Vikwazo vikali zaidi vya Marekani dhidi ya Iran vimeanza kutekelezwa

Protestors

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waandamanaji wakiwa nje ya uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran siku ya Jumapili

Vikwazo vikali zaidi vya Marekani dhidi ya Iran vinaanza kutekelezwa leo Jumatatu.

Uongozi wa Trump ulirejesha vikwazo vyote vilivyotolewa wakati wa wa makubaliano ya mwaka 2015 vikiilenga Iran na nchi zinazofanya bishaara nayo.

Vitalenga mauzo ya mafuta, usafiri kwa njia ya baharini na mabenki ambavyo vyote ni muhimu sana kwa uchumi.

Maelfu ya raia wa Iran waliokuwa wakisema "Kifo kwa Marekani" waliandamana Jumapili wakikana kuwepo mazungumzo.

Jeshi la Iran nalo limesema kuwa litafanya mazoezi ya kijeshi leo Jumatatu na Jumanne kuonyesha uwezo wake wa kijeshi.

Maandamano hayo yalifanyika wakati wa maadhimisho ya 39 ya kutekwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran, ambayo yalisababisha kutokea uhasama wa miongo minne.

Kabla ya kusafiri kwenda mkutano wa kampemni wa uchaguzi wa nusu muhula nchini Marekani, Rais Donald Trump alisema Iran ina wakati mgumu wakati mgumu nchini ya sera za uongozi wake

Kipi kilizua haya?

Marekani ilitangaza vikwazo tena baada ya Trump mwezi Mei kujito kwa mkataba wa mwaka 2015 uliolenga kupunguza mipango ya nyuklia ya Iran.

Marekani inasema inataka kuzima vitendo viovu vya Ina vikiwemo udukuzi wa mitandao, majaribio ya makombora ya masafa marefu na uungaji mkono wa makundi ya kigaidi mashariki ya kati.

Donald Trump signs presidential order

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency

Maelezo ya picha, Donald Trump aliitoa Marekani nje ya makubaliano ya nyuklia mwaka 2015 mwezi Mei

"Tunafanya kazi kuhakikisha kuwa tutaunga mkono watu wa Iran na tunaelekeza shughulia zetu kuhakikisha kuwa tabia ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran imebadilika, wazitri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Mike Pompeo alikiambia kituo cha Fox News siku ya Jumapili.

Ni athari zipi zitakuwepo?

Marekani imekuwa ikiiwekea Iran vikwazo lakini wadadisi wanasema awamuj hii ya vikwazo ndiyo kubwa zaidi.

Zaidi ya watu 700, kampuni, vyombo vya habari na ndege kwa sasa vimewekewa vikwazo, yakiwemo mabenki makubwa, wauza mafuta na kampuni za usafiri wa baharini.

Bw Pompeo amesema zaidi ya kampuni 100 kubwa zimejitoa Iran kufuatia vikwazo hivyo.

US Secretary of State, Mike Pompeo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mike Pompeo

Pia alisema mauzo ya mafuta ya Iran yameshuka kwa karibu mapipa milioni moja kwa siku, na kufunga chanzo cha fedha muhimu nchimi humo.

EU imejibu kwa njia gani?

Uingereza , Ujerumani na Ufaransa ambazo ni kati ya nchi zilizo kwenye makubaliano ya nyuklia zote zimekataa vikwazo hivyo.

Zimeahidi kuzisaidia kampuni za Ulaya zinazofanya baishara halali na Iran na kubuni njia mbadala za malipo ambazo zitasaidia kampuni kufanya bishara bila ya vikwazo vya Marekani

Supreme Leader Ayatollah Ali Khamenei

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei alisema Marekani haiwezi kuitawala Iran

Hali imekuwaje nchini Iran?

Vikwazo vya Marekani viliwekwa kuja wakati siku ubalozi wa Marekani ulitwaliwa Novemba 4 mwaka 1979, uliofanyika mara baada ya kuanguka kwa chama kilichokuwa kikiungwa mkono na Marekani cha Shah.

Raia 52 wa Marekani walishikwa mateka ndani ya ubalozi kwa siku 444 na nchi hizi mbili zimekuw maadui tangu wakati huo.

Wenye misimamo mikali hufanya maandamano kuadhimisha kutekwa kwa ubalozi lakini maandamano ya Jumapili pia yalikemea vikwazo.

Vyombo vya habari nchini Iran vilisema mamilioni ya watu walijitokeza kwenye miji kote nchini, wakielezea utiifu wao kwa kiongozi Ayatollah Ali Khamenei.

Ilifuatia hotuba kali ya Ayatollah Khamenei siku ya Jumamosi ambapo alioanya kuwa Marekani haitaweweza kuwa na ushawishi iliokuwa nao dhidi ya Iran kabla ya mwaka 1979.