Imani potofu na mashambulio changamoto za vita vya Ebola DRC

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashambulio ya Wanamgambo na ukosefu wa imani ya jamii kwa wafanyakazi wa afya mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kunakwamisha juhudi za kudhibiti mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola ambao kwa sasa umesambaa hadi nchi jirani ya Uganda.
Makundi ya waasi yenye silaha yamekuwa yakishambulia mara kwa mara vituo vya tiba ya Ebola, huku kukiwa kuna ukosefu wa imani miongoni mwa jamii za wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa na Ebola ambao walaumu wageni kwa mlipuko ni masuala yanayofanya juhudi za kukabiliana na mlipuko huo kuwa ngumu katika majimbo yenye mizozo ya Ituri na Kivu.
Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema kuwa watu 300,000 wamesambaratika kufuatia ghasia katika eneo hilo katikakipindi cha mwezi huu pekee.

Chanzo cha picha, Reuters
DRC imerekodi visa 2,025 vya Ebola na vifo 1,357 vilivyosababishwa ugonjwa huo tangu ulipolipuka mwezi Agosti 2018. Watu wawili waliovuka mpaka na kuingia Uganda kutoka Kongo walikufa tarehe 12 Juni, jambo lililozua hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo katika kanda hiyo ya Afrika.
Hata hivyo , tarehe 14 Juni, Shirika la Afya duniani (WHO), ambalo linaratibu shughuli za dharura za kiafya za kukabiliana na mlipuko kwa ushirikiano na Wizara ya Afya ya DRC , waliamua kutotangaza ugnujwa kuwa dharura ya afya ya umma ya kimataifa.
Takriban watu 11,300 walikufa kutokana na mlipuko wa Ebola katika mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia kati ya mwaka 2013 - 2016.
Kipindi cha mashambulio dhidi ya wahudumu wa afya na vituo.
Umoja wa mataifa umeripoti zaidi ya matukio 174 ya ghasia zinazoathiri wafanyakazi na vituo vinavyotoa huduma za dharura za Ebola katika majimbo ya Ituri na Kivu kaskazini tangu ulipoanza mlipuko. Matukio ,maarufu ni:

Chanzo cha picha, REUTERS
Mashambulio ya mwaka 2018:
- Septemba 22-24: Uvamizi wa vikosi vya waasi wa Uganda wa Allied Defence Forces (ADF) mjini Beni, Kivu Kaskazini ambapo watu 18 walikufa na kusababisha maandamano ya kuvurugwa kwa shughuli za kukabiliana na Ebola.
- Oktoba 20: Watu kumi na wawili waliuawa katika shambulio la ADF katika mji wa Beni na kuvuruga shughuli za kukabiliana na Ebola kwa siku kadhaa.
- Oktoba 23 : Wauguzi wawili kutoka kitengo cha tiba cha Jeshi la DRC (FARDC) waliuawa katika mji wa Butembo tarehe 22 Oktoba.
- Novemba 8: Wanamgambo wa Mayi-Mayi waliwateka kwa muda timu ya wahudumu wa kukabiliana na Ebola.
- Disemba 27:Wagonjwa walitoroka walitoroka wakati umati wa watu wenye hasira walipovamia kituo cha kupuma Ebola cha Beni.
- Februari 16: Wakazi walivamia kituo cha udhibiti wa Ebola katika jimbo la Ituri.
- Februari 24 : Watu wenye silaha waliteketeza kwa motokituo cha matibabu ya Ebola katika eno la Katwa, mjini Butembo.
- Februari 27: Afisa wa Usalama aliuawa na wagonjwa 31 walitoroka baada ya shambulio dhidi ya madaktari wasio na mpaka (MSF) katika kituo cha matibabu ya Ebola mjini Butembo.
- Machi 9 : Watu wawili, akiwemo afisa wa polisi waliuawa katika kituo cha matibabu ya Ebola katika mji wa Butembo.
- Machi 14: Mtu mmoja aliuawa katika shambulio la wizi katika kliniki ya Ebola katika ya Mamboa, eneo la Lubero , katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
- Aprili 5: Watu wenye silaha walivamia na kupora ofisi za MSF yaliyopo katika eneo la Byakato, jimboni Ituri. Hakuna binadamu aliyeripotiwa kufa.
- Aprili 19 : Daktari wa Cameroon anayefanyia kazi shirika la afya Duniani WHO alipigwa risasi katika shambulio dhidi ya kliniki ya Chuo kikuu cha Graben (UCG) iliyopo mjini Butembo.
- Aprili 20: Shambulio lilifanyika katika Hospitali ya Katwa mjini Butembo na kuzimwa na vikosi vya usalama. Mshambuliaji akauawa.
- Mei 3: Shughuli za kukabiliana na Ebolaziliahirishwa mjini Butembo baada ya makabiliano baina ya waendesha pikipiki na timu iliyokuwa ikijaribu kusimamia mazishi salama ya wagonjwa wa Ebola.
- Mei 8: Maafisa wa kukabiliana na Ebola mjini Butembo walishambuliwa na wanamgambo wa Mayi Mayi ambapo washambuliajii kumi waliuawa. Shughuli hizo ndio kwanza zilikuwa zimefufuliwa baada ya kuahirishwa kwa siku tatu .
- Mei 10 : Vipeperushi vilivyotishia wahudumu wa afya wa Ebola katika maeneo ya Beni, Butembo na Oicha,vilisambazwa vikiwaambia waondoke maeneo hayo.
- Mei 13 : Vikosi vya usalama vilizima shambulio dhidi ya kituo cha matibabu ya wagonjwa wa Ebola cha Butembo, mshambuliaji aliuawa.
- Mei 13-14: Kituo cha afya cha Mutiri kilichopo eneo la Lubero kilivamiwa , vifaa vya matibabu vikaharibiwa na wahudumu wa afya wakatishiwa.
- Mei 17: Wahudumu wa mazishi ya heshmima na salama (EDS) walishambuliwa kwa matusi na wajumbe wa familia ya marehemu katika mji wa Bunia. Katika mji wa Butembo, wahudumu wa EDS walipigwa mawe.
- Mei 25 : Chumba cha vipimo vya awali katika kituo cha afya cha Vulamba mjini Butembo kilivamiwa na wezi waliopora vifaa. Katika kijiji cha Vusahiro katika kanda ya afya ya Mabalako, wakazi waliwavamia wahudumu wa afya, na kumuua mmoja wao.
- Juni 3: Vifaa viliibiwa kutoka katika maabara ya madibabu katika eneo la Komanda. Watu kumi wakauawa wakati wa uvamizi wa watu wenye silaha katika eneo la Rwangoma, mjini Beni, muda mfupi baada ya mazungumzo ya jamii yaliyoandaliwa na tiimu ya kukabiliana na Ebola.
- Juni 4 : Maandamano yalifanyika mjini Beni yalivuruga huduma za afya ya Ebola kwa umma.
- Juni 16 : Waendesha pikipiki na timu ya udhibiti wa maambukizi ya Ebola walikabiliana katika eneo la Rwampara, Ituri.
- Juni 17: Timu ya mazishi salama ya wagonjwa wa Ebola (EDS) ilishambuliwa mjini Bunia. Wahudumu wa timu hiyo walishambuliwa na kuibiwa.
Jinsi WHO na Serikali walivyokabiliana na Ebola:

Chanzo cha picha, JOHN WESSELS/OXFAM
Wizara ya afya ya DRC imepongezwa kwa juhudi za kudhibiti ugonjwa kabla ya mlipuko wa Ebola kutokea. Mamlaka nchini humo na jamii ya kimataifa wanasema mashambulio yamesababisha udhibiti wa siku kwa siku wa mlipuko kubakia mikononi mwa maafisa wa afya na WHO.
Hata hivyo , mauaji ya daktari wa WHO wa magonjwa ya maambukizi raia wa Cameroon katika mji wa Butembo yaliyofanywa na waasi wa Mai-Mai yameleta mabadiliko inapokuja katika kushughulikia hali ya tahadhari na kwamba imekuwa wazi kuwa kushughulikia mlipuko wa Ebola imekuwa ni vigumu kutokana na hali ya usalama katika eneo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Tukio hilo lilifuatiwa na msururu wa mashambulio ambapo viwango vya maambukizi viliongezeka mara dufu na kuibuka kwa mkanganyiko wa namna umma unavyopaswa kujikinga na mlipuko.
" Haiwezekani kusitisha maambukizi ya Ebola katika hali kama hiyo wakati kuna uhasama na jamiii , uingiliaji wa kisiasa na makundi yenye silaha. Hali katika maeneo hayo haijaimarika vya kutosha kuwezesha huduma za umma kufanyika ,"amesema Mike Ryan, mkurugenzi wa WHO anayehusika na mpango wa huduma za afya za dharura.
Kupungua kwa kwa idadi ya visa na vifo kulisababishwa na ziara ya rais mpya Felix Tshisekedi, ambaye alitembelea kituo cha matibabu ya Ebolo mjini Beni. Alianzisha kikundi cha uratibu wa kiwango cha juu ukiongozwa na waziri mkuu lakini haijabainika wazi kama kuna mafanikio yoyote kutokana na hatua hiyo au kama malengo yaliyotarajiwa yalifikiwa.












