Moja kwa moja, Marekani yasema 'kiwango cha mashambulizi dhidi ya Iran kitaongezeka' huku Israel ikishambulia Beirut na Tehran

Rais Donald Trump amesema kuwa Marekani inashambulia mifumo ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Iran "kila saa moja".

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Marekani na Venezuela kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya Maduro kukamatwa

    Rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Doug Burgum walikubaliana kufanya kazi pamoja kuendeleza shughuli ya uchimbaji madini nchini Venezuela wiki hii.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Doug Burgum walikubaliana kufanya kazi pamoja kuendeleza shughuli ya uchimbaji madini nchini Venezuela wiki hii.

    Marekani na Venezuela zimekubaliana kurejelea tena uhusiano wa kidiplomasia na kibalozi.

    Taarifa zinasema pande hizo mbili zitafanya juhudi za pamoja ili kukuza utulivu, kuunga mkono ufufuaji wa uchumi na kuendeleza maridhiano ya kisiasa.

    Wakati uhusiano wao wa kidiplomasia umekuwa ukiimarika tangu jeshi la Marekani lilipomkamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro mwezi Januari katika shambulio la kushtukiza, kutangazwa kwa uhusiano rasmi wa nchi hizo mbili kunaashiria hatua kubwa.

    Rais Donald Trump aliamuru wanajeshi kumkamata Maduro na mkewe, na kuwafikisha katika mahakama ya Manhattan kujibu mashtaka ya kutumia silaha na dawa za kulevya, madai ambayo wanayakanusha.

    Soma pia:

  2. Ukraine yaishutumu Hungary kwa kuwateka raia wake saba

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha

    Chanzo cha picha, Re

    Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine ameishutumu Hungary kwa kuwashikilia mateka wafanyakazi saba wa benki ya serikali ya Ukraine huko Budapest.

    Andrii Sybiha amechapisha kwenye mtandao wa X, kuwa Waukraine hao walikuwa safarini kupitia Hungary kwa gari wakibeba fedha kutoka Austria kwenda Ukraine, wakati walipokamatwa.

    Amesema hadi sasa haijulikani mahali walipo wala sababu za kukamatwa kwao hazijulikani, na kuishutumu Hungary kwa kuiba fedha na ugaidi unaofanywa na serikali.

    Hungary - ambayo ina uhusiano wa karibu na Urusi - bado haijatoa tamko lolote.

    Hapo awali, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alimkosoa Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban kwa kuzuia msaada wa Ulaya kwa Kyiv.

    Orban ameishutumu Kyiv kwa kuweka "kizuizi cha mafuta" kwa Hungary na kuchelewesha makusudi kufunguliwa tena kwa bomba la Druzhba.

    Maelezo zaidi:

  3. Hezbollah yawataka raia wa Israel kuondoka karibu na mpaka wa Lebanon

    Israel imefanya mashambulizi zaidi ya 1,000 ya anga dhidi ya Lebanon katika muda wa siku mbili zilizopita

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Israel imefanya mashambulizi zaidi ya 1,000 ya anga dhidi ya Lebanon katika muda wa siku mbili zilizopita

    Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran linawataka raia wa Israel wanaoishi miji iliyo umbali wa kilomita 5 kutoka mpaka wa Lebanon kuondoka.

    Onyo hilo limewekwa katika ujumbe kwenye chaneli yake ya Telegraph kwa Kiebrania mapema Ijumaa, kulingana na shisrika la habari la Reuters.

    "Uvamizi wako wa kijeshi dhidi ya mamlaka ya Lebanon na raia wake, uharibifu wa miundombinu ya kiraia na kampeni ya kuwafukuza raia hautapita bila kupingwa," Hezbollah ilisema.

    Jeshi la Ulinzi la Israel, IDF, lilianza wimbi la mashambulizi dhidhi ya Lebanon ya Alhamisi jioni, baada ya kuwaambia watu waondoke maeneo ya kusini mwa mji mkuu wa Beirut, ambayo ni ngome ya Hezbollah.

    Muda mfupi uliopita, IDF pia ilisema imeanza "wimbi kubwa la mashambulizi dhidi ya miundombinu ya utawala wa kigaidi wa Iran mjini Tehran".

    Maelezo zaidi:

  4. Marekani yazamisha zaidi ya meli 30 za kivita za Iran

    .

    Chanzo cha picha, White House

    Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani, Admiral Brad Cooper, anasema kuwa Marekani imezamisha zaidi ya meli 30 za Iran kufikia sasa.

    Aliongeza, "Katika saa chache tu zilizopita, tuliishambulia meli ya kubeba ndege zisizo na rubani ya Iran ambayo ukubwa wake ni sawa na ile iliyobeba ndege za kivita wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Sasa inawaka moto."

    Cooper amesema kuwa Marekani imeshambulia kwa mabomu takriban maeneo 200 nchini Iran katika muda wa saa 72 zilizopita.

    Huku hayo yakijiri afisa wa Ikulu ya White House ameithibitishia BBC kwamba maafisa wa utawala wa Trump wanapanga kukutana na wasimamizi wa ulinzi wa Marekani leo Ijumaa, kujadili utengenezaji wa silaha.

    Mkutano huo utafanyika katika Ikulu ya White House na utahudhuriwa na kampuni kama vile Lockheed Martin & RTX, kampuni mama ya Raytheon, shirika la habari la Reuters liliripoti hapo awali.

    Majadiliano yanatarajiwa kujumuisha kuongeza kasi ya utengenezaji wa silaha, huku Pentagon ikiwa mbioni kujaza tena hifadhi yake silaha ya baada ya shambulio dhidi ya Iran kulingana na Reuters.

    Katika mkutano na waandishi wa habari muda mfupi uliopita, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema Marekani ina silaha nyingi na inaweza kuendeleza operesheni yake dhidi ya Iran hadi itakapofikia lengo lake.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Marekani yasema 'kiwango cha mashambulizi dhidi ya Iran kitaongezeka' huku Israel ikishambulia Beirut na Tehran

    Trump

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa wa Marekani Donald Trump na Waziri wake wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth wameikosoa hatua ya Uingereza kwa kukataa vituo vyake vya kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati kutumiwa kuishambulia Iran.

    Trump hapo awali aliangazia kile kinachoendelea nchini Iran katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House.

    Kwa upande wake Hegseth alisema kwa "bahati mbaya "Uingereza ilikataa ombi letu "kutoka siku ya kwanza".

    "Lakini tulifikia lengo letu. Tulifika huko, na hiyo sasa ni sehemu ya mpango ambao tunatumia kufanya mashambulizi ya angani...Ni vikosi zaidi vya wapiganaji, ni uwezo zaidi, ni uwezo wa kujilinda zaidi, na ni mashasmbulizi ya mara kwa mara," alisema.

    "Kiwango mashabulizi dhidi ya Iran na Tehran kinakaribia kuongezeka kwa kasi," alisema.

    Hegseth pia alisema Marekani na Israel zinawalenga wale waliokuwa wakiwakandamiza waandamanaji nchini Iran.

    "Kadiri unavyofanya hivyo zaidi, kuharibu nia na uwezo wao, ndivyo unavyotengeneza fursa kwa watu kusimama kwa ujasiri," Hegseth alisema.

    Melezo zaidi:

  6. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja. Leo Ijumaa 06/03/2026