Ulimwengu wa kiarabu: Je waraabu wanaipuuza dini?

Waarabu wanazidi kusema kuwa hawana dini tena, kwa mujibu wa utafiti mkubwa na wa kina uliofanywa wa eneo la mashariki ya kati na Afrika kaskazini.
Utafiti huo ni mmoja kati ya baadhi kuhusu namna waarabu wanahisi kuhusu masuala tofuati, kuanzia haki za wanawake na uhamiaji, usalama na mahusiano.
Zaidi ya watu 25,000 walihojiwa katika utafti huo - uliofanywa kwa niaba ya BBC News Arabic na kituo cha utafiti cha Arab Barometer research network - katika nchi 10 na maeneo ya Palestina kati ya mwisho wa mwaka 2018 na 2019.
Haya ndio baadhi ya matokeo:

Tangu 2013, idadi ya watu katika eneo hilo waliojtambulisha "kutokuwa na dini" imeongezeka kutoka 8% hadi 13%. Ongezeko hilo ni kubwa katika watu wenye umri wa chni ya miaka 30, miongoni mwao 18% walijitambulisha kutokuwa na dini, kwa mujibu wa utafiti huo.
Ni yemen pekee ilioshuhudia kushuka kwa kiwango katika kitengo hicho.

Watu wengi katika eneo hilo wameunga mkono haki ya wanawake kuwa waziri mkuu au rais. Algeria pekee ndio iliyokuwa na kiwango cha chini ambapo chini ya 50% ya waliohojiwa walikubali kuwa rais mwanamke anakubalika.
Lakini linapokuja suala la maisha nyumbani - wakiwemo wanawake wengi - wanamini kuwa waume ndio wanapaswa kuwana uamuzi wa mwisho kuhusu masuala ya familia.
Ni nchini Morocco pekee ambapo chini ya nusu ya raia wanadhani mume ndio daima anayepaswa kufanya maamuzi.

Suala la kukubalika kwa mapenzi ya jinsia moja lina mgawanyiko wa namna linavyopokewa lakini pia liko chini katika eneo zima. nchini lebanon kwa mfano, licha ya kuwana sifa ya kuwa na uhuru zaidi kijamii kuliko mataifa jirani, ni 6% pekee wanaolikubali hilo.
Mauaji ynayotekelezwa kutunzai heshima ya familia, kabila au jamii ambapo familia iko radhi imuue jamaa yao kwa hilo, sanasana wanawake, wanaotuhumiwa kuiviunjia familia heshima.


Kila eneo lililofanyiwa utafiti limetaja sera za Donald Trump kwa eneo la mashariki ya kati mwisho walipolinganisha viongozi hawa. Kwa utofauti, kati ya matiafa 11 yaliohojiwa 7 nusu au zaidi yake wanaridhia muelekeo wa rais wa Uturuki President Recep Tayyip Erdogan.
Lebanon, Libya na Misri zimeorodhesha sera za Putin mbele ya zile za Erdogan.


Idadi jumla za matiafa hazijumlishi 100 kwasababu 'Sijui' na 'Akataa kuitikia' hazikujumuishwa.
Bado kuna wasiwasi kuhusu usalama kwa wengikatika enoe la mashariki ya kati na Afrika kaskazini. walipoulizwa ni nchi gani zilizo na tishio kubwa kwa utulivu na usalama wa mataifa yao, baada ya Israel, Marekani imetajwa kuwa ya pili kwa tishio kieneo na Iran ya tatu.

Katika kila eneo ambako wakaazi walilohojiwa, utafiti umeashiria kuwa angalau mmoja kati ya watano wanatafakari kuhama kabisa kutoka mataifa yao. Nchini Sudan ilikuwa nusu ya raia walioko nchini humo.
sababu za kiuchumi zilitajwa pakubwa kama chanzo kikuu.
Washiriki walikuwa wanaweza kuchagua zaidi yanchi moja.
Idadi ya watu wanaofirikia kuhama kutoka Afrika kaskazini imeongezeka, na wakati sio wengi wanavutiwa na Ulaya kuliko ilivyokuwa bado linasalia kuwa eneo kuu kwa watu wanaofikiria kuondoka katika maeneo yao.
Imetengenezwa na Becky Dale, Irene de la Torre Arenas, Clara Guibourg, na Tom de Castella.

Mbinu iliyotumika
Utafiti umetekelezwa na taasisis ya utafiti, Arab Barometer. Ni watu 25,407 waliohojiwa ana kwa ana katika matiafa 10 na maeneo ya Palestina.
The Arab Barometer ni taasisi ya utafiti iliopo chuo kikuu cha Princeton. Imekuwa ikifanya utafiti kama huu tangu 2006. mahojiano ya dakika 45 yaliofanyika kwa ukubwa kupitia tabiti yalifanywa na watafiti na washirika katika maeneo ya kibinfasi.
Ni maoni ya watu katika nchi za kiarabu, kwahivyo hazijumuishi maoni kutoka Iran au Israel, licha ya kwamba inajumuisha maeneo ya Palestina. Baadhi ya mataifa katika eneo hilo yamejumuishwa lakini serikali kadhaa za ghuba zilikataa kufikia kikamilifu na kwa haki utafiti huo. Matokeo ya Kuwait yalichelewa kuweza kujumuishwa katika taarifa ya BBC Arabic. Syria haikuweza kujumuishwa kutokana na ugumu wa kulifikia eneo hilo.
Kutokana na sababu za kisheria na kitamaduni baadhi ya mataifa yaliomba baahdi ya maswali yaondolewe. Ylioondolewa yamejumuishwa katika kutangaza matokeo, kwa kujumuisha ufafanuzi wa wazi wa ambayo hayakujumuishwa.
Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu mbinu iliyotumika katika mtandao wa Arab Barometer.













