Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Konate hajafikia mkataba mpya na Liverpool

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Ibrahima Konate, 26, yuko katika msimu wake wa tano Anfield na anaamini anastahili kuwa mmoja wa mabeki wanaolipwa vizuri zaidi kwenye Ligi ya Premia. (Team talk)

Liverpool inaweza kumsajili beki wa Tottenham Micky van de Ven, kuchukua nafasi ya Konate na huku Real Madrid ikizingatia mustakabali wa beki huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 24. (Team Talk)

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Sunderland Noah Sadiki, 21, na inaweza kumtoa kiungo wa kati wa Uruguay Manuel Ugarte, 24, katika mkataba wa kubadilishana na mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo. (Give me Sport)

Kobbie Mainoo anatarajiwa kusalia Manchester United kufuatia uteuzi wa kocha wa muda Michael Carrick. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye ameichezea England mechi 10, alikuwa akifikiria kuhama kwa mkopo ili kupata muda wa kucheza. (Fabrizio Romano)

Flamengo bado wana nia ya kumsajili kiungo Lucas Paqueta kutoka West Ham United, ingawa tetesi zinasema hakujakuwa na mawasiliano kati ya vilabu hivyo tangu wiki iliyopita kuhusu mpango wa kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports),

Mchezaji Quinten Timber anayenyatiwa na klabu za West Ham na Aston Villa aliachwa nje ya kikosi cha kwanza cha Feyenoord Jumapili. Marseille tayari wamewasilisha ofa ya kumsajili Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail)

Ipswich Town inatamani kumsajili winga wa Bristol City Anis Mehmeti Januari hii. Mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Albania mwenye umri wa miaka 25 unamalizika msimu huu wa joto. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Arsenal Gabriel Jesus ananyatiwa na klabu ya Palmeiras. Mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 28 amepona jeraha la muda mrefu lakini mkataba wake unamalizika 2027 na anaweza kurejea Brazil. (Mail)

Chelsea wamefikia makubaliano ya kibinafsi na Jeremy Jacquet, 20, lakini watalazimika kuboresha mpango wao wa kumsajili beki wa Rennes na Ufaransa chini ya miaka 21 ambaye pia anasakwa na Arsenal. (Metro)

Bournemouth haina nia ya kumuachia Marcos Senesi mwezi huu ingawa Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 28 amekataa ofa nyingi za kuongeza mkataba wake, ambao unaisha msimu huu wa joto. Juventus na Barcelona zimeonyesha nia ya kumnunua beki huyo. (Talk sport)