Remmy Ongala: Familia yaandaa tamasha kumuenzi 'daktari wa Rhumba' Tanzania

Maelezo ya sauti, Remmy Ongala: Familia yaandaa tamasha kumuenzi 'daktari wa Rhumba' Tanzania

Ramazani "Remmy" Mtoro Ongala almaarufu Remmy Ongala alikuwa ni mwanamuziki wa Rhumba aliyepata umaarufu mkubwa kuanzia miaka ya 1970 kutokana na tungo zake ambazo zilivuta hisia za wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Mtaani Sinza, Dar es Salaam kuna eneo lililopewa jina lake.

Ni miaka 8 sasa tangu mwanamuziki huyu afariki lakini muziki wake bado unaendelea kupendwa.

Kwa mara ya kwanza familia yake imeandaa tamasha maalum la kumuenzi mwanamuziki huyo likiwashirikisha wanamuziki wengine kutoka Afrika Mashariki katika kuenzi muziki wa dansi na muziki asili.

Mwandishi wa BBC Shadrack Mwansasu ametuandalia taarifa hii.