Tetesi za soka Jumamosi; Glasner yuko kwenye rada ya Manchester United

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha anayeondoka Crystal Palace, Oliver Glasner, ni miongoni mwa majina yanayozingatiwa kuchukua nafasi ya ukocha wa Manchester United msimu wa joto ujao. (Mirror)
Chelsea na Manchester City wanaongoza katika mbio za kumsajili kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Mhispania mwenye umri wa miaka 18 Dro Fernandez, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 5.1 (euro milioni 6) katika mkataba wake. (Talksport)
Kocha wa Tottenham, Thomas Frank, anataka kumsajili mchezaji wa kushambulia upande wa kushoto, ama mwezi Januari au majira ya joto. (Telegraph)
Kiungo wa England James Ward-Prowse, 31, anaweza kuondoka West Ham, huku Burnley wakionyesha nia ya kumsajili nahodha wa zamani wa Southampton. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Leeds United wameulizia upatikanaji wa mshambuliaji wa Norway Jorgen Strand Larsen, 25, lakini bado hawajatoa ofa rasmi kwa Wolves. (Athletic)
Inter Milan wanapanga kumpa mkataba mpya mshambuliaji wa Italia mwenye umri wa miaka 20 Francesco Pio Esposito, ili kuzima nia ya vilabu vya Ligi Kuu ya England. (Tuttosport)
Crystal Palace wako hatarini kumpoteza mchezaji mwingine muhimu, huku mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 28, akiwa tayari kwa changamoto mpya na Juventus wakionyesha nia ya kumnyakua. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wataanza mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 25, kufuatia kuondoka kwa Xabi Alonso katika uwanja wa Bernabeu. (ESPN)
Manchester United wamekataa ofa kadhaa kutoka vilabu vya Ligi Kuu ya England na AC Milan kwa ajili ya beki wa England Harry Maguire, 32, mwezi huu. (Sun)
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane, anazingatiwa kuchukua nafasi ya Didier Deschamps kama kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa. (L'Equipe)

Chanzo cha picha, Getty Images
Stoke City wanataka kumsajili kwa mkopo winga wa England mwenye umri wa miaka 23 Jesurun Rak-Sakyi kutoka Crystal Palace kwa kipindi kilichosalia cha msimu. (Football Insider)
Fulham bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Marekani wa PSV, Ricardo Pepi, 23, licha ya kuvunjika mkono wake mapema mwezi huu. (Sky Sports)
Kiungo wa Red Star Belgrade na Serbia mwenye umri wa miaka 17 Vasilije Kostov anafuatiliwa na Arsenal. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Ofa ya Crystal Palace ya mkopo wenye sharti la kununuliwa kwa mshambuliaji chipukizi wa Ufaransa Sidiki Cherif, 19, imekataliwa na Angers, ambao wanataka uhamisho wa moja kwa moja pekee. (Foot Mercato)
Newcastle United wamejitokeza kuwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka beki wa Bosnia-Herzegovina Tarik Muharemovic, 22, wa Sassuolo, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka AC Milan. (Football Insider)
Juventus wamepunguza shauku yao ya kumsajili tena mshambuliaji wa Italia Federico Chiesa, 28, kutoka Liverpool. (Fabrizio Romano)















