Waumini Wakikristo wa Iraq 'wanakaribia kutoweka'

Askofu mkuu wa Irbil, mji mkuu wa jimbo la Iraq la Kurdistan, amewashutumu viongozi wa kikristo wa uingereza kwa kushindwa kufanya juhusi za kutosha kuilinda jamii ya inayotoweka ya Wakristo wa Iraq.
katika hojtuba aliyoitoa mjini London, Askofu Rev Bashar Warda alisema kuwa Wakristo wa Iraq sasa wanakabiliwa na hatari ya kutoweka baada ya miaka 1,400 ya kuuawa.
tangu majeshi ya marekani yalipovamia Iraq na kuuondoa madarakani utawala wa Saddam Hussein mnamo mwaka 2003, amesema, jamii ya Wakristo imepungua kwa 83%, kutoka watu milioni 1.5 hadi watu 250,000.
"Ukristo nchini Iraq," amesema , "ambao ni moja ya makanisa ya kale, kama si ya kale zaidi duniani, unakaribia kutoweka. Wengine wetu tuliobakia lazima tuwe tayari kukabiliana na kufia dini ."
Alikuwa anazungumzia tisho kubwa la hivi karibuni kutoka kwa wapiganaji wa jihadi wa Islamic State (IS) kuwa ni "vita vya mwisho vya wakristo", kufuatia mashambulizi ya awali ya kundi hilo mnamo mwaka 2014 yaliyowasambaratisha wakristo 125,000 kutoka makazi yao asilia.
"Wanaotutesa wanamaliza uwepo wetu ," alisema, "huku wakitaka kupangusa historia yetu na kuangamiza maisha yetu yajayo.
Nchini Iraq hakuna fidia kwa wale waliopoteza mali zao, nyumba wala biashara. maelfu kwa maelfu ya wakristo hawana la kuonyesha kuhusu maisha yao ya kazi, katika maeneo ambapo familia zao zimeishi, labda kwa miaka elfu moja.
Islamic State wanaofahamika katika ulimwengu wa kiarabu kama Daesh, walifukuzwa kutoka ngome yao ya mwisho ya Baghuz nchini Syria mwezi machi baada ya kushambuliwa na wanajeshi wengi wa mataifa mbali mbali na kusema kuwa ulikuwa ndio mweshi wa "mtawala wa kiislamu".
Kabla ya hapo, kundi la Islamc State lilikuwa limefukuzwa kutoka mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq wa Mosul mwezi wa Julai 2017.
Lakini makanisa , majengo ya kidini na nyumba za familia za Wakristo zimekuwa zikiangamizwa na maelfu ya familia hazijarejea tena.
Wiki hii Askofu mkuu ameonya juu ya kile alichosema kuwa ni ongezeko la makundi yenye itikadi kali yanayoamini kuwa mauaji ya Wakristo na Wayazidi yalisaidia kueneza Uislamu.
'Usahihi wa kisiasa'
Askofu huyo aliendelea kuwashutumu viongozi wa kikristo wa Uingereza kwa kile alichokitaja kuwa ni "usahihi wa kisiasa" juu ya suala - jambo ambalo alisema ni kushindwa kulaani itikadi kali "saratani ", akisema hawazungumzii kwa sauti ya kutosha kutokana na hofu ya kushutumiwa kwa kuwa na ubaguzi dhidi ya Uislamu.
"Utaendelea kukubali uovu ambao hauishi, mauaji ya kupangwa dhidi yetu ?"alisema. "Wakati wimbi lijalo la ghasia linaanza kutupiga, kuna hata mmoja wenu ambaye atachukua jukumu la kuitisha maandamano na kuonyesha ishara zinazosema 'Sote ni wakristo'?"

Chanzo cha picha, AFP
Maoni yake juu ya usahihi wa kisiasa yanaungwa mkono kwa kwa upande mmoja na Analogy wa Truro, Rt Rev PhilipFC Mounstephen, mbaye ni mwenyekiti wa ofisi huru ya udhibiti wa mauaji ya Wakristo Katika mataifa ya kigeni duniani.
"Ninadhani Askofu anasema ukweli kwamba utamaduni wa"usahihi wa kisiasa" umeyazuwia mataifa mataifa ya magharibi kuzungumza juu ya mauaji ya Wakristo," alisema. " Ninadhani hata hivyo hii hasa inasababishwa na hali ya kusita sita kuchukua hatua kutokana na majuto ya baada ya ukoloni ."
Askofu Mounstephen anasema kwamba mauaji ya Wakristo yanapaswa kuangaliwa kwa mtizamo mpana wa kidunia na yanatokana na sababu mbalimbali. "Tukiangalia tu kwa mtizamo wa wanamgambo wa kiislamu ," tutawaacha watu wengine ambao wanapaswa kuwajibika kwa mauaji."
Ukiangalia kwa mtizamo wa kihistoria, Askofu mkuu wa Irbil alilalamikia ukweli kwamba kwa karne nyingi kulikuwa na kipindi cha furaha cha ushirikiano uliozaa matunda miaka ya nyuma baina ya Waislamu na Wakristo nchini Iraq.
Wakati mwingine wanahistoria waliuelezea wakati huo kama Kipindi cha Dhahabu cha Uislam.
"Mababu zetu Wakristo walishirikiana na Waislamu Waarabu fikra za kitamaduni na filosofia," anasema Askofu Warda. "Walizungumza na nao katika mazungumzo yenye heshma kuanzia karne ya 8.
"Aina ya mazungumzo ya maelewano, na ambayo yalifanyika tu kwasababu ya viongozi wakuu wa dini ya kiislamu walivumilia Jamie za walio wacheche.Wakati uvumilivu ulipokwisha ,utamaduni na utajiri uliotokana nao pia ukaisha."
'Wakati wa ukweli'
Kwingineko katika Mashariki ya katika Mashariki ya Kati kuna picha tofauti kwa Wakristo mwaka 2019.
Wakoptiki wa Misti, ambao ni asilimia 10 ya raia zaidi ya milioni 100 wamekuwa wakikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa Mara kutoka kwa wanamgambo wa jihadi ambao walilipua makanisa yao na kujaribu kuwafurusha nje ya kaskazini mwa Sinai, lakini Februari Papa Francis alifanya ziara ya kihistoria ya siku tatu katika Falme za kiarabu iliyokuwa ya kwanza ya Papa kuwahi kuifanya katika rasi ya kiarabu ambayo ilihudhuliwa na Wakristo wanaokadiriwa kuwa 135,000 wengi wao wakiwa ni wahamiaji.Na nchini Saudi Arabia ambako Uislam ulizaliwa, ibada ya Kwanza ya Wakristo wa dhehebu la Coptic iliruhusiwa mwezi Disemba.Nchini Syria, Wakristo ambao ni wachache walihisi kwa tisho kubwa kutoka kwa makundi ya hususan y'all waasi wa Kiislamu. Huku vikosi vya rais Assad vikiwa vinakaribia kuondoka, kutokana na baadhi ya mashambulio ya kikatili, Wakristo wa Syria huenda wanapumua kutokana na ishara ndogo za amani. Hata hivyo nchini Iraq hali ya Wakristo bado ni tete. Uhasama baina ya Wasunni na Waislamu wa Kishia umeendelea kushamiri, na bado kuna wapiganaji wasiojulikana wa IS wanaojificha katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi.

Chanzo cha picha, Jewan Abdi
Askofu mkuu wa Warda ameelezea mambo ya kusikitisha juu ya hali ya baadae.Marafiki, tunaweza kuwa tunakabiliana na mwisho wetu katika ardhi ya mababu zetu. Tunabaini holiday. Katika mwisho Wetu, dunia nzima, inakabiliwa na kipindi cha ukweli. '' Je watu wa amani, wasio na hatia wataruhusiwa kuuawa na kuangamizwa kwasababu ya imani yao? Na kwa ajili ya kutozungumza ukweli kwa wauji, dunia itakuwa inashiriki katika kutumaliza?"












