Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: William Ruto atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya na IEBC

William Ruto akipokea hati ya ushindi

Chanzo cha picha, William Ruto/Facebook

Tafadhali bofya upya anwani ya ukurasa huu ili kuona matokeo ya hivi punde.

Naibu Rais wa Kenya William Ruto ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Kenya huku kukiwa na matukio ya kutatanisha.

Alimshinda mpinzani wake, Raila Odinga, kwa kupata 50.5% ya kura, kulingana na matokeo rasmi.

Tangazo hilo lilicheleweshwa huku kukiwa na mizozo na madai ya wizi wa kura na upande wa kampeni za Bw Odinga.

Makamishna wanne kati ya saba wa tume ya uchaguzi walikataa kuidhinisha matokeo hayo, wakisema hayakuwa wazi.

"Hatuwezi kuchukua umiliki wa matokeo ambayo yanaenda kutangazwa kwa sababu ya hali isiyoeleweka ya awamu hii ya mwisho ya uchaguzi mkuu," Juliana Cherera, makamu mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022

Ili kushinda duru ya kwanza, mgombea analazimika kupata 50%+1 ya kura zilizopigwa na takribani 25% ya kura za kaunti 24 kati ya 47


Mara ya mwisho kusasishwa: 15/08/2022, 18:59:31 EAT

Matokeo ya mwisho kutoka IEBC

WagombeaKura
William Ruto
50%
50.5%
7,176,141
William Ruto
7,176,141
Muungano wa Kenya Kwanza
Kura: 7,176,141
Takribani 25% ya kura za Kaunti 39/47
Raila Odinga
48.8%
6,942,930
Raila Odinga 6,942,930
Muungano wa Azimio la Umoja
Kura: 6,942,930
Takribani 25% ya kura za Kaunti 34/47
George Wahackoyah
0.4%
61,969
George Wahackoyah 61,969
Chama cha Roots
Kura: 61,969
Takribani 25% ya kura za Kaunti 0/47
David Mwaure
0.2%
31,987
David Mwaure 31,987
Chama cha Agano
Kura: 31,987
Takribani 25% ya kura za Kaunti 0/47
Wagombea wengine
0.6%
93,956
Wagombea wengine 93,956

Mchoro wa data katika jedwali la matokeo lililo hapa chini, inayoonyesha kila kiti cha Seneti kama nukta yenye rangi ilivyoashiriwa

Mara ya mwisho kusasishwa: 16/09/2022, 11:03:31 EAT

Mchoro wa data katika jedwali la matokeo lililo hapa chini, inayoonyesha kila kiti cha Seneti kama nukta yenye rangi ilivyoashiriwa
ChamaViti
Kenya Kwanza33
Muungano wa Azimio la Umoja32
Wabunge wasiofungamana na vyama2
Havijatangazwa0
Chanzo:Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka

Muungano wa chama gani unadhibiti Bunge?

Mara ya mwisho kusasishwa: 16/09/2022, 10:51:00 EAT

Mchoro wa data katika jedwali la matokeo lililo hapa chini, inaonesha kila kiti cha Bunge kama nukta yenye ufunguo wa rangi.
ChamaViti
Muungano wa Azimio la Umoja168
Kenya Kwanza167
Wabunge wasiofungamana na vyama/ wabunge wanaojitegemea14
Havijatangazwa0
Chanzo:Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka