Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Atletico Madrid wamlenga kiungo wa Wolves na Brazil Joao Gomes

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joao Gomez
Muda wa kusoma: Dakika 2

Atletico Madrid wanamlenga kiungo wa kati wa Wolves na Brazil Joao Gomes, 24, baada ya klabu hiyo ya Uhispania kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Conor Gallagher kwa Tottenham siku ya Jumatano. (Marca - In Spanish)

Wakati huo huo, kiungo wa kati wa Wanderers ya Zimbabwe Marshall Munetsi, 29, yuko tayari kujiunga na Paris FC kwa mkopo. (L'Equipe - In French)

Everton wametuma ofa rasmi kwa Fenerbahce ya Uturuki kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Morocco Youssef En-Nesyri, 28. Mazungumzo yanaendelea kwa ajili ya uhamisho wa awali wa mkopo na chaguo la pauni milioni 17 kumnunua. (Fabrizio Romano)

Nottingham Forest pia wako kwenye kinyang'anyiro cha kumwania En-Nesyri lakini hisia za Fenerbahce ni kwamba anapendelea kuhamia Everton. (Florian Plettenberg)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Youssef En-Nesyri

Everton pia wanavutiwa na dili la mshambuliaji Callum Wilson, 33, ambaye yuko kwenye mazungumzo ya kumaliza mkataba wake na West Ham. (Athletic - Subscription Required)

The Toffees, pamoja na Werder Bremen na Ajax, wanamfuatilia beki wa kulia wa Ukraine Yukhym Konoplya. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na Shakhtar Donetsk unamalizika msimu wa joto. (Florian Plettenberg)

West Ham watafanya mkutano wa ndani na wanahisa wao wikendi hii kujadili kupunguza bei inayotakiwa kwa kiungo Lucas Paqueta, 28, ambaye anasakwa na Flamengo nchini kwao Brazil. (ESPN,)

Beki wa Santos Souza, 19, anatarajiwa kufanyiwa vipimo na Tottenham mjini London siku ya Alhamisi, huku Spurs wakikamilisha dili la pauni milioni 13 kumsaini beki huyo wa kushoto wa Brazil. (Sky Sports)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Souza

Brentford wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 15.6 kwa mshambuliaji wa Lazio na Italia Matteo Cancellieri, 23. (Gazzetta dello Sport - In Italy).

Crystal Palace wako kwenye mazungumzo na klabu ya Ligue 1 Angers kuhusu mshambuliaji wa Ufaransa Sidiki Cherif. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye anaweza kucheza katikati na nje, ana miaka miwili na nusu kwenye mkataba wake. (Sky Sports)

Roma italipa ada ya mkopo ya pauni milioni 2 kwa fowadi wa Aston Villa Donyell Malen, 26, huku mkataba huo ukijumuisha kipengele cha pauni milioni 25 kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi kwa misingi ya kudumu. (Fabrizio Romano),

Bournemouth wanafahamu kuwa wanaweza kukabiliwa na vita ya kumsaka kiungo wa kati Mwingereza Alex Scott, 22, mwaka huu huku klabu za Ligi ya Premia Manchester United, Manchester City, Aston Villa na Newcastle United zikimwania. (Team Talks)