Kwa Picha: Kituo kipya cha uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Tanzania chafunguliwa

Kwa Picha: Kituo kipya cha uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Tanzania
Muda wa kusoma: Dakika 3

Rais wa Tanzania, John Magufuli amefungua jengo la tatu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Abiaria waanza kuhudumiwa

Hii ni ishara ya safari Mpya ya Tanzania kujizatiti kukabiliana na ushindani katika soko La biashara ya usafiri wa anga.

Uwanja huu ambao sasa unaweza kupokea watu millioni sita kwa mwaka, umejengwa kwa gharama ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 300, ujenzi ulioanza mwaka 2013.

Abiria wa kimataifa wanahudumiwa

Jengo hilo litakuwa likitumiwa na abiria wanaokwenda na kutoka nje ya Tanzania.

Raisi Magufuli amesema kukamilika kwa jengo hilo kutachangia kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.

Raisi wa Tanzania Dokta John Magufuli

Amesema katika majengo mawili yaliyopo hadi sasa, moja lina uwezo wa kuhudumia abiria 500,000 na la pili abiria milioni 1.5 huku hilo la tatu likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

"Jengo hili nimeambiwa linaweza kuhudumia abiria 2,800 kwa saa, haya ni maendeleo makubwa sana kwa Taifa na limegharimu zaidi ya Sh710 bilioni. Ninamshukuru Jakaya Mrisho Kikwete (rais mstaafu) kwa kuanzisha mradi huu," amesema Rais Magufuli.

Kituo hicho kipya cha muundo wa kisasa

Huku akisisitiza kuwa jengo hilo pamoja na miradi mingine mikubwa nchini ni ya Watanzania amesema, "Watanzania tunaweza kama tutaamua na kuthubutu, tumeamua na tunaendelea kuamua. Ni heshima ya mradi huu uende kwa Watanzania wenyewe na miradi yote inayotekelezwa ni ya Watanzania."

Rais Magufuli na waziri mkuu majaliwa katika jengo hilo jipya

"Nataka kuwaambia kujiita masikini tukutupe, nchi yetu ni tajiri ila tulitaka kuaminishwa na watu waliotaka kujimilikisha. Kila palipo na nia Mungu yupo na ndugu zangu watanzania Mungu yupo pamoja na sisi."

Watu wakishangilia jambo uwanjani

Jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2013 na awali ulipangwa kutekelezwa kwa Sh705.3 bilioni lakini kutokana na kubadilika kwa taratibu za kikodi, mchoro wa mradi , gharama ya mradi huo iliongezeka kwa Sh85.3 bilioni.

Baadhi ya watanzania wanaonekana kupokea kwa furaha uzinduzi huu.

Tukio hili linakuja ikiwa siku kadhaa zilizopita shirika la ndege la Tanzania likiwa limeanza Safari zake zakimataifa na kunuia kupanua wigo zaidi.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 3

Sasa Tanzania inatarajia kupokea mashirika ya Ndege mpya zitakazokuwa zinatua katika uwanja huo.

Eneo la wageni kuondoka

Wakati mradi unaanza ulitarajiwa ungekamilika Desemba 2017, baadaye ukaongezewa mwaka mmoja hadi Desemba 2018, lakini haukukamilika badala yake umekamilika Mei, 2019.

Kituo hicho kinalenga kuwahudumia abiria wengi zaidi

Kampuni iliyotekeleza mradi huo ni BAM International ya Uholanzi ambayo ndiyo iliyofanya kazi za ukandarasi na kampuni ya Arab Consulting Engineers (ACE) ya Misri, ilifanya kazi za ushauri.