Je, ni kweli Wakristo wanateswa Nigeria kama anavyodai Trump?

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Olaronke Alo
- Nafasi, BBC Global Disinformation Unit
- Author, Chiamaka Enendu
- Nafasi, BBC Global Disinformation Unit
- Author, Ijeoma Ndukwe
- Akiripoti kutoka, Lagos
- Muda wa kusoma: Dakika 8
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia "kuingia" Nigeria na kukomesha "mauaji ya Wakristo" nchini humo.
Kwa miezi kadhaa, wanaharakati na wanasiasa mjini Washington wamekuwa wakidai kwamba wanamgambo wenye itikadi kali za kidni wamekuwa wakiwalenga wakristo nchini Nigeria.
Lakini BBC imegundua kuwa baadhi ya data zinazotegemewa kufikia hitimisho hili ni vigumu kuthibitisha.
Mnamo Septemba, mtangazaji maarufu wa runinga na mcheshi Bill Maher aliangazia kile kilichowakabili waumini wa Kikristo nchini Nigeria kama "mauaji ya halaiki".
Akizungumzia kundi la Boko Haram, alisema "wameua zaidi ya 100,000 tangu 2009, wamechoma makanisa 18,000".
Takwimu kama hizo pia zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Serikali nchini Nigeria imepuuza madai haya ikiyaelezea kama "uwakilishi mbaya wa ukweli"
Serikali hata hivyo haikupinga kwamba kumekuwa na ghasia nchini humo. lakini maafisa walisema kwamba "magaidi wanawashambulia watu wote bila kujali misimamo yao ya kidini - Waislamu, Wakristo na hata wale wasiogemea upande wowote wa kidini".
Makundi mengine yanayofuatilia ghasia nchini Nigeria yanasema idadi ya Wakristo waliouawa ni iko chino, na kuongeza kuwa wathiriwa wakuu wa kundi hilo ni Waislamu.
Mchambuzi wa masuala ya usalama wa Nigeria Christian Ani alisema kuwa ingawa Wakristo walishambuliwa kama sehemu ya mkakati mpana wa kuendeleza ugaidi, ni vigumu kuthibitisha madai kwamba Wakristo walikuwa wakilengwa kimakusudi.
Na Nigeria inakabiliwa na machafuko mbalimbali ya kiusalama kote nchini, sio tu ghasia za makundi ya kijihadi, na haya yana sababu tofauti hivyo haipaswi kuchanganyikiwa.
Watu milioni 220 nchini humo wamegawanyika katika makundi mawili ya kidini na idadi yao inakadiriwa kuwa nusu kwa nusu huku idadi kubwa ya Waislamu wakiwa kaskazini, ambako mashambulizi mengi hufanyika.
Wanasiasa wa Marekani wanasema?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Seneta mashuhuri wa Texas Ted Cruz amekuwa akizungumzia suala hilo kwa muda sasa, akitaja takwimu sawa na zile zilizonukuliwa na Maher tarehe 7 Oktoba, aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba "tangu mwaka 2009, zaidi ya Wakristo 50,000 nchini Nigeria wameuawa na zaidi ya makanisa18,000 na shule 2,000 zinazoendeshwa na mashirika ya Kikristo zimeharibiwa".
Katika barua pepe kwa BBC, afisi yake ilisema wazi kwamba, tofauti na Maher, seneta huyo hakuwa akiita "mauaji ya halaiki" bali anaelezea "mateso" wanayopitia.
Lakini Cruz aliwashutumu maafisa wa Nigeria kwa "kupuuza na kuendekeza mauaji makubwa ya Wakristo yanayofanywa na wanamgambo wa kijihadi". Trump, ameelezea Nigeria kama "nchi iliyofedheheshwa", kwa kutumia maneno sawia na ya Seneta Cruz akisema serikali "inaendelea kuzembea huku mauaji dhidi ya Wakristo yakiendelea".
Serikali ya Nigeria imekanusha hilo, ikisema kuwa inajitahidi kadiri iwezavyo kukabiliana na wanamgambo hao. Maafisa wengine pia wamekaribisha mpango wa Marekani wa kusaidia kupambana na waasi, lakini hatua hiyo isichukuliwe na upande mmoja pekee.
Mamlaka imejitahidi kukabiliana na makundi ya kijihadi yanayoendesha mitandao ya uhalifu - kila wiki kufanya mashambulizi mapya au kuwateka raia.
Boko Haram –waliopata umaarufu kwa Kuwateka nyara wasichana wa Chibok zaid i ya muongo mmoja uliopita - limekuwa likiendesha shughuli zake nchini humo tangu mwaka 2009, hasa katika eneo la kaskazini mashariki, ambalo lina idadi kubwa ya waumini wa dini ya Kiislamu.
Takwimu za vifo vya Wakristo zilizotajwa na baadhi ya watu nchini Marekani ni za kutisha, lakini ni vigumu kutathmini uhalisia wa takwimu hizo.
Takwimu hizo zinatoka wapi?
Linapokuja suala la chanzo cha data, akizungumza kwenye podcast ya BBC mwezi Septemba , Cruz alinukuu ripoti ya 2023 ya Jumuiya ya Kimataifa ya Uhuru wa Kiraia na Utawala wa Sheria (InterSociety) - shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia na kunakili ukiukaji wa haki za binadamu kote nchini Nigeria. Ofisi yake pia iliwasilisha kwa BBC nyaraka kadhaa za makala za mtandaoni kuhusu suala hilo - nyingi wazo ziki nukuu InterSociety.
Maher hakujibu ombi la BBC la kuwasilisha chanzo cha takwimu zake, lakini kutokana na maelezo yaliyotolewa na Cruz, kuna uwezekano mkubwa alikuwa akinukuu ripoti ya InterSociety.
Ukizungumzia data ambayo inaweza kuunda sera ya Marekani kuelekea Nigeria, kazi ya InterSociety haieleweki.
Katika ripoti yake iliyochapishwa mwezi Augusti, ambayo ilikuwa mchanganyiko wa tafiti zilizopita ambazo takwimu zake zinangazia hali ya sasa nchini humo mwaka 2025, ilisema makundi ya kijihadi huko Nigeria yaliwaua takribani Wakristo 100,000 tangu mwaka 2009.
Pia inabainisha kuwa "Waislamu wenye msimamo wa wastani" 60,000 pia waliuawa katika kipindi hicho.
InterSociety haikushiriki orodha maalum ya vyanzo, hivyo kufanya iwe vigumu kuthibitisha jumla ya idadi ya vifo inayoripoti.
Kujibu ukosoaji huu, shirika hilo limesema kuwa "ni haiwezekani kutoa ripoti zetu zote na marejeleo yao yaliyoanzia 2010. Njia yetu rahisi ni kuchukua muhtasari wa takwimu zao na kuziongeza kwenye uvumbuzi wetu mpya au matokeo ili kuunda ripoti zetu mpya." Lakini vyanzo vya data vilivyonukuliwa na InterSociety katika ripoti zake havioneshi takwimu zilizochapishwa.
Pia inasema kuwa watu 60,000 ambao ni ''Waislamu wenye misimamo ya kadr'' walifariki katika kipindi hicho.
InterSociety haikuwasilisha orodha maalum ya vyanzo vyake, hali ambayo inafanya kuwa vigumu kuthibitisha idadi kamili ya vifo inayoripoti.
Kujibu ukosoaji huo, shirika hilo limesema kwamba"ni vigumu kurejelea ripoti zetu kwa kutumia vyanzo vya kutoka mwaka 2019. Njia rahisi ni kuchagua vidokezo vya takwimu zao na kuzijumuisha kwenye tafiti zetu mpya au matokeo ili kuandaa upya ripoti zetu." Lakini vyanzo vya data vilivyonukuliwa na InterSociety katika ripoti zake hazionyeshi takwimu zilizochapishwa.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Vipi kuhusu waliouawa 2025?
Kwa kuangalia vifo vya mwaka huu pekee, InterSociety ilihitimisha kuwa kati ya Januari na Agosti zaidi ya Wakristo 7,000 waliuawa. Hii ni takwimu nyingine ambayo imekuwa ikiangaziwa sana kwenye mitandao ya kijamii, akiwemo Mbunge wa Republican Riley M Moore, ambaye amekuwa sauti inayoongoza katika suala hili katika Baraza la Wawakilishi.
InterSociety inajumuisha orodha ya ripoti 70 za vyombo vya habari kama baadhi ya vyanzo vya utafiti wake kuhusu ya ===mashambulizi dhidi ya Wakristo mwaka wa 2025. Lakini karibu nusu ya matukio haya, hadithi za awali hazikutaja utambulisho wa kidini wa waathirika.
Kwa mfano, InterSociety ilinukuu ripoti ya Al Jazeera ya mashambulizi kaskazini-mashariki mwa Nigeria, ikisema kwamba kulingana na shirika la habari "sio chini ya wakulima 40 hasa Wakristo walitekwa nyara na Boko Haram huko Damboa sehemu ya Jimbo la Borno"
Lakini ripoti ya Al Jazeera haikutaja kwamba wahasiriwa walikuwa "hasa Wakristo", kama ilivyonukuliwa na InterSociety.
InterSociety iliiambia BBC kwamba inafanya uchambuzi zaidi kubaini historia yao, bila kueleza jinsi hasa katika kesi hii, lakini ilitaja ujuzi wao wa wakazi wa eneo hilo na matumizi ya "ripoti za vyombo vya habari vya Kikristo".
Kuongeza idadi ya vifo vinavyoangaziwa katika ripoti hizi zilizotajwa na InterSociety hakusababishi jumla ya 7,000 iliyobainishwa.
BBC ilijumlisha idadi ya vifo kutokana na ripoti hizo 70 na kugundua kuwa jumla ya vifo hivyo ni takribani 3,000. Baadhi ya mashambulizi pia yanaonekana kuripotiwa zaidi ya mara moja.
Ili kuelezea upungufu huo, InterSociety inasema pia inakadiria idadi ya watu ambayo inaamini kuwa wamekufa wakiwa utumwani na inajumuisha ushuhuda wa mashahidi ambao
Chanzo cha mauaji ni nini?
Waliojumuishwa katika orodha yake ya wahalifu ni Makundi ya wapiganaji wenye itikadi kali za kidini kama Boko Haram lakini pia wafugaji wa jamii ya Fulani. Wafulani ni kabila kubwa la Waislamu ambao wanaishi kote Afrika Magharibi na tangu jadi wamejikimu kimaisha kwa kufuga ng'ombe na kondoo.
Kujumuishwa kwa wafugaji wa Fulani, ambao InterSociety inawaelezea kama "wanamgambo wa kijihadi" katika ripoti zake zote, hata hivyo, ni chanzo cha baadhi ya mabishano nchini Nigeria kuhusu jinsi mauaji haya yanapaswa kuainishwa.
Wakati wafugaji wanaelekea kuwa Waislamu, baadhi ya watafiti katika uwanja huu wanapibgn maelezo yanoyotolewa kuhusiana na hili kama mzozo wa kidini, wakisema mara nyingi ni kuhusu upatikanaji wa ardhi na maji.
Wafugaji wa jamii ya Fulani wamezozana na jamii zote mbili za Waislamau na Wakristo kote nchini Nigeria.
Wafugaji wa Fulani wameingia kwenye mzozo na jumuiya za Waislamu na Wakristo kote nchini Nigeria.
Mchanganuzi wa masuala ya usalama Bw Ani anahoji kuwa "kusema kwamba wao ni wanamgambo wa kjihadi - ni jambo la mbali. Haihusiani na hilo. Inahusiana zaidi na wahalifu na wahalifu."
Confidence McHarry, mchambuzi mkuu wa masuala ya usalama katika shirika la Ujasusi linalolenga Afrika SBM, anasema mapigano hayo mara nyingi yanatokana na mivutano ya kikabila na ushindani wa rasilimali.
"Inaweza kuwa ya kikabila kwa asili - wanatafuta kunyakua ardhi, wanatafuta kupanua eneo, lakini kadiri wanavyozihamisha jamii na kadiri wanavyoshambulia vituo vya ibada, ndivyo mambo haya yanavyoelekea kutazamwa kwa njia hiyo."
InterSociety pia inawataja wanaojulikana nchini Nigeria kama majambazi, wakisema wengi wao ni kabila la Fulani kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, ambao wanahusika katika utekaji nyara na wana rekodi ya kuua Wakristo na Waislamu.

Chanzo cha picha, Reuters
Nani amekuwa akifanya kampeni kwenye hili?
Wasiwasi kuhusu vitisho vinavyowakabili Wakristo wa Nigeria imejadiliwa na wanasiasa nchini Marekani na makundi ya kimataifa ya Kikristo kwa muda mrefu.
Katika miaka ya nyuma, imekuzwa nchini Marekani na Wenyeji wa Biafra (Ipob) - kikundi kilichopigwa marufuku nchini Nigeria ambacho kinapigania jimbo lililojitenga katika eneo lenye Wakristo wengi kusini-mashariki.
Intersociety imeshutumiwa na jeshi la Nigeria kwa kuhusishwa na Ipob lakini NGO imekana uhusiano wowote.
Kundi jingine la wanaotaka kujitenga la Biafra pia limedai kuwa na jukumu muhimu katika kukuza simulizi ya "mauaji ya kimbari ya Wakristo" katika Bunge la Marekani.
Serikali ya Jamhuri ya Biafra iliyoko Uhamishoni, BRGIE, ilieleza kuwa ni "juhudi iliyopangwa sana", ikisema kuwa iliajiri makampuni yenye ushawishi na kukutana na maafisa wa Marekani, akiwemo Cruz.
Seneta huyo alikataa kutoa maoni yake.
Mashirika mengine ya utafiti yanasemaje
Takwimu za InterSociety ziku juu kuliko vyanzo vingine vya data kuhusu idadi ya Wakristo waliouawa nchini Nigeria.
Acled, ambayo inafuatilia kwa karibu matukio ya ghasia Afrika Magharibi, imetoa takwimu tofauti. Vyanzo vyayale yaliyochapishwa vinaweza kufuatiliwa na kuchakatwa kwa urahisi.
Mchambuzi wake mkuu, Ladd Stewart, hakuzungumzia moja kwa moja ripoti za InterSociety lakini aliiambia BBC kwamba idadi ya vifo 100,000, iliyotajwa kwenye mitandao ya kijamii, itajumuisha vitendo vyote vya unyanyasaji wa kisiasa nchini Nigeria, na hivyo haitakuwa kweli kusema hii ni idadi ya Wakristo ambao wameuawa tangu 2009.
Acled imegundua kuwa chini ya raia 53,000 - Waislamu na Wakristo - wameripotiwa kuuawa katika ghasia za kisiasa zilizolengwa tangu 2009.
Ukiangalia kipindi cha kuanzia 2020 hadi Septemba 2025, Acled inasema kuwa takriban raia 21,000 waliuawa katika utekaji nyara, mashambulizi, ukatili wa kijinsia na matumizi ya vilipuzi.
Ilibainisha matukio 384 ambapo Wakristo walilengwa hasa kutoka mwaka 2020 hadi Septemba 2025, ambapo watu 317 walikufa, ikiashiria kuwa ni sehemu ndogo tu ya waliouawa.
Kuhusu vyanzo vyake, Acled inategemea vyombo vya habari vya jadi, mitandao ya kijamii ambapo ripoti zinaweza kuthibitishwa, makundi ya kutetea haki na washirika wa ndani.
Vipi kuhusu takwimu zilizotolewa na Trump?
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social Ijumaa iliyopita, Trump alisema Wakristo 3,100 waliouawa. Alikuwa akizungumzia ripoti ya Open Doors inayoangazia vifo vya miezi 12 kuanzia Oktoba 2023, afisa wa Ikulu alisema.
Open Doors ni shirika la misaada linalotafiti kuhusu madhila yanayowakabili -- Wakristo kote duniani.
Katika ripoti yake inasema kwamba ingawa Wakristo 3,100 walifariki, Waislamu 2,320 pia waliuawa katika kipindi hicho cha miezi 12.
Open Doors pia inajumuisha kile inachokiita "Makundi ya kigaidi ya Fulani" katika orodha yake ya wahalifu na inasema walihusika takribani theluthi moja ya Wakristo waliouawa katika miezi hiyo 12.
Frans Veerman, mtafiti mwandamizi mwenzake katika Open Doors, alisema "tunachokiona sasa ni kwamba Wakristo bado wanalengwa, lakini inaongeza kuwa baadhi ya Waislamu wanalengwa na wapiganaji wa Fulani"
Wachambuzi wanasema kuna mashambulizi mengi ya kikatili dhidi ya misikiti na jamii za Kiislamu kaskazini-magharibi mwa nchi.
"Mtu anaweza kusema kwamba hii ni sehemu ya ukosefu wa usalama," alisema Bw McHarry. "Mauaji haya hayaonekani kuwa na mwelekeo wa kidini kwasababu utambulisho wa watu wanaofanya mashambulizi haya dhidi ya Waislamu wenyewe ni Waislamu."












