Turkana: Eneo lililo na utajiri mkubwa wa kihistoria na utamaduni

Turkana ni eneo ambalo mabaki ya kale ya kijana mwenye umri wa miaka 15 anayeaminika kuwa miongoni mwa binadamu wa kwanza yalipatikana.

Turkana
Maelezo ya picha, Shanga ni miongni mwa utamaduni ulioonyeshwa katika tamasha maarufu linalojulikana kama Kiturkana Tubong’ulore ikimaanisha, ‘karibu nyumbani.’ Zaidi ya watu 10,000, kutoka jamii na tabaka mbalimbali wamejumuika pamoja kwa lengo la kuimarisha utalii, kustawisha maendeleo ya ukanda huu na kudumisha amani miongoni mwa jamiii hasimu.
Sherehe hii husaidia kudumisha Amani.
Maelezo ya picha, Sherehe hii husaidia kudumisha Amani. Turkana, ni miongoni mwa jamii chache nchini Kenya ambazo zimeweza kuhifadhi mila na tadamuni zao.
wafugaji
Maelezo ya picha, Jamii za hapa ni wafugaji na hutegemea mifugo kama kitega uchumi. Hata hivyo mifugo hao wamekuwa chanzo cha uhasama mkubwa baina ya Jamii tofauti nchini Kenya, Uganda, Ethiopia na Sudan kusini. Uraibu hatari wa wizi wa mifugo umeshamiri hapa.
harusi
Maelezo ya picha, Mitindo ya mavazi na vyakula, vinavyoonyesha jinsi jamii hii inavyoenzi na kukuza utamaduni wao.
sherehe hizi huwapa matumaini ya ushirikiano mwema na amani ya kudumu itakayo wasaidia kukuza utamaduni wao na kuwasaidia kimaendelo
Maelezo ya picha, sherehe hizi huwapa matumaini ya ushirikiano mwema na amani ya kudumu itakayo wasaidia kukuza utamaduni wao na kuwasaidia kimaendelo
Viatu
Maelezo ya picha, Hali ya kila mara ya ukame ambayo pia husababisha njaa na ukosefu wa maji kwa binadamu na mifugo.
Hii inatokana na hali ya kila mara ya ukame ambayo pia husababisha njaa na ukosefu wa maji kwa binadamu na mifugo.
Maelezo ya picha, Licha ya utamaduni wake, eneo hili ni miongoni mwa maeneo maskini zaidi nchini Kenya.