Iraq: Mama alazimika kuchagua kati ya mwanawe mume wake ambaye ni mpiganaji wa IS na familia yake

Mother cuddling her child

'Jovan' alikuwa akiishi kwa raha na mume wake na watoto wao watatu katika kijiji cha jamii ya Yazidi nchini Iraq.

Wanamgambo wa Islamic State walipovamia kijiji hicho alitekwa na kupelekwa katika soko ya watumwa ambapo aliuzwa kwa mpiganaji wa kundi hilo - na kuzaa nae.

Wote wawili waliponea mashambulizi ya "wanamgambo" lakini alilazimika kuchagua kati ya familia yake ya Yazidi na mtoto wake mchanga.

Adam alikuwa mtoto mwenye na nywele rangi na macho rangi tofauti. Hakufanana na ndugu zake. "Nilimpenda punde nilipomsikia akilia kwa mara ya kwanza," mama yake Jovan anasema. Alikuwa mwanga gizani.

Lakini baba ya Adam alikuwa mtekaji wake na sasa hana budi kumpeana.

Jovan alifuraihia sana maisha, aliishi na mume wake Khedr na watoto wao watatu katika kijiji kizuri ambacho walikulia tangu utotoni.

Watoto walipolala walitoka nje kimya kimya kujionea mandhari ya kupendeza ya anga iliyojaa nyota za kuvutia kwa jinsi zilivyong'aa.

"Nilikuwa na raha sana," Jovan anasema. "Niiishi maisha mazuri kadri ya uwezo wangu."

Lakini maisha hayo yalibadilika kabisa msimu wa kiangazi wa mwaka 2014. Siku moja mwanzoni mwa mwezi Augosti, muda mfupi baada ya kula chakula cha mchana, gari mbili zilizokuwa zimefungwa bendera nyeusi ziliwasili katika kijiji chao.

Mji wa Sinjar, Februari 2015.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bonde la Sinjar

Jovan na Khedr hawakua na uhakika kilichokuwa kikifanyika lakini walifahamu fika wapo hatarini.

Ni wazi kwamba wanaume hao walikuwa wapiganaji hatari wa kundi la Islamic State (IS).

Lakini wakati mwingine nyoso zao zilitambuliwa na ilibainika wanatokea - kijiji jirani na Khedr aliwafahamu. Wanaume hao waliwaahidi kuwa hawatawadhuru bora washirikiane nao.

Familia yao na zingine 20 zililazimishwa kujiunga na msafara kutoka kijiji kimoja hadi kingine katika bonde la Sinjar.

Kile kitu ambacho hawakujua ni kwamba kulikua na mpango wa IS kuwashambulia kutoka pande zote za mpaka wa Iraq na Syria.

Mwanzo wa mwaka, Kundi hilo liliteka miji iliyopo karibu na Baghdad. Mji wa Mosul, ambao ulikuwa karibu na kijiji cha Jovan na Khedr, pia ulitekwa miezi mitano baadae. Sasa IS wameanza tena ajenda yao.

Habari zilisambaa haraka katika vijiji vilivyopo karibu, na hatimae msafara uliposalia na karibu nusu saa kuwasili, wanavijiji wengi walikua wametorokea nyanda za juu za mlima wa Sinjar.

Mwezi Agosti mwaka 2014, Umoja wa Mataifa ulielezea tukio hilo kama wakati ambapo maisha yalitokomezwa Kaskazini mwa Iraq na mwanzo wa ukatili dhidi ya binadamu.

Kiongozi wa msafara alimwambia Khedr kwenda milimani kuwashawishi wanavijiji kurejea nyumbani - na kwamba hawakuwa na mpango wa kuwadhuru.

Maelfu ya watu wengi wao kutoka jamii ya Yazidis, walianza kutoroka kutoka mlima Sinjar Kaskazini mwa Iraq na mji wanZakho city kuelekea milima iliopo karibu upande wapili wa mpaka nchini Uturuki kwa kuhofia kushambuliwa na makundi yaliyojihami yanayoongozwa na Islamic State (IS), Mwezi Augosti 2014.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanavijiji walikimbilia milimani kujificha wasishambuliwe na IS

"Tuliwasilisha ujumbe huo lakini hakuna mtu aliyeamini," Khedr anasema. Mmoja wa wale waliotorokea milimani alikuwa ndugu yake.

Khedr alitaka familia yake irejee nyumbani lakini ndugu yake alipinga wazo hilo akihoji hatari inayowakabilia.

Wanamgambo wa IS wanafahamika kwa kuwachukua kwa nguvu wanaume na kuwatumia kuwaua watu kwa niaba yao.

Khedr, sawa na mke wake alikuwa na hofu hususan kuhusu jamii ya kidini ya -Wayazidi

Hawakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yoyote, wale waliotorokea mlima Sinjar walikwama huko bila maji wala chakula na mamia ya wengine walifariki kutokana na baridi kali.

Maelfu ya Wayazidi waliosalia chini ya mlima huo walitekwa na wanamgambo wa IS.

Familia zilitenganishwa na wavulana walilazimishwa kujiunga na kundi hilo la kigaidi na kupewa mafunzo katika kambi zao huku wanawake na wasichana wakitumikishwa kama watumwa wa nkingono.

Wanaume waliokataa kujiunga na dini ya Kiislam waliuawa.

Hakuna mtu aliye na uhakika ni Wayazidi wangapi walitekwa nyara na wanamgambo wa IS.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anakadiria kuwa Wayazidi 400,000 walikuwa wakiishi mjini Sinjar wakati huo na kwamba maelfu ya watu waliuawa na zaidi ya 6,400 walikuwa Wayazidi- wengi wao wanawake na na watoto -ambao walifanywa watumwa, wengine walibakwa, kupigwa na kuuzwa.

Jovan, na watoto wake watatu na karibu wanawake na watoto 50 katika kijiji hicho waliingizwa kwenye lori na kusafirishwa hadi mji wa Raqqa nchini Syria - ambao ulikua makao makuu ya kundi la IS.

"Hatukuweza kufanya lolote kujilinda," anasema Jovan. Hakuruhusiwa kumuona tena Khedr kwa miaka mingine minne.

Kuzuiliwa

Illustration of a woman held captive

Jovan baadae alibaini sehemu aliyopelekwa ilikuwa Soko la watumwa mjini Raqqa.

Yeye na watoto wake walizuiliwa katika nyumba ya ghorofa tatu iliyojaa wanawake na watoto -karibu 1,500 walikuwa hapo.

Jovan anasema aliwafahamu baadhi ya wanawake hao- walikuwa jamaa zake na wengine majirani kutoka vijiji tofauti.

"Tunajaribu kufarijiana kwa kupeana matumaini kwamba muujiza unaweza kufanyika tukaachiliwa," anasema.

Badala yake, Jovan alilazimishwa kuamua anataka kupeanwa kwa kundi lipi la wanamgambo wa IS. alipewa mwanamume wa Kitunisia aliyepewa jina la utani la Abu Muhajir al Tunisi, kamanda wa ngazi ya juu- ambaye alikuwa mdogo, mwembamba na mwenye madevu yaliyowekwa nadhifu.

Mwanmgambo wa IS nchini Syria, Septemba 2014

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamgambo wa IS nchini Syria, Septemba 2014

Jovan alitarajiwa kujiunga na dini ya Kiislam na baadae "kuolewa" nae.

Alilia kwa siku kadhaa. Alijaribu kutoroka mara tatu, lakini watoto wake walitibua mpango huo kwasababu walikuwa wadogo - Haitham, aliyekuwa mkubwa, alikuwa na miaka 13, lakini Azad, ambaye ndiye mdogo alikuwa na miaka mitatu.

Kila alipojaribu kutoroka Abu Muhajir aligundua njama yake na kumfungia katika chumba kimoja.

"Nilitamani kujitoa uhai lakini nilipofikiria mateso watakayopitia watoto wangu nabadili nia,pia niliwaza kuwaacha nitoroke lakini nilishindwa kufanya hivyo kabisa"

Hatimae Jovan hakuwa na budi kujiunga na dini ya Kiislamu. Hatma yake ilikomea hapo.

Jovan aliathiriwa vibaya kiakili na hapendi kusimulia aliyopitia mikononi mwa mtekaji wake. Lakini anasema kuwa alimruhusu kusalia na watoto wake na kuahidi kuwatunza wote.

Watoto wengi wa Wayazidi walitenganishwa na mama zao- Wavulana walipelekwa katika kambi ya mafunzo ya kijeshi na wasichana walifanywa watumwa wa kingono na wafanyikazi wa nyumbani.

Jovan, watoto wake na mwanamume wa Kitunisia walihamia nyumba fulani mjini Raqqa ambayo mwenyewe alitoroka.

Kufikia wakati huo IS walikuwa wanadhibiti maeneo mengi nchini Iraq na Syria -eneo ambalo lilingana kwa ukubwa na Uingereza, kwa mujibu wa kituo cha Kitaifa cha Marekani cha kukabiliana na Ugaidi.

Map showing Raqqa, Mosul and Sinjar

Asipokuwa katika mapigano, Mtunisia huyo alitimiza ahadi yake ya kuwatunza vizuri Jovan na wanawe, kwa kuwapeleka kucheza katika bustani moja dogo karibu na nyumbani.

Hata hivyo katika miezi mitano ya kwanza ya mahusiano yao, Jovan aligundua amepata ujauzito.

"Hapakua na dawa na sikujua la kufanya," Jovan anasema.

Vikosi vinavyoongozwa na Marekani vilikuwa vikishambulia kwa mabomu ya angani maeneo yanayokaliwa na wanamgambo wa IS karibu kila siku.

Wapiganaji wa Iraq na wale wa Kikurdi waLifanya mashambulizi ya ardhini katika mipaka ya Syria na Iraq.

Mtekaji wa Jovan wakati mwingi alikuwa vitani hadi wakati mmoja akaamua kumuuza kwa mfuasi mwingine wa IS.

Mateka wa Yazidi walikuwa wakiuzwa mara kwa mara lakini alipogundua Jovan ni mjamzito alibadili mpango wa kumuuza.

Akiwa na ujauzito wa miezi saba, Jovan alipata habari kuwa Abu Muhajir ameuawa vitani.

Jukumu la kuwalea watoto sasa limesalia kuwa lake peke yake .

Adam alizaliwa wakati Raqqa ilikuwa ikishambuliwa karibu kila siku na vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani.

Hawa na Haitham walimsaidia mama yao kujifungua ndugu yao wa kiume. Jovan anasema watoto hawkuwa na uhakika wamchukulie vipi ndugu yao mdogo aliyekuwa na muonekano tofauti na wao.

"Nadhani watoto walimpenda. Walimtunza vuzuri. Haswa Hawa - ni binti yangu lakini pia ni rafikia yangu mkubwa. Alimlisha Adam na kumbembeleza hadi alale."

Mashambulizi ya mara kwa mara yalimlazimisha Jovan na watoto wake kuhamia nyumba nyingine lakini maisha yalikuwa magumu sana kwao.

Chakula kilikua kidogo na wakati mwingine Jovan alilazimika kula kidogo na kuwaachia watoto.

"Wakati mwingine tulikula mkate na maji yaliyochanganywa na sukari kidogo. Nilifahamu ya kuwa nisipokula sitakuwa na maziwa ya kumnyonyesha mtoto Adam, lakini sikuwa na jinsi."

Licha ya changamoto zote alizopitia anasema mtoto Adam alimpatia ujasiri wa kuendelea na maisha.

"Nilimpenda sana. Nilifahamu baba yake hakuwa mume wangu halisi, baba yake alikuwa muuaji, lakini [Adam] alikuwa damu yangu."

Kutoroka

Money changing hands at the border

Nyumbani Iraq, Khedr hakuwa na habari kumhusu mtoto huyo na wala hakuwa na ufahamu wowote ilipo familia yake.

Ni miezi 14 tangu familia yake ilipotekwa na amekuwa akimtafuta mke wake na watoto.

Kila aliposikia kuna mwanamke na watoto wameachiliwa huru alikuwa akienda mpakani kuangalia kama ni familia yake.

Hatimae alifahamu walipo kupitia mtandao wa walanguzi wa watu uliokuwa ukinunua wanawake wa jamii ya Wayazidi na watoto kutoka kwa wanamgambo wa IS. Khedr alihitaji kutafuta $6,000 kwa kila mtoto.

Haitham, Hawa na Azad waliunganishwa na baba yao. Jovan, hata hivyo alilazimika kusalia Raqqa kwa miaka mingine miwili. Hakuwa na uhakika Khedr atamkubali Adam.

Kwa miezi kadhaa Khedr alitafakari cha kufanya. Wafuasi wa imani ya Yazidi, moja ya dini ya iliyo na waumini chini ya Milioni moja kote duniani wanatakiwa kufuata sheria maalum ya kidini.

Moja ya kanuni ya sheria hiyo ni kwamba yeyote atakayejiondoa katika dini hiyo hawezi kurudi hadi uamuzi utolewe na baraza la kidini la Yazidi hasa kwa wanawake waliotekwa kwa nguvu na IS na kuingizwa kwa dini ya Kiislamu.

Lakini kwa watoto waliozaliwa na wapiganaji wa IS hali ilikuwa tofauti kabisa. Mtu anaweza tu kuzaliwa ndani ya dini hiyo wala hawezi kujiunga nayo. Mtoto anakubaliwa nyumbani ikiwa wazazi wote wawili ni Wayazidi.

Jovan sasa alikuwa akiishi na wajane wengine wa Kiyazidi waliokuwa wameolewa na watekaji wa IS.

Wanawake wote walikuwa wakiogopa kurudi nyumbani katika kijiji cha Sinjar kwa sababu wamevunja mwiko.

"Wengine wamezaa watoto zaidi ya mmoja na wapiganaji wa IS, sasa wanaogopa kujiunga tena na familia zao,"alisema.

Khedr hatimae aliamua kuwa watoto wake wanamuhitaji mama yao, na hapo alimwambia Jovan kuwa mtoto Adam anakaribishwa.

A woman divided in three, one iteration cuddling her child

Jovan alisafiri kurudi kijijini kwao Sinjar na mwanawe Adam, miaka minne baadae. Lakini siku chache baadae hali ilibadilika.

Jovan anasema familia yake ilianza kumshawishi ampeane Adam.

"Walianza kunielezea umuhimu wa kufuata mafundisho ya kidini, na jinsi jamii haitawahi kumkubali mtoto wa Kiislamu ambaye baba yake ni mpiganaji wa IS."

Khedr Alimpeleka Jovan kukutana na Sakineh Muhammed Ali Younes, msimamizi wa makaazi ya watoto yatima mjini Mosul akitarajia kuwa atamshawishi mke wake kukubali kumuacha Adam hapo.

Sakineh anasema alitumia saa kadhaa akijaribu kumshawishi Jovan kukubali wazo hilo wakati huo anasema , Khedr alikuwa akilia kwa machungu nae Jovan alikuwa akimwangalia mwanawe Adam, akisema hawezi kumpeana.

"Machozi yalikuwa yakimtiririka alipompeana mtoto huyo. Hakuna kitu kigumu kama kumchukua mtoto wa Yazidi kutoka kwa mama yake. Ni mithili ya kukata sehemu ya roho yake," alisema.

"Lakini imani ya jamii ya Wayazidi ni muhimu kuliko matakwa ya mtu binafsi. Mimi na mume wake tumekubaliana kuwa nitamchukua mtoto wake, hata iweje. Na mwisho hatukuwa na budi kudanganya."

Sakineh alimwambia Jovan amuache Adam kwa wiki kadhaa, kwa sababu ni mgonjwa na anahitaji kupewa matibabu.

"Nilimwambia mtoto wako yuko chini ya uangalizi wangu hadi suluhisho kuhusu suala hili lipatikane."

Baadhi ya majina yamebadilishwa ili kulinda usalama wa wachangiaji.