Mtandao wa Facebook waanzisha programu itakayolinda uingiliwaji wa data zako

Muasisi wa Facebook Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza akiahidi kutoa pragramu mpya ya udhibiti wa data za watumia katika mkutano mwaka 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muasisi wa Facebook Mark Zuckerberg kwa mara ya kwanza akiahidi kutoa pragramu mpya ya udhibiti wa data za watumia katika mkutano mwaka 2018

Facebook inafichua ni data gani inazozikusana kutoka kwa watumiaji wake

Wengi, wengi hawapendi wanachokiona .

Programu iliyowekwa na Facebook inayoitwa Off-Facebook Activity...yaani Jje ya shughuli za facebook, itaonyesha programu zote na mitandao inayotuma taarifa kukuhusu wewe kwenye Facebook, ambazo hatimae hutumiwa kulenga matangazo kwa ubora zaidi.

Programu hiyo mpya itakuwezesha kuwa na uwezo wa kufuta historia yako na kuzuwia tabia ya mtandao huo kuingiliwa tena .Lakini mtaalamu mmoja anasema hatua hiyo huenda isiwe na athari kubwa katika faida ya kampuni ya facebook.

Kwa sasa , mpango huo unaendelea taratibu huku Ireland, Korea Kusini na uhispania zikipata huduma hiyo. Lakini lengo ni hatimae kuitoa huduma hii kote duniani.

Utoaji wa huduma hii unakuja wakati Apple na Mozilla tayari wamekwishachukua hatua za kuizuwia Facebook na huduma nyingine za mtandao kuwachunguza watumiaji kupitia mtandao mmoja wa hadi mwingine kwa njia ya kurambaza.

Programu hii itawawezesha watumiaji kutambua ni watu gani wengine au programu zipi zinazotumia data zako katika facebook

Chanzo cha picha, Facebook

Maelezo ya picha, Programu hii itawawezesha watumiaji kutambua ni watu gani wengine au programu zipi zinazotumia data zako katika facebook

Zaidi ya hayo , wasimamizi wa ushindani nchini Ujerumanji walikuwa wameiambia Facebook kuwa inapaswa kuweka ukomo wa namna ilivyokusanya na kujumuisha data zake juu ya ya watumiaji wa mtandao wake la sivyo itatakiwa kujibu juu ya hofu za watumiaji kuliko ilivyofanya awali.

Maslahi shirikishi

Facebook hukusanya data zaidi ya zile zilizopo kwenye ukurasa wako kwasababu labda umeamua kutumia mtandao wa kijamii lkuingia katika Facebook au kuoingia katika programu(app), au hata kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua data zako kwasababu mtandao hutumia kitu kinachoitwa Facebook Pixel kufuatilia shughuli zako mtandaoni.

Hii ndio sababu unapo ramabaza mtandao pengine ukitaka kununua bidhaa kama viatu , utabaini kuwa kuna tangazo la kibiashara linachungulia ghafla kwenye ukurasa wako wa Facebook na baadae utaona ujumbe pengine kama baada ya nusu saa hivi ukipendekeza viatu unavyoweza kuvinunua ambavyo umekuwa ukivisaka kwenye mtandao wako wa facebook.

Mtu akitumia simu yake kufikia mtandano wa Facebook

Kuanzishwa kwa programu ya Off-Facebook Activity itakusaidia kufichua kikamilifu ni data gani au kurasa gani za mtandao zinashirikisha taarifa kukuhusu - Facebook inasema simu ya kawaida ya smartphone ina programu 80 na 40 kati hizo hutumiwa na huenda wanaweza kuwa zaidi.

Utaweza sasa kukata mawasiliano ya data zako na utambulisho wako wa Facebook - ima kwa kampuni au kwa vyanzo binafsi vinavyokusaka. Ikiwa utatumia fursa hii , itamaanisha kuwa yale matangazo ya viatu yataacha kujitokeza katika simu yako wakati wote .

Ni muhimu kusisitiza kwamba Facebook bado itakuwa inakusanya data, lakini kutakuwa hakuna utambulisho - wanaweza kujua kuwa watu wengi wamekuwa wakitafuta bidhaa fulanu , lakini hawatajua kuwa wewe ulikuw amiongoni mwao.

Off-Facebook Activity imekuwepo zaidi ya mwaka mmoja na utekelezaji wake unatokana na ahadi aliyoitoa Mark Zuckerberg katika kikao cha mwaka jana ambapo aliahidi kuwapatia watumiaji wa mtandao wa Facebook udhibiti mkubwa wa namna taarifa(data) zao zinavyotumiwa.