Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: William Ruto atangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya na IEBC

Tafadhali bofya upya anwani ya ukurasa huu ili kuona matokeo ya hivi punde.

Naibu Rais wa Kenya William Ruto ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Kenya huku kukiwa na matukio ya kutatanisha.

Alimshinda mpinzani wake, Raila Odinga, kwa kupata 50.5% ya kura, kulingana na matokeo rasmi.

Tangazo hilo lilicheleweshwa huku kukiwa na mizozo na madai ya wizi wa kura na upande wa kampeni za Bw Odinga.

Makamishna wanne kati ya saba wa tume ya uchaguzi walikataa kuidhinisha matokeo hayo, wakisema hayakuwa wazi.

"Hatuwezi kuchukua umiliki wa matokeo ambayo yanaenda kutangazwa kwa sababu ya hali isiyoeleweka ya awamu hii ya mwisho ya uchaguzi mkuu," Juliana Cherera, makamu mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).