Unajua cha kufanya ukikwamwa na mwiba wa samaki kooni?

.

Chanzo cha picha, shutterstock

Maelezo ya picha, Miba ya samaki
Muda wa kusoma: Dakika 3

Kitoweo cha mchuzi wa Samaki ni mlo mzuri sana kwa wale wasiopenda mboga. Kuna aina nyingi ya samaki wanaopatikana, ikiwa ni pamoja na samaki wa baharini na samaki wa maji safi.

Watu wengi wamekuwa wakila samaki kwa madai kwamba wana mafuta kidogo kuliko kondoo na kuku.

Lakini tatizo la samaki ni miiba.

Haijalishi wanataka kula kiasi gani, watu wengi hufikiria mara mbili juu ya kula samaki kwa hofu kwamba watakuwa na miiba.

Ikiwa mwiba mdogo katika kipande cha samaki utapita kooni na kushuka tumboni wakati wa kula, hakuna hatari kubwa.

Hata hivyo, mwiba huo mdogo ukikwama kwenye koo, au mwiba mkubwa ukiingia tumboni na kutoboa matumbo, inaweza kuwa tatizo.

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Shutterstock

Tahadhari ya kula samaki mwenye miba

Katika muktadha huu, unapaswa kufanya nini ili kuepuka mwiba wa samaki kunasa kwenye koo lako? Je, unapaswa kula samaki vipi?

Dkt. Kalyani, daktari wa upasuaji na profesa mkuu katika hospitali ya serikali huko Vijayawada, alizungumza na BBC kuhusu nini cha kufanya ikiwa mwiba utakwama katika koo lako.

"Wakati wa kula samaki ni vyema kuutoa uti wa mgongo kabla ya kumla, sisi madaktari tunapendekeza vivyo hivyo, iwapo mwiba wa samaki umekwama kwenye koo, ufanyike uchunguzi wa endoscope ili kuutoa, ukishuka kwenye koo hupigwa picha ya X-ray ili kuchunguzwa mahali ulipo na kufanyiwa upasuaji wa kuutoa.

Kesi za aina hiyo hazijaripotiwa katika hospitali ya serikali ya Vijayawada siku za hivi karibuni," alisema Dkt Kalyani.

"Ni hatari sana mwiba wa samaki ukikwama kwenye umio, kuna hatari ya kuambukiza kifua kizima, hii inaitwa mediastinitis, ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya kula mchuzi wa samaki ili kuepuka hali hii," alisema.

Je, kuna tiba?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi mfupa wa samaki unapokwama kwenye koo unaweza kuondolewa kirahisi, pia hakuna haja ya kuwa na wasiwasi ukiingia kwenye umio, hii ni kwa sababu asidi ya tumbo inaweza kuyeyusha mfupa huo wa samaki kwa urahisi.

Jampa Mangamma, 54, kutoka Bikkavolu katika wilaya ya Godavari Mashariki, hivi alikula mchuzi wa samaki kabla ya mfupa wa kitoweo hicho kukwama katika koo lake.

Alikwenda katika Hospitali ya Apollo huko Kakinada akiwa na dhiki kubwa, ambapo madaktari walimfanyia vipimo mbalimbali na kugundua kuwa mfupa wa samaki ulikuwa umekwama karibu na moyo wake.

Hata hivyo, upasuaji huo ulifanyika bila kufungua moyo na bila kuathiri mifupa ya kifua.

Madaktari Sivaramakrishna, Nageswara Rao na Vamsi Chaitanya waliofanya upasuaji huo, waliviambia vyombo vya habari kuwa walitoa mfupa wa samaki uliokwama karibu na moyo wa mgonjwa huyo kwa kutumia utaratibu unaoitwa Traver procedure kupitia mrija.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hatua za kuchukua mwiba wa samaki unapokwama kooni

Dkt. Hariharan alitoa mapendekezo.. 'Ikiwa mfupa wa samaki utakwama kwenye koo,

Bonyeza kwa nguvu tumbo. Hii itasaidia mfupa kutoka pamoja na hewa.

"Inasaidia kunywa soda mara kwa mara. Gesi iliyo kwenye soda huweka shinikizo kwenye koo, ambayo husababisha mwiba kutoka," alisema.

Ikiwa tiba hizi za nyumbani hazisaidii, unapaswa kushauriana na daktari mara moja.

Onyo:

"Mara kwa mara, mfupa wa samaki pia unaweza kusababisha maambukizi. Matatizo kama vile maambukizi ya ngozi ya bakteria au osteomyelitis (maambukizi ya mifupa) au septicemia (maambukizi ya damu) .

Lakini haya hutokea tu katika matukio machache," anasema Dk Hariharan.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla