Maduro afikishwa mahakamani New York

Washirika wa kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani, ikiwa ni pamoja na China na Iran, wanaitaka Marekani kumwachilia huru.

Muhtasari

Moja kwa moja

Ambia Hirsi & Rashid Abdallah

  1. Wahamiaji 22 wa Ethiopia wafariki katika ajali mbaya ya barabarani

    Ju

    Chanzo cha picha, Facebook

    Mamlaka inasema wahamiaji wasiopungua 22 wameuawa na wengine 65 kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la kaskazini mashariki mwa Afar nchini Ethiopia.

    Takriban wahamiaji 85 wa Ethiopia walikuwa wakisafiri mashariki wakati lori hilo lilipopinduka katika mji wa Semera Jumanne asubuhi, afisa mkuu wa Afar, Mohammed Ali Biedo amesema katika taarifa.

    Bado haijajuulikana walikuwa wanaelekea wapi, lakini njia hiyo kwa kawaida huanzia Ethiopia kupitia Djibouti, kuvuka Bahari ya Shamu hadi Yemen, na kuendelea hadi Saudi Arabia na nchi zingine za Mashariki ya Kati.

    Biedo alisema kwamba 30 kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.

    Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linaelezea safari kutoka Pembe ya Afrika - inayojumuisha Somalia, Djibouti, Ethiopia na Eritrea - hadi Yemen kama "mojawapo ya njia za uhamiaji zenye shughuli nyingi na hatari zaidi".

    Licha ya hatari hizo, zaidi ya wahamiaji 60,000 waliwasili Yemen mwaka wa 2024 pekee, wengi wao wakielekea Saudi Arabia, kulingana na IOM.

  2. Waziri wa mambo ya nje wa Israel ameitembelea Somaliland

    Hj

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli Gideon Saar ameitembelea Somaliland, eneo lililojitenga la Somalia, siku ya Jumanne, vyanzo viwili viliiambia Reuters.

    Ni siku 10 baada ya Israeli kuitambua rasmi Jamhuri ya Somaliland iliyojitangaza kuwa nchi huru.

    Moja ya vyanzo hivyo, afisa mkuu wa Somaliland, alisema Saar alikutana na Rais wa Somaliland Abdirahman Mohamed Abdullahi kujadili njia za kuimarisha uhusiano wa pande mbili.

    Chanzo cha pili kilithibitisha uwepo wa waziri wa Israeli huko Somaliland.

    Wizara ya mambo ya nje ya Israel hakujibu ombi la kutoa maoni kuhusu kama alikuwa Somaliland.

    Israeli iliitambua rasmi Somaliland kama taifa huru Desemba 27, hatua ambayo ilikosolewa na Somalia, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikipinga juhudi za Somaliland za kujitenga.

    Hakuna nchi nyingine ambayo imeitambua rasmi Somaliland.

    Wakati huo, Abdullahi amesema Somaliland itajiunga na Makubaliano ya Abraham , makubaliano yanasimamiwa na utawala wa Trump kutoka mwaka 2020 ambayo yalishuhudia mataifa ya Ghuba, Falme za Kiarabu — mshirika wa karibu wa Somaliland — na Bahrain yakianzisha uhusiano na Israeli.

  3. Kwaheri hadi kesho

  4. Bei ya dhahabu yapanda baada ya Marekani kumkamata Maduro

    l

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Thamani ya Dhahabu imepanda baada ya Marekani kumkamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro huku operesheni hiyo ikiongeza wasiwasi kwa wawekezaji.

    Dhahabu ilikuwa juu kwa takriban 2.4% ikiwa $4,433 (£3,293) kwa aunsi, huku bei ya fedha ikipanda kwa 4.9%, huku pesa zikihamishiwa katika mali zinazoitwa "mahali salama".

    Hisa za ulinzi kote Ulaya pia ziliongezeka kutokana na matukio ya wikendi kwa kutarajia matumizi makubwa zaidi kwa jeshi.

    Bei ya mafuta haijabadilika sana, lakini hisa katika makampuni ya nishati ya Marekani zimepanda kwa matarajio kwamba watapata akiba ya mafuta ya Venezuela.

    Bei za madini ya thamani kama vile dhahabu na fedha mara nyingi hupanda wakati wa kutokuwa na uhakika kwani huonekana kama mali salama zaidi kuhifadhiwa.

    Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kutumia akiba kubwa ya mafuta ya Venezuela baada ya kumkamata Maduro na kusema Marekani "itaendesha nchi hiyo” hadi kumalizika kipindi cha mpito.

    Lakini wachambuzi wa sekta hiyo wamesema hatua hiyo haitakuwa na athari ya haraka kwa kiasi ambacho watu na biashara hulipa kwa ajili ya nishati.

    Wataalamu pia wamesema itagharimu mabilioni ya dola kurekebisha miundombinu ya mafuta ya Venezuela, ambayo imekuwa ikiporomoka tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000.

    Uzalishaji ghafi wa mafuta ya Venezuela unachangia takriban 1% tu ya uzalishaji wa mafuta duniani, amesema mtaalamu wa mikakati ya uwekezaji Vasu Menon kutoka benki ya OCBC.

    Mtendaji mkuu wa zamani wa BP, Lord Browne, amekimbia kipindi cha BBC Today, ili Venezuela ifufue uzalishaji wake wa mafuta itahitaji "uwekezaji mkubwa wa ujuzi."

    Pia unaweza kusoma:

  5. Katika picha: Maduro akisafirishwa kwenda mahakamani New York

    Jjj

    Chanzo cha picha, Reuters

    Gh

    Chanzo cha picha, Reuters

    Jjj

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kj

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kkk

    Chanzo cha picha, Reuters

    Jj

    Chanzo cha picha, Reuters

  6. Maandamano ya Iran yaingia siku ya tisa huku Trump akitishia kuingilia kati

    Y
    Maelezo ya picha, Maandamano huko Sari, kaskazini mwa Iran tarehe 4 Januari 2025

    Wimbi la maandamano yaliyosababishwa na uchumi unaodorora wa Iran limeingia katika siku yake ya tisa, huku Rais Donald Trump akiongeza tena tishio la kuingilia kati.

    Siku ya Jumapili, video zilizochapishwa mtandaoni zilionyesha maandamano huko Tehran, pamoja na majimbo ya Fars, Ilam, Khorasan Kaskazini na Semnan.

    Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema maandamano yamefanyika katika majimbo 26 kati ya 31 nchini tangu wiki iliyopita, na angalau waandamanaji 19 na afisa mmoja wa vikosi vya usalama wameuawa.

    "Tunafuatilia kwa karibu sana. Wakianza kuwaua watu kama walivyofanya hapo awali, nadhani watapigwa vibaya sana na Marekani," Trump aliwaambia waandishi wa habari kwenye Air Force One.

    Siku ya Jumatatu asubuhi, spika wa bunge la Iran alisema "madai halali" ya waandamanaji yanapaswa kusikilizwa na kutumika kama msingi wa mabadiliko.

    Lakini Mohammad Baqer Qalibaf aliongeza kwamba mawakala wowote wa kigeni wanaojaribu kutumia vibaya maandamano hayo "watakabiliwa vyema."

    Matamshi yake yanafanana na yale ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ambaye ametangaza kwamba "waasi wanapaswa kuwekwa mahali pao".

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran pia aliishutumu Israeli kwa kutaka "kudhoofisha umoja wetu wa kitaifa", baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuelezea "mshikamano wa serikali yake na mapambano ya watu wa Iran" siku ya Jumapili.

    Esmail Baqai aliambia mkutano na waandishi wa habari kwamba kauli za Netanyahu na "maafisa fulani wa Marekani wenye msimamo mkali" "zinachochea vurugu tu".

    Iran na Israeli zilipigana vita vya siku 12 mwezi Juni mwaka jana, ambapo ndege za kivita za Israeli na Marekani zilishambulia vituo muhimu vya nyuklia vya Iran kwa mabomu.

    Maandamano ya hivi punde nchini Iran yalianza wakati wafanyabiashara wa maduka walipoingia mitaani mjini Tehran mnamo Desemba 28 kuelezea hasira zao kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu ya Iran dhidi ya dola ya Marekani.

    Rial imeshuka hadi kiwango cha chini kabisa na mfumuko wa bei umeongezeka hadi 40% huku vikwazo dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran vikikandamiza uchumi.

    Wanafunzi wa vyuo vikuu walijiunga na maandamano hayo na wakaanza kusambaa hadi miji mingine.

    Maandamano hayo yamekuwa mengi tangu ghasia za mwaka 2022 zilizosababishwa na kifo cha Mahsa Amini, mwanamke kijana Mkurdi ambaye alikamatwa na polisi wa maadili kwa madai ya kutokuvaa hijab yake ipasavyo.

    Mamia ya watu waliuawa na maelfu kukamatwa katika msako mkali wa vikosi vya usalama.

  7. Maduro afikishwa mahakamani ya New York

    l

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais aliyeondolewa madarakani wa Venezula, Nicolás Maduro ambaye alikamatwa katika operesheni ya Marekani amefikishwa katika mahakama ya New York, Marekani.

    Maduro amefika katika jengo la mahakama ya Manhattan, ambapo orodha kamili ya mashtaka dhidi yake itasomwa leo.

    Maduro anatuhumiwa na Marekani kwa biashara haramu ya dawa za kulevya na makosa yanayohusu silaha, na kuendesha utawala wa "kigaidi wa dawa za kulevya," madai anayokana.

    Mke wa Maduro, Cilia Flores pia naye alikamatwa katika operesheni hiyo na anatuhumiwa kwa rushwa.

    Washirika wa kiongozi aliyeondolewa madarakani, ikiwa ni pamoja na China na Iran, wanaitaka Marekani kumwachilia huru Beijing inasema vitendo vya Washington ni "ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa."

  8. Delcy Rodríguez kuapishwa kuwa rais wa mpito Venezuela

    o

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Makamu wa Rais wa Venezuela na Waziri wa Mafuta Delcy Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari katika Wizara ya Mambo ya Nje huko Caracas, Venezuela Agosti 11, 2025.

    Makamu wa Rais wa Venezuela, Delcy Rodríguez anatarajiwa kuapishwa hivi karibuni kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya Mahakama Kuu kumteua mwishoni mwa wiki kufuatia kukamatwa kwa rais Nicolás Maduro na Marekani.

    Anatarajiwa kuapishwa rasmi katika uzinduzi wa kila mwaka wa Bunge la Kitaifa la nchi hiyo.

    Rodríguez 56 amekuwa makamu wa rais tangu 2018, akihudumu kwanza kama waziri wa fedha na kisha kama waziri wa mafuta.

    Kabla ya hapo alikuwa waziri wa mawasiliano, waziri wa mambo ya nje na mkuu wa bunge linalounga mkono serikali.

    Anafanya kazi kwa karibu na kaka yake, Jorge Rodriguez, ambaye ni mkuu wa Bunge la Kitaifa.

  9. Man Utd kumteua meneja wa muda hadi mwisho wa msimu

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tunasikia kwamba Manchester United wanatarajiwa kumteua kocha wa muda uliosalia wa msimu huu na mtu huyo hatakuwa Darren Fletcher, ambaye atasimamia mechi ijayo dhidi ya Burnley Jumatano.

    United wanapanga kumteua meneja wa kudumu msimu ujao

  10. Waziri wa Ujerumani asema ulinzi wa Greenland utajadiliwa na NATO ikihitajika

    l

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul katika mkutano na waandishi wa habari Beijing, China Desemba 8, 2025.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amesema Greenland ni mali ya Denmark na muungano wa NATO unaweza kujadili kuimarisha ulinzi ikiwa ni lazima.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Wadephul amezungumza hayo Jumatatu akiwa ziarani China baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutoa vitisho vipya vya kuichukua Greenland, kufuatia kumpindua kiongozi wa Venezuela Nicolas Maduro.

    Trump amerudia kusema anataka kuichukua Greenland, azma aliyoitoa kwa mara ya kwanza mwaka 2019 wakati wa muhula wake wa kwanza wa urais.

    Akizungumza na waandishi wa habari huko Lithuania, Wadephul alisema Ujerumani ina maswali kuhusu kuondolewa kwa Maduro na kusisitiza kwamba watu wa Venezuela wanapaswa kuamua mustakabali wa nchi yao katika uchaguzi huru na wa haki, baada ya Trump kusema Marekani itaiendesha nchi hiyo.

    Kuhusu Greenland, Wadephul amesisitiza kuwa ni sehemu ya Denmark.

    "Na kwa kuwa Denmark ni mwanachama wa NATO, Greenland, kimsingi, pia itakuwa chini ya ulinzi wa NATO," amesema.

    "Na ikiwa kuna mahitaji zaidi ya kuimarisha ulinzi kuhusu Greenland, basi tutalazimika kujadili hili ndani ya mfumo wa muungano."

    Hakufafanua zaidi kuhusu aina ya majadiliano hayo.

    Pia unaweza kusoma:

  11. Uganda yapiga marufuku matangazo mubashara ya ghasia

    po

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wafuasi wa mgombea urais wa Uganda Robert Kyagulanyi, anayejulikana pia kama Bobi Wine, wa chama cha National Unity Platform (NUP), katika msafara wake wa kampeni kabla ya uchaguzi mkuu jijini Kampala, Uganda Desemba 15, 2025.

    Serikali ya Uganda imesema siku ya Jumatatu kuwa inapiga marufuku matangazo ya moja kwa moja ya ghasia, "maandamano yasiyo halali" na matukio mengine ya vurugu kabla ya uchaguzi ambapo Rais Yoweri Museveni anataka kuongeza muda wa utawala wake wa miaka 40.

    Serikali imewakamata mamia ya wafuasi wa upinzani kabla ya uchaguzi wa Januari 15, ambapo Museveni mwenye umri wa miaka 81 atapambana na Bobi Wine mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni nyota wa pop aliyegeukia siasa.

    "Kutangaza moja kwa moja au kurusha matangazo ya ghasia, maandamano haramu, au matukio ya vurugu ni marufuku, kwani kunaweza kuzidisha mvutano na kueneza hofu," Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema.

    Serikali mara nyingi huelezea maandamano ya kupinga serikali kama ghasia.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Wizara hiyo pia imepiga marufuku usambazaji wa maudhui yoyote "yanayo chochea chuki au ya vurugu."

    Zaidi ya watu 50 waliuawa kabla ya uchaguzi uliopita mwaka 2021 katika msako mkali uliofanywa na vikosi vya usalama dhidi ya wafuasi wa Wine, waliomtuhumu Museveni kwa kuiba uchaguzi huo, jambo ambalo alilikana.

    Museveni, ambaye aliingia madarakani mwaka 1986 baada ya kuongoza uasi wa miaka mitano, ndiye rais wa tatu kwa kutawala muda mrefu zaidi barani Afrika.

    Wakosoaji na makundi ya haki za binadamu kwa muda mrefu wamekuwa wakivishutumu vikosi vya usalama vya serikali yake kwa kuwatesa na kuwatisha wapinzani ili serikali iendelee kushikilia madaraka, madai ambayo ameyakanusha.

    Kundi la haki za binadamu la Amnesty International lilisema Jumatatu kwamba vikosi vya usalama vya Uganda vimeanzisha "kampeni kali ya ukandamizaji" dhidi ya wafuasi wa Wine katika kipindi cha kuelekea uchaguzi, na kuwatia mbaroni, kuwapiga na kuwatesa kiholela.

    Wasemaji wa serikali na polisi hawakujibu maombi ya kutoa maoni kuhusu taarifa hiyo.

    Mwanachama mwingine mkuu wa upinzani, Kizza Besigye, bado yuko gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kukamatwa kwa mashtaka ya uhaini. Anakana mashtaka hayo.

    Pia unaweza kusoma:

  12. Kumi wapatikana na hatia kumnyanyasa mke wa rais wa Ufaransa kwa kudai alizaliwa mwanaume

    p

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Brigitte Macron, mke wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akisubiri kumpokea Waziri Mkuu wa Kroatia Andrej Plenkovic na mkewe Ana Maslac Plenkovic kwa chakula cha jioni cha kitaifa katika Jumba la Elysee

    Mahakama ya Paris, imewapata na hatia watu kumi kwa unyanyasaji wa mtandaoni wa mke wa rais wa Ufaransa, Brigitte Macron, kwa kusambaza madai ya uongo kwamba yeye ni mwanamke aliyebadili jinsia baada ya kuzaliwa mwanaume, vyombo vya habari vya Ufaransa viliripoti.

    Brigitte na mumewe, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wamekabiliwa na madai ya uwongo mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni huku baadhi wakisema alizaliwa chini ya jina Jean-Michel Trogneux, jina halisi la kaka yake mkubwa.

    Wakiwa na tofauti ya umri wa miaka 24 wanandoa hao wamekumbwa na madai ya uongo ambayo waliyapuuza kwa muda mrefu lakini yameanza kuyashughulikiwa mahakamani.

    Uamuzi wa Jumatatu unatoa msukumo kwa wana ndoa hao kwani pia wanafuatilia kesi maarufu ya kashfa huko Marekani dhidi ya mtangazaji wa podikasti wa mrengo wa kulia Candace Owens, ambaye pia amedai Brigitte alizaliwa akiwa mwanaume.

    Wanaume hao wanane na wanawake wawili walipatikana na hatia ya kutoa maoni mabaya kuhusu jinsia ya Brigitte Macron, hata kulinganisha tofauti ya umri wake na mumewe na "unyanyasaji wa watoto."

    Wamehukumiwa kifungo cha hadi miezi minane jela na vifungu vilivyoghairishwa, vyombo vya habari vya Ufaransa vimeripoti.

    Pia unaweza kusoma:

  13. Manchester United yamfukuza kazi meneja wake Amorim

    cx

    Chanzo cha picha, Reuters

    Manchester United imemfuta kazi kocha mkuu Ruben Amorim 40, klabu hiyo ya Ligi Kuu England imesema siku ya Jumatatu, siku moja baada ya kulazimishwa sare na Leeds United, timu iliyo hatarini kushuka daraja.

    "Huku Manchester United ikiwa katika nafasi ya sita katika Ligi Kuu, uongozi wa klabu umefanya uamuzi bila kusita kwani ni wakati mwafaka kufanya mabadiliko. Hii itaipa timu fursa bora ya kumaliza Ligi Kuu ikiwa kiwango cha juu zaidi," klabu hiyo imesema.

    Manchester United wako nyuma kwa pointi 17 dhidi ya vinara Arsenal, na wameshinda mechi moja tu kati ya tano zilizopita.

    Pia unaweza kusoma:

  14. 'Tunaitaka Greenland': Trump arudia tishio la kulinyakua eneo la Denmark

    L

    Donald Trump amependekeza tena kuichukua Greenland, baada ya kiongozi wa Denmark kumsihi "akomeshe vitisho" kuhusu kisiwa hicho.

    Akizungumza na waandishi wa habari, rais wa Marekani amesema "tunaihitaji Greenland kwa ajili ya usalama wa taifa."

    Trump analitaka eneo la Denmark lenye uhuru wa ndani kuwa sehemu ya Marekani, akilitaja kama eneo la kimkakati kwa madhumuni ya ulinzi na utajiri wa madini.

    Waziri Mkuu wa Greenland, Jens Frederik Nielsen, amesema "inatosha sasa" na kulielezea wazo la Marekani la kukidhibiti kisiwa hicho kuwa ni "matamanio."

    Waziri mkuu wa Denmark alitoa taarifa yake baada ya Katie Miller – mke wa mmoja wa wasaidizi wakuu wa Trump, Stephen Miller - kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii ramani ya Greenland yenye rangi za bendera ya Marekani pamoja na neno "SOON".

    Matamshi kuhusu Greenland yanakuja baada ya operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya Venezuela siku ya Jumamosi, ikimkamata rais wake Nicolás Maduro na mkewe na kuwahamisha hadi New York.

    Hilo limeibua hofu kwamba Marekani inaweza kutumia nguvu ili kupata udhibiti wa Greenland, kisiwa kikubwa katika Aktiki.

    Greenland, ambayo ina idadi ya watu 57,000, inajitawala tangu 1979, ingawa ulinzi na sera za kigeni bado ziko mikononi mwa Denmark.

    Ingawa Wagreenland wengi wanapendelea uhuru kutoka Denmark, kura za maoni zinaonyesha kuna upinzani mkubwa kuwa sehemu ya Marekani.

    Pia unaweza kusoma:

  15. Samaki auzwa kwa dola milioni 3.2 katika mnada Japan

    dx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kiyoshi Kimura, ndiye ambaye kampuni yake imemnunua samaki huyo

    Samaki mkubwa aina ya Jodari (tuna bluefin) ameweka rekodi katika soko la samaki la Toyosu jijini Tokyo Jumatatu asubuhi, kwa kuuzwa kwa yen milioni 510.3 ($3.2m; £2.4m) katika mnada wa kwanza wa soko hilo mwaka huu.

    Samaki huyo wa kilo 243 amenunuliwa na na kampuni ya kuuza chakula ya Kiyomura Corp.

    Kiyoshi Kimura, rais wa kampuni hiyo aliwaambia waandishi wa habari baada ya mnada "alishangazwa na bei hiyo," AFP iliripoti.

    "Nilidhani tungeweza kumnunua kwa bei nafuu kidogo, lakini bei ilipanda," amesema.

    Bw. Kimura alilipa yen milioni 56.5 kununua samaki aina Jodari mwaka 2012 na yen milioni 155 mwaka 2013.

    Mwaka 2019 alinunua samaki mwingine aina hiyo kwa yen milioni 333.6 ($2.1m; £1.6m).

    Mnada wa kwanza katika soko la samaki la Toyosu jijini Tokyo kwa kawaida hushuhudia samaki wakiuzwa kwa bei kubwa.

    Mwaka jana, samaki aina hiyo katika mnada huo alinunuliwa kwa yen milioni 207 na kampuni ya Onodera Group, kampuni nyingine ya chakula. Na kusema samaki huyo ataliwa na wateja katika migahawa yake kote nchini.

    Pia unaweza kusoma:

  16. Ecowas yataka uhuru wa Venezuela uheshimiwe

    ol

    Chanzo cha picha, Getty Images/NIPAH DENNIS/AFP

    Jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi ECOWAS imeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ilivyo nchini Venezuela na kutoa wito wa kujizuia na kuheshimu sheria za kimataifa.

    Katika taarifa iliyotolewa jijini Abuja, Nigeria, ECOWAS inatambua haki ya mataifa kupambana na uhalifu wa kimataifa kama vile ugaidi na biashara ya dawa za kulevya lakini imeonya kwamba juhudi hizo "lazima zifanyike kulingana na kanuni zilizowekwa za sheria za kimataifa."

    Kambi hiyo imeikumbusha jumuiya ya kimataifa kuhusu wajibu wake wa kuheshimu uhuru na mipaka ya chini katika Kifungu cha 2(4) cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

    ECOWAS imesema "inaunga mkono kikamilifu msimamo wa Umoja wa Afrika," na kuhimiza mazungumzo jumuishi miongoni mwa Wavenezuela kama njia ya kutatua mgogoro huo.

    ECOWAS imetoa kauli hii kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na kukamatwa kwa Rais Nicolás Maduro.

    Umoja wa Afrika umeonyesha "wasiwasi mkubwa" kuhusu matukio hayo, ukisisitiza kwamba hali hiyo inatishia amani na usalama wa kimataifa.

    Umoja wa bara la Afrika, "umesisitiza umuhimu wa mazungumzo, utatuzi wa migogoro kwa amani, na heshima kwa mifumo ya kikatiba na kitaasisi, katika roho ya ujirani mwema, ushirikiano, na kuishi kwa amani miongoni mwa mataifa."

    Umoja wa Afrika umesema changamoto za ndani za Venezuela "zinaweza kushughulikiwa kupitia mazungumzo ya kisiasa miongoni mwa Wavenezuela wenyewe."

    Afrika Kusini imehimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano haraka, ikielezea mashambulizi ya Marekani na kumkamata Maduro kama "uvamizi wa kijeshi."

    Wizara ya Mahusiano na Ushirikiano wa Kimataifa ya nchi hiyo imesema vitendo vya Marekani ni ukiukaji dhahiri wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambao unazitaka nchi zote wanachama kujiepusha na matumizi ya nguvu dhidi ya uhuru wa eneo au uhuru wa kisiasa wa taifa lolote.

    Jirani wa Afrika Kusini, Namibia pia amelaani vitendo vya Marekani, akielezea kukamatwa kwa Maduro na mkewe kama ukiukaji wa uhuru wa Venezuela.

    Wizara ya Mahusiano na Biashara ya Kimataifa ya Namibia imesisitiza kwamba uadilifu wa eneo na uhuru wa kisiasa wa mataifa yote lazima uheshimiwe kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa.

    Venezuela, taifa la Amerika Kusini linakabiliwa na miaka mingi ya kutokuwa na utulivu wa kisiasa, ugumu wa kiuchumi, na shinikizo la kimataifa, na kuacha mgawanyiko mkubwa kuhusu njia bora ya kutatua mgogoro huo.

    Pia unaweza kusoma:

  17. Cuba inaomboleza raia wake 32 waliouawa wakimtetea Maduro

    Gari lililoharibiwa katika mashambulizi ya Marekani nchini Venezuela.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Gari lililoharibiwa katika mashambulizi ya Marekani nchini Venezuela.

    Cuba imethibitisha kuwa raia wake 32 waliuawa wakati wa operesheni ya Marekani ya kumkamata Nicolás Maduro.

    Nchi inayoongozwa kikomunisti - ambayo inategemea mafuta ya Venezuela - ilikuwa ikisimamia ulinzi wa Maduro na ina maafisa wake katika jeshi la Venezuela.

    "Kutokana na shambulio la kihalifu lililofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya taifa la Venezuela, (...) Wacuba 32 walipoteza maisha katika mapigano, serikali ya Rais Miguel Díaz-Canel ilisema.

    Siku mbili za maombolezo zimetangazwa huku Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel akisema ni kwa heshima ya "wapiganaji jasiri wa Cuba ambao walivamia magaidi waliovalia sare za kifalme waliomteka nyara na kuwaondoa kinyume cha sheria rais wa Venezuela na mkewe kutoka nchini mwao."

    Alipoulizwa kuhusu uwezo wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Cuba, Donald Trump alisema hakuna haja hatua kama hiyo kwani kuna uwezekano ikaanguka yenyewe.

    Lakini hakupuuza uingiliaji kati kijeshi dhidi ya Colombia, akimtaja rais wake wa mrengo wa kushoto Gustavo Petro kama mlanguzi wa dawa za kulevya na "mtu mgonjwa".

    Petro amekanusha tuhuma hizo, akimwonya Trump kutomkashifu.

    Maduro anatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Marekani leo.

    Soma zaidi:

  18. Waziri Mkuu wa Denmark amuomba Trump kukomesha 'vitisho' dhidi ya Greenland

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Waziri mkuu wa Denmark amemwambia Donald Trump "kukomesha vitisho" vya kuichukua Greenland.

    Mette Frederiksen anasema "vitisho vya Marekani kuichukua Greenland havina msingi wowote", na kuongeza: "Marekani haina haki ya kunyakua taifa lolote kati ya mataifa matatu katika ufalme wa Denmark."

    Kauli yake inajiri baada ya Katie Miller - mke wa mmoja wa wasaidizi wa Trump, Stephen Miller - kuweka mtandaoni ramani ya Greenland yenye rangi za bendera ya Marekani sambamba na neno "SOON" kumaanisa ''HIVI KARIBUNI''.

    Trump amerejelea mara kwa mara uwezekano wa Greenland kuwa sehemu ya Marekani.

    Katika taarifa yake, iliyowekwa kwenye tovuti ya serikali ya Denmark, Frederiksen alisema alikuwa akisema na Marekani "moja kwa moja".

    Alisema Denmark - "na hivyo Greenland" - ilikuwa mwanachama wa Nato na ina dhamana ya usalama ya muungano huo.

    Denmark tayari ilikuwa na makubaliano ya ulinzi na Marekani ambayo yaliipa nafasi ya ufikiaji wa Greenland, alisema, na kuongeza kuwa Denmark imeimarisha uwekezaji usalama katika eneo la Arctic.

    Soma pia:

  19. Tinubu aamuru msako dhidi ya washambuliaji katika Jimbo la Niger

    Majambazi walichoma moto soko la kijiji na kupora bidhaa

    Chanzo cha picha, Zakari Kontagora

    Maelezo ya picha, Majambazi walichoma moto soko la kijiji na kupora bidhaa

    Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria ameviagiza vikosi vya usalama kuwasaka na kuwakamata waliohusika na shambulio la Kasuwan Daji katika jimbo la Niger na kuwafikisha mahakamani mara moja.

    Pia aliagiza kuokolewa kwa haraka kwa waathiriwa wote waliotekwa nyara.

    Maagizo ya rais ya Jumapili yanakuja kufuatia mauaji ya wanakijiji katika Jimbo la Niger.

    Takriban, watu 30 waliuawa katika shambulio hilo na wengi kutekwa nyara.

    Ofisi ya rais ilisema shambulio hilo lilitekelezwa na "magaidi wanaoshukiwa kukimbilia Sokoto na Zamfara baada ya shambulio la anga la Marekani kmkesha wa Krismasi."

    Rais Tinubu alituma rambirambi zake kwa familia za waathiriwa, na pia kwa serikali na watu wa Jimbo la Niger.

    Pia alilaani utekaji nyara wa wanawake na watoto.

    Maelezo zaid:

  20. Trump amuonya kiongozi mpya wa Venezuela, Maduro akitarajiwa kufikishwa mahakamani

    Rais wa Marekani Donald Trump amemuonya kiongozi mpya wa Venezuela Delcy Rodríguez kwamba anaweza "kukabiliwa vikali, pengine kuliko Maduro" ikiwa "hatafanya kilicho sahihi".

    Kauli yake kwa jarida la Marekani la The Atlantic inakujawakati rais wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani Nicolás Maduro akitarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya New York leo Jumatatu.

    Marekani inamshutumu Maduro, ambaye anashtakiwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu wa silaha, kwa kuendesha serikali ya "magaidi wa mihadarati", madai ambayo anayakanusha.

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio amesisitiza kuwa Marekani haiko vitani na Venezuela, baada ya mashambulizi ya anga mjini Caracas siku ya Jumamosi yaliyoishia Maduro na mke wake kuwekwa chini ya ulinzi na kusafirishwa hadi Marekani.

    Baadhi ya wabunge wa chama cha Democratic wanasema operesheni hiyo ni "kitendo cha vita".

    Katika mahojiano na The Atlantic Jumapili, Trump alisema kuhusu Rodríguez: "Ikiwa hatafanya kilicho sahihi, atalipa gharama kubwa sana, pengine kubwa kuliko Maduro."

    Aliongeza kuwa kwa Wavenezuela, "Mabadiliko ya utawala, chochote unachotaka kukiita, ni bora kuliko ulichonacho sasa hivi. Haiwezi kuwa mbaya zaidi".

    Soma zaidi: