Ununuzi wa Greenland: Trump avunja safari ya kuelekea Denmark

Greenland ni eneo la Denmark linalojitawala kati ya bahari ya kaskazini ya Atlantic na ile ya Arctic

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Greenland ni eneo la Denmark linalojitawala kati ya bahari ya kaskazini ya Atlantic na ile ya Arctic
Muda wa kusoma: Dakika 3

Rais wa Marekani Donald Trump amefutilia mbali ziara yake rasmi nchini Denmark baada ya waziri mkuu wa taifa hilo kusema kwamba Greenland haitauziwa Marekani.

Rais huyo alitarajiwa kuzuru taifa hilo Septemba 2 kufuatia mwaliko wa malkia wa taifa hilo Margrethe II

Na wiki iliopita bwana Trump alipendekeza kwamba Marekani ilikuwa na hamu kukinunua kisiwa cha Greenland , Jimbo la Denmark linalojitawala.

Waziri mkuu wa Denmark Mette Frederiksen alitaja mpango huo kwamba ni upuzi na kusema kwamba alitumai bwana Trump hakulichukulia swala hilo na uzito mkubwa.

Akitangaza kuvunja safari yake bwana Trump alituma ujumbe wa twitter akisema: Denmark ni taifa maalum lenye watu wazuri sana lakini kutokana na matamshi ya waziri mkuu Mette Frederiksen kwamba hatakuwa na hamu ya kuzumngumzia ununuzi wa Greenland , nitaahirisha mkutano wangu uliopangwa wiki mbili zijazo kwa muda mwengine.

Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse alithibitisha kwamba ziara hiyo ya rais imefutiliwa mbali.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Rais huyo awali alikuwa amethibitisha ripoti kwamba alikuwa na hamu ya kununua kisiwa hucho cha Greenland.

Alipoulizwa siku ya Jumapili iwapo anaweza kuuza ardhi ya Marekani ili kununua kisiwa kwengineko , alisema ...Kweli vitu vingi vinaweza kufanyika.

Maafisa katika kisiwa hicho cha Greenland wamesisitiza kwamba kisiwa hicho hakiko katika soko.

''Greenland ina utajiri wa madini, maji safi zaidi na barafu, samaki, chakula cha baharini kawi na ni kivutio kikuu cha utalii. Tuko wazi kwa biashara lakini sio kuuzwa'', ilisema wizara ya kigeni katika taarifa yake iliotumwa katika mitandao ya kijamii.

Waziri mkuu wa Greenland Kim Kielsen alirejelea matamshi yake katika taarifa nyengine tofauti .

''Greenland haiuzwi lakini iko wazi kibiashara na ushirikiano na mataifa mengine'', ilisema taarifa.

Mbunge wa Greenland Aaja Chemnitz Larsen pia alikuwa miongoni mwa wale waliopinga hamu hiyo ya rais wa Marekani.

''Hapana ahsante kwa bwana Trump kununua Greenland'' , aliandika katika mtandao wa Twitter, akiongezea ''ushirikiano wa usawa kati ya Marekani na Greenland ndio suluhu pekee''.

Poul Krarup muhariri mkuu wa gazeti la Sermitsiaq aliambia BBC hakuamini matamshi ya bwana Trump. ''Greenland ni sehemu ilio huru katika ufalme wa Denmark na inahitaji kuheshimiwa'', alisema.

Lakini alisema kwamba alidhani kwamba ndoto ya Bwana Trump haiwezi kuafikiwa.

''Tungependa kushirikiana na Marekani , bila shaka lakini sisi tuko huru na tunaamua marafiki zetu ni akina nani

Je Greenland iko wapi?

Greenland ndio kisiwa kikubwa zaidi duniani baada ya Australia ambayo inajulikana kama bara.

Ramani ya Greenland
Presentational white space

Kisiwa hicho kina takriban watu 56,000 walio na makaazi yao katika pwani yake. Takriban asilimia 90 ni raia wa Greenland . Ina serikali yake na bunge lake.

Asilimia 80 ya kisiwa hicho imefunikwa na barafu ambayo inahofiwa kuyeyuka kutokana na viwango vya joto duniani.

Kuyeyuka kwa barafu hiyo kumesaidia katika utafutaji wa madini katika ardhi ya kisiwa hicho.

Lakini inaaminika kwamba kuyeyuka kwa barafu hiyo kunaweza kusababisha madhara yanayotokana na mabaki ya kinyuklia yaliowachwa katika kambi kadhaa za jeshi la Marekani wakati wa vita baridi.

Kwa nini kisiwa hicho kinamvutia Trump?

Bwana Trump ameripotiwa kuvutiwa na kisiwa hicho kutokana na madini yake kama vile mkaa, Zinc, Shaba na Chuma.

Lakini huku Greenland ikiwa na utajiri wa mali asli, inategemea Denmark kwa thuluthi mbili za mapato yake .

Ina viwango vya juu vya watu kujitoa uhai, ulevi wa pombe na ukosefu wa ajira.

Bwana Trump alithibitisha ripoti kwamba alikuwa na hamu ya kukinunua kisiwa hicho

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bwana Trump alithibitisha ripoti kwamba alikuwa na hamu ya kukinunua kisiwa hicho

Marekani imekuwa ikikiona kisiwa hicho kama eneo muhimu la kimkakati na liliweka kambi ya wanahewa wake mbali na rada yake wakati wa vita baridi

Mbunge wa Republican Mike Gallagher alitaja wazo hilo la Trump kama la kisiasa.

''Marekani ina hamu ya kukimiliki kisiwa cha Greenland na hilo lazima lisemwe'', alituma ujumbe wake katika mtandao wa Twitter.

Je Marekani imewahi kutaka kununua kisiwa vya Greenland?

Wazo la kuinunua Greenland kwa mara ya kwanza liliwasilishwa 1860 chini ya urais wa Andrew Johnson.

Mwaka 1867 ripoti ya idara ya kigeni ilipendekeza kwamba eneo la kimkakati la Greenland pamoja na mali yake asli ni muhimu kulinunua.

Lakini hakuna hatua rasmi iliochukuliwa hadi 1946 , wakati Harry Truman aliipatia Denmark $100m kununua eneo hilo.

Alikuwa amewasilisha mpango wa kutaka kubadilishana ardhi ya Alaska na Greenland kulingana na AP.