiyo ambayo mataifa ya Magharibi na na maeneo mengi duniani bado yanaitumia leo.
Hispania, Ureno, Ufaransa, Poland, Italia na Luxemburg yalikuwa mataifa ya mwanzo mwanzo kuipitisha.
Nchi zinazosheherekea Krismasi Januari 7
Ukiacha mataifa yaliyotajwa hapo juu, mataifa mengine duniani yanayoshehereklea Krisimasi Januari 7 ni pamoja na;
- Bulgaria
- Belarus
- Egypt
- Ethiopia
- Eritrea
- Georgia
- Israel
- Kazakhstan
- Macedonia
- Moldova
- Montenegro
- Serbia
Zaidi ya tarehe: Mfungo na ibada

Chanzo cha picha, Getty Images
Tofauti ya Krismasi ya Orthodox haiishii kwenye tarehe pekee.
Kwa Waorthodox wengi, Krismasi huja baada ya kipindi cha siku 40 za kufunga, kinachojikita katika sala, tafakari na kujizuia kula vyakula fulani kama nyama na maziwa. Mfungo huu huonekana kama maandalizi ya kiroho kabla ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu.
Sherehe huanza rasmi mkesha wa Krismasi, Januari 6, kwa ibada ndefu na za kipekee kanisani. Ibada hizo mara nyingi huambatana na mishumaa, nyimbo za kale na sala za kitamaduni zilizorithishwa kwa vizazi vingi.
Chakula, familia na mila
Baada ya mfungo kumalizika, familia hukusanyika kusherehekea kwa chakula cha pamoja. Katika baadhi ya jamii, sherehe huanza kwa vyakula vya asili kama kutia chenye mchanganyiko wa nafaka, asali na karanga vinavyoashiria maisha, matumaini na baraka.
Nyumba hupambwa, zawadi hutolewa na jamii huungana kusherehekea, kwa namna inayofanana na Krismasi ya Magharibi, lakini kwa mila na desturi zilizojengwa juu ya historia ndefu ya imani ya Kanisa la Orthodoksi.
Krismasi ile ile, ladha tofauti

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa furaha, mapambo na ujumbe wa upendo vinafanana, Krismasi ya Orthodoksi ina ladha yake ya kipekee yenye misingi ya imani, historia na mtazamo tofauti wa muda.















