Uchaguzi2019 DRC: Marekani yawawekea vikwazo maafisa wa tume ya uchaguzi DR Congo

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Marekani imewawekea vikwazo maafisa watatu wa tume ya uchaguzi nchini DR Congo pamoja na wale wa serikali ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Joseph kabila kwa tuhuma za ufisadi.
Taarifa iliochapishwa katika mtandao wa wizara ya fedha nchini Marekani, inasema kuwa watatu hao walidaiwa kula rushwa ili kuzuia na kuchelewesha maandalizi ya uchaguzi wa haki na ulioshirikisha pande zote.
Watatu hao ni rais wa tume ya uchaguzi nchini DRC Corneille Yobeluo Nangaa (Nangaa), naibu wake Norbert Basengezi Katintima (Katintima), na mwanawe Katintima, Marcellin Basengezi Mukolo (Basengezi), ambaye ni mshauri mkuu katika tume hiyo ya uchaguzi CENI.
Kulingana na taarifa hiyo iliotiwa saini na katibu wa maswala ya ugaidi na intelijensia ya kifedha nchini Marekani Sigal Mandelker, watuhumiwa hao walifanya vitendo ambavyo vilikandamiza mikakati ya kidemokrasia au taasisi zake nchini DRC.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
''Hii leo idara ya fedha inayosimamia mali ya kigeni OFAC imewawekea vikwazo maafisa watatu wakuu wa tume ya uchaguzi nchini DR Congo CENI kwa kukandamiza demokrasia nchini DRC'', ilisema taarifa hiyo.

Matokeo ya Uchaguzi huo uliompatia ushindi rais aliyeko madarakani Felix Tshisekedi ulipingwa na jamii ya kimataifa ikiwemo Marekani pamoja na mpinzani mkuu wa Joseph kabila katika uchaguzi huo Martin fayulu.
Matokeo yaliyotangazwa na CENI:
- Felix Tshisekedi 7,051,013 (38.57%)
- Martin Fayulu Madidi 6,366,732 (34.83%)
- Emmanuel Shadary 4,357,359 (23.84%)
*Waliojitokeza kupiga kura kwa mujibu wa CENI ni 47.56%.
Katika taarifa hiyo Marekani imesema kuwa inaunga mkono hatua ya raia wa DR Congo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo wa Disemba 30 licha ya kuwa bado ina wasiwasi kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi huo ambapo inaishutumu tume ya uchaguzi nchini humo CENI kwa kushindwa kuhakikisha kuwa matokeo ya kura hiyo ni sambamba na matakwa ya raia hao.
Imesema kuwa Marekani itaendelea kuwasaidia wale walio tayari kukabiliana na ufisadi lakini haitasita kuwachukulia hatua kali wahusika wanaokandamiza mchakato wa kidemokrasia na kuendeleza ufisadi nchini DRC na ulimwenguni kwa jumla.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 3
Imeongezea kwamba chini ya uongozi wa rais wa tume ya uchaguzi CENI Corneille Yobeluo Nangaa, uchaguzi uliotarajiwa kufanyika Disemba 2016 uliahirishwa hadi Disemba 2018 kwa kisingizio cha kuwepo kwa haba wa fedha mbali na kuchelewa kwa usajili wa watu.

Matumizi mabaya ya fedha za uchaguzi
Akiwa mkuu wa CENI afisa huyo alidaiwa kufuja na kutumia vibaya fedha za uchaguzi huo mbali na kuchukua hatua zilizochelewesha kimakusudi usajili wa wapiga kura, hatua iliochelewesha uchaguzi huo.
Vivile chini ya uongozi wa rais huyo maafisa wa CENI walidaiwa kutumia kampuni kadhaa za mafuta kufuja fedha za operesheni za tume hiyo kwa malengo yao ya kibinafsi pamoja na yale ya kisiasa.
Maafisa hao walidaiwa kujitajirisha kupitia ununuzi wa petroli hatua iliochelewesha usajili wa wapiga kura katika eneo la Kasai likiwa eneo lenye wafuasi wengi wa upinzani na hivyobasi kusababisha wapiga kura wengi kutosajiliwa.
Aidha maafisa hao wanatuhumiwa kuongeza hadi $100m gharama ya mashine za kupigia kura kwa lengo la kujinufaisha kibinafsi, kutoa rushwa na kuchangisha fedha za kampeni ya mgombea wa rais wa zamani Joseph Kabila.
Mustakabali wa uchaguzi huo ulizidi kuingia dosari baada ya tume ya uchaguzi kutangaza kuahirishwa kwa upigwaji kura katika mikoa mitatu hadi mwezi machi 2019.

Kucheleweshwa kwa uchaguzi
Kura hiyo ambayo ilitakiwa kupigwa Disemba 23 mwaka uliopita iliahirishwa kwa wiki moja hadi Disemba 30,.
Uchaguzi huo ulikuwa tayari umescheleweshwa kwa miaka , huku wapinzani na wanaharakati wakimlaumu rais amalizaye muda wake Joseph Kabila kwa kutafuta visingizio kusalia madarakani.
Mgombea wa chama tawala Ramazani Shadary ni mshirika mkubwa wa Kabila na alitarajiwa kuendelea kulinda maslahi ya Kabila akiwa madarakani.
Maeneo hayo matatu ambayo yanaonekana kuwa ni ngome za upinzani ni Beni na Butembo kwa upande wa mashariki ambayo yamekuwa yakipambana na milipuko ya ugonjwa hatari wa Ebola toka mwezi Agosti mwaka huu.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Eneo la tatu ni Yumbi lilopo magharibi mwa nchi ambapo watu zaidi ya 500 waliuawa katika makabiliano ya kikabila.
hatahivyo msemaji wa Tume huru ya uchaguzi Jean Pierre Kalamba, kupitia barua iliyotiwa saini na tume hiyo amekanusha tuhuma hizo za rushwa na kuongeza kuwa ilifanya kazi nzuri ya kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa njia ya amani.
Bwana Kalamba aliahidi kutoa ripoti ya maandalizi ya uchaguzi kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka huu.

Kwa upande wake Lambert Mende ambaye alikuwa msemaji wa serikali ya Joseph Kabila alisema vikwazo hivyo havitakuwa na mafanikio yoyote.
Marekani vilevile iliwawekea vikwazo vya usafiri maafisa wa kijeshi na maafisa wa serikali wanaoamnikia kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu na kuhujumu mchakato wa uchaguzi nchini D.R.C.
''Maafisa hawa walinufaika kutokana na ufasadi, au kuwazuia watu kuandamana na kuwanyima uhuru wa kujieleza.''iliongeza taarifa hiyo.