Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Aston Villa kumsajili Tammy Abraham

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tammy Abraham
Muda wa kusoma: Dakika 2

Aston Villa wanataka kuweka mkataba wa kudumu na mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Besiktas kutoka Roma.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alitumia msimu wa 2018-19 kwa mkopo katika klabu ya Villa na kuwasaidia kupandishwa daraja hadi Ligi ya Premia. (Times - Subscription Required)

Manchester United wanazidi kujiamini kuwa watamsajili kiungo wa kati wa Cameroon Carlos Baleba, 22, kutoka Brighton msimu wa joto. (Sun),

Juventus wamefanya uchunguzi kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 28, kutoka Crystal Palace mwezi huu wakitafuta mbadala wa muda mrefu wa mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 25. (Sky Sports).

Inter Milan, Napoli na Fiorentina wote wanawania kumnunua beki wa Manchester United na Uingereza Harry Maguire, 32, mwezi Januari. (Tuttomercato - In Italy)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harry Maguire

Mlinzi wa Nottingham Forest na Brazil Murillo, 23, anazingatiwa na Manchester United huku wakitafuta mbadala wa Maguire wa muda mrefu. (Mail)

Chelsea wanataka kusajili mlinzi dirisha hili huku mchezaji wa kimataifa wa Argentina wa Bournemouth Marcos Senesi, 28, akiwa miongoni mwa walengwa kadhaa. (Talksport),

Kocha mkuu wa muda wa Manchester United Michael Carrick ana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Middlesbrough Muingereza Hayden Hackney, 23, ambaye pia anavutia Tottenham. (TeamTalks),

Valencia wamewasiliana na Brentford kuhusu upatikanaji wa kiungo wa kati wa Nigeria Frank Onyeka, 28. (Sky Sports)

West Ham inaonekana huenda ikamkosa mlinzi wa Toulouse Charlie Cresswell, 23, baada ya Wolfsburg kuwasilisha ombi la £15.6m kwa Muingereza huyo. (Athletic - Subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Cressewell

Nottingham Forest wanashinikiza kumsajili kiungo wa kati wa Italia na Inter Milan Davide Frattesi, 26. (Tuttomercato - In Italy)

Kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo anaweza kuondoka kwa mkopo iwapo muda wake wa kucheza Manchester United hautaimarika mwezi huu, huku Napoli wakiongoza mbio za kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Star),

Crystal Palace na Brighton wanashindana na Celtic na Norwich kumnunua mlinzi wa Dundalk mwenye umri wa miaka 17 kutoka Ireland Vinnie Leonard. (Football Insider)

Aston Villa wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Dani Ceballos, 29, baada ya kukosa kumsajili Conor Gallagher. (Talksport)

Tottenham wanatafuta njia za kumuuza mshambuliaji wa Argentina Alejo Veliz, 22, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Rosario Central na wako kwenye mazungumzo na klabu ya Bahia ya Brazil. (Athletic - Subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Silva

Galatasaray, Napoli, Juventus na vilabu nchini Saudi Arabia vinamfuatilia kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 32, ambaye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Manchester City na bado kukubaliana kuongeza muda. (Caught Offside),

Wolves wanatumai kuwashinda mahasimu wengi wa Premier League kwa vijana wawili wa Uskoti - mshambuliaji wa Dundee United Kai Hutchinson, 15, na kiungo wa kati wa Aberdeen Cooper Masson, 17. (TeamTalks)

Sheffield United wamesajili nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Ross Barkley, 32, ambaye anatatizika kwa muda wa kawaida wa kucheza Aston Villa. (Football Insider)