Ebola DRC: Wafanyikazi wa afya watishiwa kuuawa kwa kuokoa maisha

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlipuko wa Ebola uliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umefikia mwaka mmoja leo (Agosti mosi) na umesababisha vifo vya karibu watu 1800.
Jamii ya Kimataifa inajaribu kusaidia kukabiliana na ugonjwa huo lakini hofu na uvumi umewafanya watu kuwashambulia walewanaosaidia kukabiliana na ugonjwa huo - Karibu wafanyikazi saba wa afya wameuawa mwaka huu nchini DRC.
BBC imezungumza na madaktari na wauguzi kuhusu hatari wanayokabiliana nayo wakijaribu kuokoa maisha.
"Watu wanadhani ni uwongo hakuna Ebola," anasema Dkt Pascal Vahwere, mataalamu wa magonjwa ya kuambukiza anayefanya kazi ya kukabiliana na ugonjwa huo.
"Tulishambuliwa kwa kufanya kazi yetu."
Dkt Vahwere aliisimulia BBC kilichomkuta alipozingirwa na kundi la watu waliokuwa na hasira mwezi Machi alipokua akiongoza kundi la wafanyikazi wa afya kwenda kutoa chanjo katika kijiji kimoja mkoani Kivu Kaskazini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC).
"Ghafla tulishtukia tumezingirwa na kundi la watu waliojihami kwa silaha za moto na mapanga. Hatukujua kwa nini walitaka kutushambulia. Tuliogopa. Tulizungumza nao kupitia viongozi wa kijamii na hatimae waliondoka bila kutudhuru."

Chanzo cha picha, MSF
Wafanyikazi wa umma wanawatambua watu ambao tayari wameambukizwa na kuwaleta katika vito vya matibabu. Pia wanawasidia kuwazika waliofarika.
Lakini kwa ni hatari sana kwa wafanyikazi hao kwenda katika vijiji vilivyo na watu walioambukizwa Ebola.
Huku maambukizi ya Ebola yakiendelea kusababisha vifo vya watu wengi, wafanyikazi wa afya nchini DRC wanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa na wanamgambo wenye hasira kufuatia uvumi unaosambazwa kupitia makundi ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp.
Karibu wafanyikazi saba wa afya wameuawa mwakahuu peke yake. BBC imezungumza na baadhi ya wale wanaokabiliana na ugonjwa wa Ebola kufahami ni nini kinachofanyika.
Uvumi
Nadharia ya njama na ukosefu wa mbinu ya kukabiliana na ugonjwa huo inawapandisha ghadhabu watu wanaokabiliwa na hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kusambaa kwa taarifa za uwongo kumewafanya watu kuamini kuwa Ebola ni biashara ya kuwatengenezea pesa wanasiasa," anasema Dkt Vahwere.
Anafanya kazi na shirika la Kimataifa la Afya mjini Goma, Mashariki mwa DRC.
Mji huo uliripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa huo wiki mbili zilizopita. Kisa cha pili cha Ebola kiligunduliwa mjini humo wiki hii.
"Baadhi yao hata wanasema matibabu ya ugonjwa huo yanalenga kuwaua watu," aliongeza.
Mashambulio
Uvumi huo umechangia ongezeko la mashambulizi hatari.
"Kutoka Januari mosi hadi Julai 24 mwaka 2019, mashambulio 198 yameripotiwa dhidi ya vituo vya afya na wafanyikazi wake kama ilivyoratibiwa na WHO imesbabisha vifo vya watu saba na wengine 58 kujeruhiwa DRC," Sakuya Oka, Meneja wa Mawasiliano WHO aliiambia BBC.

Chanzo cha picha, Institute of Tropical Medicine
Orodha ya waliouawa inajumuisha mtaalamu magonjwa yanayosababisha majanga wa ngazi ya juu wa WHO Richard Mouzoko.
Aliuawa wakati wakati wa shambulio dhidi ya Hospitali ya Chuo Kikuu ya Butembo Aprili 19. Watu wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio hilo.
Mwezi Mei wanavijiji Mashariki mwa DRC waliwashambulia wafanyikazi wa afya na kuiba vifaa katika vituo vya tiba.
Tarehe 15 Julai wafanyikazi wawili wa afya walikuwa wakiendesha kampeini ya kukabiliana Ebola waliuawa majumbani mwao katika Mkoa wa Kivu Kaskazini.
Kusambaa
Visa vya mashambulizi hatari vinaendelea kupungua dhidi ya wale wanaokabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ilichukua takribani siku 224 kwa idadi ya visa vya maambukizi kufika 1,000, lakini ilichukua siku zingine 71 kufikia watu 2,000.
"Kufikia (Jumatatu) wiki hii visa 57 vya ugonjwa wa Ebolaviliripotiwa katika kituo cha tiba cha Beni. Hii ni kumaanisha tunakabiliwa na kibarua kigumu kudhibiti hali ya mambo," anasema Dkt Freddy Sangala.
Ebola ni ugonjwa unaoambukizwa na virusi ambapo aliyepata maambukizi hupata dalili za homa, uchovu, maumivu ya viungo na koo.
Watu huambukizwa kwa njia ya kugusana, njia ya mdomo na pua, pia kwa njia ya damu, matapishi, kinyesi,majimaji ya kwenye mwili wa mtu mwenye Ebola
Wagonjwa hupoteza maisha kutokana na kupungukia maji mwilini na viungo kushindwa kufanya kazi.
Hakuna tiba ya Ebola, lakini ugunduzi wa mapema wa dalili zake na kukabiliana na nazo husaidia kuokoa maisha.
Chanjo
Hivi karibuni chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola imeanza kutumiwa na watu wamekuwa wakipewa chanjo hiyo ilikudhibiti maambukizi ya Ebola nchini DRC.

Chanzo cha picha, Getty Images
Karibu watu 170,000 waliotangamana na watu waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari wamepewa chanjo.
Lakini visa vya mashambulizi dhidi ya wahudumu wa afya vililemaza kampeini ya chanjo, hali iliyochangia kuongezeka na kusambaa zaidi kwa maambukizi mapya.
Kutoaminiana na waasi
Mlipuko wa Ebola unatokea katika eneo ambalo ni nyumbani kwa makumi ya makundi ya waasi.
Baadhi yao wanalaumiwa na serikali kwa kufanya mashambulizi dhidi ya wahudumu wa afya.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Cha kusikitisha ni kuwa tuna uwezo wa kiufundi wa kukabiliana na Ebola, lakini hatuwezi kufanya hivyo hadi mashambulizi yakomeshwe, itakuwa vigumu kukabiliana na mlipuko huu," Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliandika katika Twitter yake Mei 10 baada ya wahudumu wa afya kushambuliwa.
Katika eneo la Kivu Kaskazini, kundi la waassi linalofahamika kama Mai-Mai linalaumiwa kwa kuhusika na baadhi ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na wafanyikazi wake kwa mujibu wa serikali.
Kunsi lengine la waasi ni lile la Allied Defence Forces (Kundi la waasi wa Uganda linalofanya kazi DR Congo) pia linalaumiwa kwa kusababisha wahudumu wa afya kusitisha huduma zao.
Kumekuwa na msururu wa maambukizi kutoka kwa kundi lingine lisilojulikana dhidi ya vituo vya tiba ya Ebola.
Katika kisa kimoja Mwezi Mei, jamaa wa familia moja waliwavamia wahudumu wa afya waliyokuwa wakiwasaidia kuwazika jamaa zao.













