Greenland na Mfereji wa Panama haziuzwi. Kwa nini Trump anatishia kuzinyakua?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais mteule Donald Trump
Muda wa kusoma: Dakika 3

Rais mteule Donald Trump alisema kwenye jukwaa la kuitenga Marekani kutokana na migogoro ya kigeni kama vile vita vya Ukraine, kuongeza ushuru kwa washirika wa biashara ya nje, na kujenga upya viwanda vya ndani.

Lakini katika siku za hivi majuzi amependekeza mbinu ya uchokozi zaidi kwa sera yake ya mambo ya kigeni.

Mwanzoni, alitania kuhusu Canada kuwa jimbo la ziada la Marekani. Tangu wakati huo, ametishia kutwaa tena udhibiti wa Mfereji wa Panama. Pia alisisitiza hamu kutoka kwa muhula wake wa kwanza wa kumiliki eneo linalojitegemea la Denmark la Greenland, ambalo haliuzwi.

Kuna uwezekano kwamba Marekani itadhibiti eneo lolote kati ya haya. Lakini kauli hizi zinaweza kuashiria kwamba maono ya Trump ya "Marekani Kwanza" ni pamoja na kunyoosha misuli ya nguvu kubwa nje ya mipaka yake kwa ajili ya biashara ya Marekani na maslahi ya usalama wa taifa.

Siku ya Jumapili, Trump aliambia mkutano wa kihafidhina huko Arizona kwamba Panama ilikuwa inatoza meli za Marekani ada "za ujinga, zisizo za haki" kutumia mfereji wake wa majina.

Baada ya kuchukua jukumu la kujenga mfereji huo mwanzoni mwa karne ya 20, Marekani iligeuza udhibiti kamili kwa Panama katika miaka ya 1970 kupitia mkataba. Lakini wiki hii, Trump alisema kwamba ikiwa "unyanyasaji huo" hautakoma, angetaka mfereji huo urudishwe kwa Marekani - ingawa hakufafanua jinsi gani.

Trump aliongeza kuwa hataki Mfereji wa Panama "uanguke katika mikono isiyofaa" na akataja haswa China, ambayo ina masilahi makubwa katika njia hiyo ya maji.

"Kuna nia ya kweli ya usalama wa taifa wa Marekani... katika kudhibiti kutoegemea upande wowote," Will Freeman, Msomi kuhusu masuala ya Amerika Kusini katika Baraza la Mahusiano ya Kigeni, alisema kuhusu matamshi ya Trump.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Tamko la Trump linahusu hilo."

China ni mtumiaji wa pili kwa ukubwa wa Mfereji wa Panama baada ya Marekani, kulingana na data. Ina uwekezaji mkubwa wa kiuchumi nchini pia.

Mnamo 2017, Panama ilikata uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan na kuitambua kama sehemu ya Uchina, ushindi mkubwa kwa Beijing.

Mfereji wa Panama sio tu muhimu kwa biashara ya Marekani katika eneo la Pasifiki, Bw Freeman alisema - ikiwa kuna mzozo wowote wa kijeshi na Uchina, itahitajika kuhamisha meli za Marekani na mali zingine.

Pia alibainisha maoni ya mara kwa mara ya Trump kuhusu kutotendewa haki kwa washirika wa kibiashara wa Marekani, pamoja na ahadi ya rais mteule ya kuongeza kwa kasi ushuru wa forodha kwa bidhaa za kigeni, hasa zile kutoka China.

Malalamiko ya Trump kuhusu ada za meli yalionekana kuakisi maoni yake kuhusu biashara, Bw Freeman alisema.

Ingawa matamshi hayo yanaweza kuwa "ya kulazimisha", alisema Bw Freeman, bado haijaonekana "ikiwa mamlaka ya mifereji huo itapunguza ada kwa mizigo ya Marekani ili kukabiliana na tishio".

Rais wa Panama José Raúl Mulino ametoa taarifa akisema kuwa mfereji huo na eneo jirani ni mali ya nchi yake - na itasalia kuwa hivyo.

Trump aimezea mate Greenland

Mwishoni mwa juma, Trump alisema katika chapisho la mtandao wa kijamii kwamba Marekani "inahisi kwamba umiliki na udhibiti wa Greenland ni jambo la lazima kabisa" kwa sababu za usalama wa taifa na uhuru wa kimataifa.

Marekani inamiliki kituo cha kijeshi cha Pituffik Space Base huko Greenland. Eneo hilo lina utajiri wa maliasili, ikiwa ni pamoja na madini na mafuta adimu duniani, na ni eneo la kimkakati la biashara huku mataifa yenye nguvu duniani yakijaribu kupanua ufikiaji wao katika Arctic Circle.

Urusi, haswa, inaona eneo hilo kama fursa ya kimkakati.

Trump aliwasilisha wazo la kununua Greenland mnamo 2019, wakati wa muhula wake wa kwanza kama rais, na halijafanikiwa.

Waziri mkuu wa Greenland, Múte B Egede, alijibu maoni ya hivi punde ya Trump wiki hii: "Hatuuzwi na hatutauzwa."

Bado, Trump aliendelea kusisitiza taarifa zake za umma mtandaoni.

Katika mtandao wa kijamii wa Truth Social, akaunti ya Trump ilionyesha picha ya bendera ya Marekani ikiwa imepandikizwa katikati ya Mfereji wa Panama.

Mwanawe wa pili wa kiume, Eric Trump, alichapisha picha kwenye X iliyoonyesha Marekani ikiongeza Greenland, Mfereji wa Panama na Canada kwenye toroli ya ununuzi ya mtandaoni ya Amazon.

Kwa Trump, ahadi za kutumia uwezo wa Marekani kwa manufaa yake zilisaidia kuendeleza kampeni zake mbili za urais zilizofanikiwa.

Ilikuwa ni mbinu aliyotumia wakati wa urais wake wa kwanza, kutishia ushuru na kutumwa kwa "askari wenye silaha" kuiongoza Mexico katika kuimarisha utekelezaji kwenye mpaka wake wa Marekani.

Kuelekea muhula wake wa pili, Trump anaweza kutumia kitabu kama hicho mara tu atakapoingia madarakani tarehe 20 Januari.

Wakati inabakia kuonekana nini kitatokea, Denmark imeonyesha nia ya kufanya kazi na utawala wake.

Pia ilitangaza ongezeko kubwa la matumizi ya ulinzi kwa Greenland, saa chache baada ya Trump kurudia hamu yake ya kulinunua eneo hilo la Arctic.

Imetafsiriwa na Seif Abdalla