Kwa nini mapinduzi ya Benin yalifeli wakati mengine yalifanikiwa Afrika Magharibi?

A vendor arranges his newspaper display in Benin a day after the attempted coup. "Patrice Talon reassures the country", reads the headline on one.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    • Author, Paul Melly
    • Nafasi, West Africa analyst
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Kama jaribio la mapinduzi nchini Benin lingefanikiwa wiki iliyopita, lingekuwa jaribio la tisa kufanikiwa katika ukanda wa afrika Magharibi ndani ya kipindi cha miaka mitano pekee.

Siku chache tu baada ya wanajeshi kuchukua madaraka nchini Guinea-Bissau wakati shuhguli za kuhesabu kura za uchaguzi wa rais ikiendelea, viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas) waliamua haraka kwamba jaribio la kupindua serikali ya Rais Patrice Talon nchini Benin lilikuwa hatua ya ziada ya kuiingiza kanda hiyo katika machafuko zaidi.

Kwa kuiunga mkono serikali ya Benin, ndege za kivita za Nigeria zilishambulia wanajeshi waasi katika kituo cha televisheni na redio ya taifa, na katika kambi ya jeshi iliyo karibu na uwanja wa ndege mkubwa wa Cotonou.

Ecowas pia ilitangaza kupeleka majeshi ya nchi kavu kutoka Ghana, Nigeria, Ivory Coast na Sierra Leone ili kuimarisha ulinzi wa utawala wa kikatiba.

Hii ni kanda ambayo imetikiswa na misururu ya mapinduzi tangu 2020, na ambayo miezi 10 tu iliyopita ilishuhudia tawala za kijeshi za Mali, Burkina Faso na Niger zikitangaza kujiondoa kabisa kutoka ECOWAS jumuiya ambayo wenyewe walikuwa waanzilishi miaka 50 iliyopita.

Hivyo, kwa kukabiliwa na uwezekano wa serikali nyingine ya kiraia kupinduliwa na wanajeshi waasi, marais wa nchi wanachama wa Ecowas walihitimisha haraka kwamba jaribio la mapinduzi la Cotonou lazima lizuiliwe.

Kujifunza kutokana na makosa yaliyopita

Baada ya wanajeshi waasi mapema asubuhi kushambulia makazi na ofisi ya Talon, wanajeshi watiifu tayari walidhibiti mji mkuu na kuzingira makazi ya serikali.

Hata hivyo, wanajeshi wa mapinduzi waliokuwa wanakabiliana bado walikataa kushindwa, wakiwa tayari kutumia nguvu hata kama itadhuru raia.

Kujibu hali hiyo, Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, aliruhusu mashambulizi ya anga, na siku hiyo hiyo ECOWAS ilituma wanajeshi wa ardhini kusaidia.

Rais wa Ghana, John Mahama, naye alituma wanajeshi wake, licha ya kuwa kiongozi wa nchi yenye demokrasia thabiti, lakini alikuwa na uhusiano mzuri na serikali za kijeshi za Sahel.

Hii ilionyesha kuwa ECOWAS imejifunza kutokana na mapinduzi ya 2023 Niger, ambapo jaribio la kuokoa rais asipinduliwe lilishindikana kwa sababu walikuwa hawajakusudia wala kuchukua hatua ya kuingilia mapema.

Mara hii nchini Benin, Talon bado alikuwa na udhibiti kamili, hivyo aliweza kuomba msaada wa kibiashara kutoka nchi wenzake wa kanda. Hali hii pia ilionekana kuwa na msaada kwa raia wa Cotonou.

Benin soldiers dressed in army uniform appearing on national tv to announce suspension of the country’s constitution.

Chanzo cha picha, BTV

Maelezo ya picha, Wengi wa wanajeshi waliokuwa kwenye televisheni ya taifa mapema Jumapili wamekimbia mafichoni

Ingawa malalamiko dhidi ya Talon yaliyoonyeshwa kwenye televisheni na waliotaka kujaribu kufanya mapinduzi yameelezwa kwa kiasi kikubwa, hakukuwa na ishara yoyote ya msaada wa umma katika jaribio lao la kutaka kuiondoa serikali kwa nguvu.

Hivyo Benin iliwakilisha muktadha unaofaa kwa uingiliaji wa nguvu wa ECOWAS kulinda utawala wa kiraia chini ya katiba.

Wapanga mapinduzi wanaweza kuwa walengwa wa hasira inayoongezeka ya umma wakati taarifa za vifo zinaposambaa. Angalau raia mmoja ambaye ni mke wa mshauri mkuu wa kijeshi wa Talon – aliuawa.

Siku za hivi karibuni, maafisa wakuu wawili wa kijeshi waliokuwa wamekamatwa wakati wa jaribio la mapinduzi la Jumapili wameokolewa, lakini nguvu za usalama bado zinamtafuta kiongozi wa mapinduzi Luteni Kanali Pascal Tigri na wapanga mapinduzi wengine.

Malalamiko yaliyotokota

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hili lilikuwa jaribio jipya tu kati ya mfululizo wa majaribio kadhaa ya mapinduzi katika eneo hilo, ingawa mengine mengi yamefanikiwa.

Yote yamejitokeza katika muktadha wa udhaifu na yanazidi kuongezeka Afrika Magharibi.

Kuna kukata tamaa kwa viongozi wa kisiasa. Hata ambapo uchumi unakua, kuna uhaba mkubwa wa ajira katika eneo hilo.

Hata hivyo, ingawa muktadha wa kanda unashirikishwa sana, sababu zinazosababisha mapinduzi mara nyingi ni za ndani na ni za kipekee kwa kila nchi.

Ukosefu wa msaada wa umma kwa wawaliojaribu mapinduzi ya Cotonou unapingana kabisa na hali katika mitaa ya Conakry, mji mkuu wa Guinea, Septemba 2021, wakati kamanda wa vikosi maalumu, Col Mamady Doumbouya aliongoza kuangusha utawala wa Rais wa wakati huo Alpha Condé.

Kama Talon, Condé alikuwa amechaguliwa kidemokrasia awali lakini baadaye alihakikisha uchaguzi mpya katika mazingira yasiyo ya wazi, na alisimamia kupungua kwa uhuru wa kisiasa. Hata hivyo, Condé alikuwa amesimamia ukandamizaji mkubwa zaidi kuliko Benin.

Condé alikuwa ameshinda muhula wake wa tatu akiwa na umri wa miaka 83, huku Talon mwenye umri wa miaka 67 ameahidi kuondoka madarakani Aprili mwakani, ingawa amebadilisha kanuni za uchaguzi ili karibu kuhakikisha ushindi rahisi kwa mrithi wake, Waziri wa Fedha Romuald Wadagni.

Tofauti nyingine muhimu ni rekodi ya uchumi ya Condé iliyoibua hasara kubwa, huku Talon akisimamia ukuaji imara na huduma bora.

Wwimbi la mapinduzi katika nchi za Sahel katika miaka ya hivi karibuni pia lilisababishwa na mazinfgira ya ndani.

Nchini Mali na Burkina Faso, makamanda wa kijeshi walikuwa wamechoshwa na uongozi dhaifu wa marais waliyochaguliwa katika kampeni dhidi ya waasi wa Kiislamu. Katika nchi zote mbili, serikali zao za kiraia zilionekana kutoweza kusambaza silaha za ziada au hata chakula wanachohitaji wanajesh kukabiliana na waasi.

Kulikuwa pia na chuki kubwa kwa kushindwa kwa Ufaransa kuwadhibiti wanmgambo wa jihadi, licha ya silaha za kisasa zilizokuwa mikononi mwa wanajeshi wake waliokuwa wamesambazwa katika kanda ya Sahel.

Pia Mali, baadhi ya makundi ya kisiasa na kijeshi yalichoshwa na utekelezaji wa makubaliano ya amani ya 2015 na waasi wa zamani wa Tuareg kaskazini, yaliyoangaliwa na wanajeshi wa UN.

Nchini Niger, hali zilizozunguka mapinduzi ya 2023 zilikuwa tofauti pia.

Msaada wa kisiasa kwa Rais Bazoum ulikuwa umepungua kwa ushirikiano wake wa wazi na Ufaransa, hasa ombi lake la kutuma wanajeshi kulinda mpaka wa kaskazini-magharibi dhidi ya uvamizi wa wanajihaadi wa Mali.

Mapinduzi yaliyofuata hivi karibuni huko Gabon, Agosti 2023, yalitokana pia na hasira za ndani. Katika mapinduzi hayo, usimamizi wa matokeo ya uchaguzi uliopelekea ushindi usio wa kawaida wa Rais Ali Bongo, ambaye alikuwa na hali dhaifu baada ya kukumbwa na ugonjwa wa kiharusi.

Hivyo, hali zinatofautiana sana. Na matukio ya hivi karibuni yanathibitisha mwelekeo tofauti.

Eneo hilo kwa hakika linakabiliwa na mzozo wa usalama, siasa au maendeleo pia.

Lakini mazingira na masuala ya ndani kitaifa mara nyingi ndizo yanasababisha kutokea kwa mapinduzi au jaribio la mapinduzi.

Wengi wanashuku kwamba mapinduzi ya kijeshi ya Guinea-Bissau yalilenga kuzuia ushindi ambao ungeingiza upinzani madarakani.

Wakati wapiganaji wa Benin walionekana kuhamasishwa na mambo mengi mchanganyiko ikiwemo malalamiko ya jeshi, na malalamiko ya kisiasa na kiuchumi kwa ujumla.

Lakini walishindwa kutambua kabisa shauku ya umma Cotonou kwa mabadiliko yoyote ya nguvu au ya kinyume cha kawaida. Umma haukuwa pamoja na waliojaribu kufanya mapinduzi.