Uchaguzi DRC: Kwa nini uchaguzi wa mwaka huu DR Congo ni muhimu
Joseph Kabila ametawala siasa za DR Congo kwa miaka 17 iliyopita. Alichukua hatamu baada ya babake kuuawa na mlinzi wake mwaka 2001.
Uchaguzi mkuu uliokuwa umepangiwa kufanyika mwaka 2016 ulicheleweshwa kwa miaka miwili.
Lakini sasa unafanyika akiwa hayupo kwenye karatasi za kupigia kura. Kwa hivyo, uchaguzi ukiendelea kutakuwepo na kiongozi mpya.