Maelezo ya picha, Alaa ni mtoto mwenye umri wa miaka 12 akiandika lugha ya kiingereza kwenye ubao katika shule moja iliyoko katia mji mkuu wa Khartoum,Sudan
"Watu huku hawajazoea kumuona mwanamke ameshika kamera na kuzunguka katika mitaa kupiga picha lakini niliamua kuwa napiga picha ya kila nnachopendezewa nacho" mpiga picha Ola Alsheikh aeleza
Kuchekwa,kutokubalika au kudharaulika na watu wasiomjua ndio mambo ambayo Ola anakabiliana nayo kila mara katika mji huo wa Khartoum lakini alikataa kukatishwa tamaa.
"Nataka kuonesha maisha halisi ya Sudan kwa maana tumekuwa tunapewa picha za kusadikika na dunia yote kwa muda mrefu juu ya Sudan"Ola aliongeza.
Hizi ni miongoni mwa picha anazozipenda mpiga picha huyo
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, Nyama hii iliyokaushwa inaitwa Sharmoot ,ni miongoni mwa chakula kinachopendwa zaidi nchini Sudan na huwa inaliwa pamoja na uji.Picha hii inamuonesha mwanamke aliyekuwa anakausha nyama nyumbani kwake
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, "Mtindo wa nywele za binti huyu zilinivutia" Ola alisema.
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, Muuza matundar Soleiman Mohamed Toum akiuza matikitimaji,zabibu na ndizi katika duka lake lililopo kisiwani
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, "mchanganyiko wa rangi wa kijana aliyekuwa anacheza mpira wa mguu ulimvutia," Ola alisema.
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, "Kinyozi mtaani ni miongoni mwa mambo mapya ambayo yameanza kuepo mjini Khartoum," Ola anasema"Kabla kulikuwa na maduka ambayo wanaume waliweza kunyoa nywele zao lakini sasa vinyozi wapo hata sokoni,mtaani au katika vituo vya daladala".
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, Mwanamitindo Nuha Malik ni rafiki yake Ola kwa muda mrefu na picha hii inaonesha mfululizo wa picha zilizopo kwenye mtandao kwenye mtandao wa instagram zikionyesha mitindo ya nywele
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, Mchoraji Sari Awad akionesha picha aliyochora inayowasisitiza jamii kuwa na umoja na ubinadamu
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, Katika picha hii Ola anasema alipenda ukimya uliotawala siku ya ijumaa na alipenda pia muonekano wa rangi katika eneo hilo pamoja na gari.
Chanzo cha picha, Ola Alsheikh
Maelezo ya picha, "Enas Siddig ni muendesha farasi anayeiwakilisha Sudan kimataifa