Madhila ya mayaya wanaotafuta kazi katika nchi za kiarabu
Mataifa mengi ya Afrika na Asia yamepiga marufuku watu kufanya kazi za majumbani katika mataifa ya kiarabu wanaojisajili katika mfumo wa "kafala". Katika mfumo huo, mayaya huingia katika mkataba na mwajiri na wana haki chache mno.
Waajiri huwanyanyasa wanawake wengi, kwa kuwafanyisha kazi kupita kiasi, huwalipa fedha kidogo na kuwanyanyasa kimwili. Ushahidi wa wanawake walioponea via hivi unaonyesha kushindwa nguvu, na unyanyasaji unaendelea nyuma ya milango.
Ndio makala ya wiki hii ya BBC Africa Eye

