Mwanajeshi wa Korea Kaskazini atorokea Korea Kusini baada ya kuvuka mpaka

Wanakjeshi wa Korea Kusini wanapigia doria karibu na uzio wa eneo hilo la mpakani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eneo la mpaka huo linalindwa na maelfu ya wanajeshi kutoka pande zote mbili.

Korea Kusini inamzuia mwanajeshi wa Korea Kaskzini ambaye alivuka mpaka unaolindwa sana na wanajeshi na ambao unagawanya mataifa hayo mawili.

Aligunduliwa akivuka mpaka huo usiku , alisema mkuu wa majeshi ya Korea Kusini.

Mtu huyo ambaye hajatambuliwa alikuwa mwanajeshi ambaye alikuwa na hamu ya kuhamia Seoul, alisema mkuu huyo.

Makumi ya watu hutoroka Korea Kaskazini kila mwaka lakini utorokaji kupitia kuvuka mpaka wa mataifa hayo mawili ni hatari na sio swala la kawaida.

Mnamo mwezi Novemba 2017, mwanajeshi wa Korea Kaskazini alipigwa risasi mara 40 na wanajeshi wenzake alipokuwa akivuka mpaka huo kutorokea Korea Kusini.

Katika kisa cha hivi karibuni , mtu huyo alionekana mwendo wa saa sita siku ya Jumatano karibu na mto Imjin , ambao maji yake hutoka Korea Kaskaizni na kuelekea Korea Kusini kupitia mpaka huo unaollindwa sana magharibi mwa rasi ya Korea. Alikamatwa na wanajeshi wa Korea Kusini na kuzuiliwa

Mwanajeshi akitoroka Korea Kaskazini

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora mawili ya masafa mafupi.

Chombo cha habari cha Korea Kaskazini kilisema uzinduzi huo uliosimamaiwa na rais Kim Jong un ulikuwa ni kufanyia majaribio makombora hayo .

Majaribio hayo yalikuwa onyo kwa Korea Kusini kuhusu zoezi la kijeshi la pamoja na Marekani linalotarajiwa kufanyika mbaadaye mwaka huu , kulingana na Korea kaskzini.