Mfahamu kiongozi mkuu wa dini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei

Ayatollah Ali Khamenei 2014

Chanzo cha picha, AFP

Ayatollah Ali Khamenei ndiye kiongozi wa dini mbali na kuwa kiongozi mkuu wa utawala wa Iran. Yeye ndiye anayefanya uamuzi wa mwisho kuhusua msawala ya kisiasa nchini Iran.

Akijulikana kama kiongozi mkuu wa taifa hilo , Ayatollah Khamenei mara ka mara amepinga mataifa ya magharibi na hususan lile la Marekani.

Licha ya kuunga mkono kundi la wapatanishi wa taifa lake , Ayatollah Khamenei amekuwa akipinga matokeo kuhusu mazungumzo na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran.

Ayatollah Khemenei alimrithi mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ayatollah Khomeini 1989.

Kabla ya kuchukua wadhfa huo alikua rais wa taifa hilo kwa mihula miwili kuanzia 1981 hadi 1989.

Mnamo mwezi Septemba 2014, Ayatollah Khamenei, akiwa na umri wa miaka75, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume nchini Tehran.

Tangazo kuhusu upasuaji huo kabla ya utaratibu halikutarajiwa kwa kuwa afya ya ya kiongozi huyo huwa swala la siri kubwa.

Miaka saba awali kulilkua na uvumi kuhusu kifo cha kiongozi huyo duniani , kwa kuwa hakutangaza kwamba alikuwa na homa mbaya na hakuweza kuhudhuria hafla za umma.

Uwezo wake ulihojiwa

Wakati alipokuwa rais , Ayatollah Khamenei alikuwa na uhusiano mbaya na waziri mkuu Mirhossein Mousavi ambaye alionekana kulemea upande wa magharibi.

Hatahivyo Mousavi aliungwa mkono na kiongozi huyo wa dini huku tofauti zao za kiuchumi, kijamii na sera za kidini zikiendelea.

Uamuzi wa kwanza wa Ayatollah Khamenei kuwa kiongozi mkuu wa dini kufuatia kifo cha Ayatollah Khomeini ulikuwa kubadilisha katiba na kuondoa wadhfa wa waziri mkuu.

Mabango ya Ayatollah Khamenei na Ayatollah Ruhollah Khomeini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ali Khamenei (kushoto) ndio kiongozi wa pili wa mapinduzi baada ya Ruhollah Khomeini (r)

Ayatollah Khamenei amedaiwa kukosa ucheshi na umaarufu mkubwa kama mtangulizi wake. Khomeini alikuwa kiongozi wa dini wa hadhi ya juu aliyefaa kuigwa.

Wakati Ayatollah Khamenei alipochukua uongozi , katiba ililazimika kufanyiwa ukarabati ili kuruhusu wadhfa huo kuchukuliwa na kiongozi yeyote wa dini bila kutilia shime wadhfa wake.

Aliimarisha uongozi wake kama kiongozi mkuu wa dini nchini humo kwa kujenga uhusiano wake na taasisi mbalimbali nchini humo pamoja na vikosi vya usalama, hususan jeshi lenye uwezo mkubwa la Islamic Revolution Guards Corps (IRGC).

Mwaka 1997 , alikosana na Ayatollah Hossein Montazeri , kiongozi wa dini aliyeheshimika na msomi.

Ayatollah Montazeri , mkosoaji wake mkubwa aliyefariki 2009 , alihoji uwezo wa kiongozi huyo wa dini.

Hatua hiyo ilisababisha kufungwa kwa shule yake ya kidini , shambulio katika afisi yake ya Qom na kuhukumiwa kifungo cha nyumbani kwa muda.

Ali Khamenei akivuta sigara

Chanzo cha picha, other

Maelezo ya picha, Cha kushangaza kuhusu kiongozi huyo wa dini Ali Khamenei alikuwa akivuta sigara

Uamuzi wa Ayatollah Khamenei pia ulikosolewa.

Wakati alipomuunga mkono rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad, kufuatia ushindi wake katika uchaguzi uliokumbwa na utata 2009 , raia wengi wa Iran walifanya maandamano wakipinga matokeo hayo.

Wagombea walioshindwa Mirhossein Mousavi na Mehdi Karroubi walipinga uchaguzi huo .

Wote waliwekwa katika kifungo cha nyumbani mnamo mwezi Februari 2011 , pamoja na mke wa bwana Mousavi Zahra Rahnavard, baada ya kuitisha maandamano wakiunga mkono mapinduzi ya raia yaliokuwa yakiendelea nchini Misri na Tunisia.

Udhibiti wa kihafidhina

Kama kiongozi wa kidini, Ayatollah Khamenei ana uwezo wa kuwachagua moja kwa moja wanachama wa baraza la walezi . Baraza hilo linasimamia uchaguzi mbali na ukaguzi wa wagombea.

Katika uchaguzi wa Mwaka 2004, baraza hilo liliwaondoa katika kinyang'anyiro maelfu ya wagombea wa ubunge ikiwemo wenye misimamo ya wastani, wanaopigania mageuzi na wanachama wa serikali iliopita.

Wahafidhina walishinda kwa asilimia 70 ya kura zilizopigwa.

Mwaka 2013, baraza hilo lilimzuia Akbar Hashemi -Rafsanjani , rais wa zamani na kiongozi wa baraza lenye ushawishi mkubwa nchini Iran kutowania urais kutokana na madai ya kuwa mzee.

Bwana Rafsanjani alikuwa ameunga mkono waandamanaji baada ya uchaguzi wa 2009.

Ayatollah Khamenei amekuwa akiunga mkono usimamizi wa baraza hilo la walezi , licha ya ukosoaji mkubwa kwamba kuwandoa wagombea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kunaharibu demokrasia.

Uhusiano wa kigeni

Katika hotuba yake kama rais 1981 , Ayatollah Khamanei aliahidi kukabiliana na upotofu, ukombozi na wasomi wanaounga mkono sera za Marekani.

Mwaka 2009 wakati rais Barrack Obama alipoipatia Iran 'mwanzo mpya wa mazungumzo ya kidiplomasia' jibu la Ayatollah Khamenei lilifutiliwa mbali.

Alisema kwamba hajawahi kuona mabadiliko katika sera ya Marekani akisisitiza kuhusu Marekani kuisaidia Israel na kuiwekea vikazo Iran.

Lakini alisema kua iwapo rais Obama angebadili sera hiyo ya Marekani basi alikua tayari kushirikiana nae.

Mwaka 2013, kabla ya kufanyika kwa mazungumzo ya kinyuklia ya Iran pamoja na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani , Ayatollah alisema kuwa hapendi diplomasia.

Ayatollah Ali Khamenei 2014

Katika lugha ambayo ahusishwi nayo , Ayatollah Khamenei alizungumza kuhusu diplomasia kuwa chanzo cha kutabasamu katika mazungumzo.

Mnamo mwezi Novemba 2013, Iran na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani waliafikia makubaliano ya kwanza ya kinyuklia na Iran, ambapo taifa hilo la Kiislamu lilikubali kusitisha mpango wake wa kinyuklia ili kuondolewa vikwazo.

Lakini tarehe 7 mwezi Julai 2014, ikiwa ni wiki mbili kabla ya makubaliano ya mpango huo kuafikiwa , Ayatollah Khamenei alitoa hotuba yenye maelezo mengi ya kiufundi , akisisitiza kuwa Iran inahitaji sana kuongeza uzalishaji wa madini ya Uranium.

Siku ya miwsho ya mwezi Julai ilipita na pande hizo mbili zikakubaliana na kuongeza muda wa mazungumzo hadi mwezi Novemba 2014.

Wakati na baada ya vita vya Marekani dhidi ya Iraq , Khamenei aliikosoa sera ya Marekani. ''Uvamizi wa Iraq sio kitu ambacho Marekani inaweza kumeza'', alisema.

Mnamo mwezi Juni 2014, baada ya wapiganaji wa Kijihadi wa Islamic State kuteka maeneo ya kaskazini mwa Iraq , Ayatollah kwa mara nyengine alipinga hatua ya Marekani kuingilia kati .

Lakini mnamo mwezi Agosti, aliunga mkono uteuzi wa Haydar al-Abadi kuwa waziri mkuu mpya akikata uhusiano na mwandani wake wa zamani Nouri Maliki.